Waraka kwa Zitto: Kigoma mjini tunaangamia

talentbrain

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,187
759
Habari yenu wanajamvi.

Bila maneno mengi naomba kuelekea kwenye mada moja kwa moja.

Kwa siku saba Kigoma mjini iliyokaribu kabisa na ziwa Tanganyika imeingia kwenye tatizo la ukosefu wa maji safi na salama yaliyokuwa yakisambazwa na KUWASA kutokana na kile kinachosemekana kuwa kukatiwa umeme na TANESCO kutokana na malimbikizo ya madeni ya umeme ya muda mrefu.

Haijawahi kutokea tatizo la maji kuwa kubwa namna hii katika uhai wangu wote. Japo awali kulikuwa na miundombinu hafifu na tatizo la umeme KUWASA ilijitahidi kutoa maji hata kwa zamu. Maeneo ambayo maji hayakuweza kufika watu wa maeneo hayo walikuwa na sehemu ya kuyafuata kwakuwa ilikuwa si mbali sana.

Kwa sasa Kigoma mjini yote haina huduma ya maji. Kwa hali ilivyo tutegemee mlipuko wa kipindundu. Wananchi hasa akina mama wanatumia zaidi ya nusu ya siku kuhangaikia maji. Watu tunatembea tunanuka jasho. Kwa wajasiliamali imekuwa ni ahueni kwao ambapo maji ambayo hayajatibiwa yanauzwa kwa 1500/= kwa dumu la lita 20. Huku ndiko tumefikia.

Wananchi wa kawaida tunabaki na mshangao tu, Ikiwa kila mwezi tunalipa bill za maji na ikizidi mwezi mmoja unakatiwa iweje KUWASA ishindwe kulipa bill zao za umeme? Kinachosikitisha zaidi ni wananchi kuteseka kwa uzembe wa watendaji na wasimamizi wa mamlaka. Tunajiuliza tatizo hili litachukua muda gani?

Mheshimiwa Mbunge wetu Mwami Ruyagwa.Tunafahamu una mambo mengi sana ya kushughulikia kitaifa, ila kumbuka tulikuchagua utatue matatizo yetu kwanza. Wewe na chama chako tuliwapa mamlaka ya kutuongoza hapa Manispaa tukiamini mtatengeneza team nzuri ya kutatua kero zetu na kutuletea maendeleo.

Ni muda sasa tunataka kuona jitihada hizo. Meya ndio msimamizi mkuu wa shughuli ndani ya Manispaa amefanya nini kutatua tatizo hili kabla halijaleta maafa? Mbunge wetu huoni sasa ni muda wa wewe kuja Kigoma kuhakikisha tatizo hili linapata ufumbuzi wa kudumu?

Nia ya waraka huu ni kueleza hali halisi na kukumbusha wajibu tuliowapa kwenye sanduku la kura. Kuna mengi mlituahidi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zetu za masingi. Tunatarajia kuona suala hili linaisha haraka na kwamba halitarudia tena. Sisi wananchi tunaoteseka kwa sasa si makosa yetu kwakuwa bills zetu tunalipa.

Kwa niaba ya wananchi wenzangu ambao tumeamua kufanya ziara ya kwenda kuoga kila siku ziwani ni mimi.

Talentbrain wa Kigoma/Ujiji
 
Poleni sana
Kama mpo Ujiji,Maweni,Katonga,Kibilizi,
Mjikamue muende ziwani lakini mkumbuke Kuchemsha maji kuliko kulialia,
Wale wa Gungu Sogeeni kwenye bwawa
Mkumbuke kuchemsha pia
Mwandiga mna mto
poleni lakini
Hizo option unazosema ni as if rahisi sana. Mtu wa maweni asiye na gari, guta, pikipiki au bajaji itamchukua masaa mangapi kupata ndoo tano kwa ajili ya matumizi madogo ya nyumbani?? Mlole nao waende wapi??
 
Mlole aende Kitale
 
ZITO yupo DAR na anafuatilia isshu ya Makonda(Mkuu wa Mkoa mwingine),na pia alikuwa arudi ila NAPE Nae kaibuka.
Subirini kiki ziishe kwanza tutarudi.
Mkuu mie Nimeishi huo mkoa,kwanza ZITO ni mtoto wa Kijiji,na ndio maana alikuwa boarding pale Kigoma Seco.

Sasa kutoka kijijini kuongoza Maalwatan wa Kigoma mjini lazima atatambaa sana.
Ila ajue kwamba mkoa huo sio kabisaa,amuulize Dr.Walid Amaana Kabourou aliependwa kuliko Mbunge yoyote na alikuwa msomi kuliko ZITO ila watu walimpgiga chini na Chedema yake.

