Mkuu william
nimeshangazwa sana na mpango wako wa kuja kugombea ubunge katika lile jimbo alilokataliwa baba yako mzazi,
nimesoma kule facebook na huku jf nikaona kwa mkono wako mwenyewe umeandika hayo tena kwa majivuno ya hali ya juu
mkuu najua kabisa una haki kama mtanzania yeyote yule kuja na kugombea ubunge kwa kuwa ni haki yako ya kuzaliwa
lakini tangu nilipojua nia yako ya kufanya vile nilianza kujiuliza maswali mengi sana,hivi unafikiria nini hasa mpaka ufikie uamuzi wa aina hiyo,hivi unawaonaje watanzania hasa<HIVI UWEZO WAko wa kufikiri ukoje hasa,
mkuu umeishi marekani miaka mingi wewe na mkeo na familiya yako,sijui kama unapataga nafasi ya kuja kuchungulia nini kinaendelea kwenye nchi yako na kuondoka,
baba yako alipowasaidia kupitia mgongo wake kama waziri mkuu aliona kabisa nyie hamna future hapa tanzania,sijui nini kilimsukuma yule mzee aliyebadili dini uzeeni kufanya vile,
lakini wengi tulibaki nyumbani ambao ni rika moja na wewe kutokana na uwezo duni wa wazazi wetu ambao kwa kweli sipendi kukumbuka jinsi tulivyolelewa kwa taabu kubwa sana (mimi umri wangu kama wako)
umeishi maisha mazuri sana huko @NYC ambako unapasifia kila ukituma post kule facebook
nia na madhumuni yako ya kuja kugombea ubunge ni kiburi cha uzima,umeishi maisha mazuri tangu unazaliwa mpaka leo unapozeeka,
maana yako ya kuja kugombea ubunge sio kuwasaidia wale wagogo walioshindwa kusaidiwa na baba yako kipindi cha karibu miaka 20 alipokuwa mbunge wao,(mtoto wa nyoka ni nyoka)
nia yako ya kuja kugombea ubunge ni kuendeleza umaskini wa wale watu wa dodoma wanaoongoza kuomba omba pale dsm,
mkuu nataka ujue tupo watanzania wengi wenye uwezo huo,kuliko wewe kutoka @NYC uje kugombea ubunge bora atoke mtanzania yeyote popote pale ndani ya tanzania kama kule dodoma wamekosa mtu wa kufanya hivyo
nasema hivyo kwa sababu tume-share matatizo yetu tumebebeana mizigo wakati wewe una enjoy na wamarekani