Watu wa Kigoma huwa hawachelewi hata kidogo kukupoteza Mbunge kwenye kura za mwisho.
Nimekulia Mkoa huo naujua vizuri saaana.Na nimesoma Kigoma Seco kabla ya kwenda Mwenge Secondary.Na niliwahi kuwa Polling Agent wa NLD
 
waambie na hao jamaa wenzako ,mnaonuka jasho,muendeke kibirizi au shule ya msingi mwenge pale kuna duka zuri tu wanauza pafyumu za bei poa .nafikiri tatizo lenu litakuwa angalau limekwisha .
 
Habari yenu wanajamvi.

Bila maneno mengi naomba kuelekea kwenye mada moja kwa moja.

Kwa siku saba Kigoma mjini iliyokaribu kabisa na ziwa Tanganyika imeingia kwenye tatizo la ukosefu wa maji safi na salama yaliyokuwa yakisambazwa na KUWASA kutokana na kile kinachosemekana kuwa kukatiwa umeme na TANESCO kutokana na malimbikizo ya madeni ya umeme ya muda mrefu.

Haijawahi kutokea tatizo la maji kuwa kubwa namna hii katika uhai wangu wote. Japo awali kulikuwa na miundombinu hafifu na tatizo la umeme KUWASA ilijitahidi kutoa maji hata kwa zamu. Maeneo ambayo maji hayakuweza kufika watu wa maeneo hayo walikuwa na sehemu ya kuyafuata kwakuwa ilikuwa si mbali sana.

Kwa sasa Kigoma mjini yote haina huduma ya maji. Kwa hali ilivyo tutegemee mlipuko wa kipindundu. Wananchi hasa akina mama wanatumia zaidi ya nusu ya siku kuhangaikia maji. Watu tunatembea tunanuka jasho. Kwa wajasiliamali imekuwa ni ahueni kwao ambapo maji ambayo hayajatibiwa yanauzwa kwa 1500/= kwa dumu la lita 20. Huku ndiko tumefikia.

Wananchi wa kawaida tunabaki na mshangao tu, Ikiwa kila mwezi tunalipa bill za maji na ikizidi mwezi mmoja unakatiwa iweje KUWASA ishindwe kulipa bill zao za umeme? Kinachosikitisha zaidi ni wananchi kuteseka kwa uzembe wa watendaji na wasimamizi wa mamlaka. Tunajiuliza tatizo hili litachukua muda gani?

Mheshimiwa Mbunge wetu Mwami Ruyagwa.Tunafahamu una mambo mengi sana ya kushughulikia kitaifa, ila kumbuka tulikuchagua utatue matatizo yetu kwanza. Wewe na chama chako tuliwapa mamlaka ya kutuongoza hapa Manispaa tukiamini mtatengeneza team nzuri ya kutatua kero zetu na kutuletea maendeleo.

Ni muda sasa tunataka kuona jitihada hizo. Meya ndio msimamizi mkuu wa shughuli ndani ya Manispaa amefanya nini kutatua tatizo hili kabla halijaleta maafa? Mbunge wetu huoni sasa ni muda wa wewe kuja Kigoma kuhakikisha tatizo hili linapata ufumbuzi wa kudumu?

Nia ya waraka huu ni kueleza hali halisi na kukumbusha wajibu tuliowapa kwenye sanduku la kura. Kuna mengi mlituahidi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zetu za masingi. Tunatarajia kuona suala hili linaisha haraka na kwamba halitarudia tena. Sisi wananchi tunaoteseka kwa sasa si makosa yetu kwakuwa bills zetu tunalipa.

Kwa niaba ya wananchi wenzangu ambao tumeamua kufanya ziara ya kwenda kuoga kila siku ziwani ni mimi.

Talentbrain wa Kigoma/Ujiji
Kwa hiyo unataka Zitto alipe deni la Umeme?
 
Mbunge wenu yuko bize na skendo ya Daudi Bashite ameshalisahau jimbo lake kabisa ila endeleeni kuisoma namba mliyataka wenyewe zito kabwe alibadirishana jimbo na Peter na nyie mkasapoti hicho kitu huku mkijua Peter Serukamba hakuna alichofanya Kigoma mjini na kinachowaponza zaidi nyie watu wa Kigoma mna ubishi ambao hauna faida yyt!!Zitto msimchague tena hana faida kwa wana Kigoma mkoa wenyewe huo umekuwa dormant miaka nenda rudi.
 
Zzk yuko bize mirija yake imekatwa huku mjini anahaha kwa hali na mali, sijui kama atawasikiliza!
 
Inashangaza wale tunaowalipa bili kila mwezi wanashindwa na wao kulipa tanesco hii Kali kweli nimeamini kila mnyoa nae hunyolewa.
 
Back
Top Bottom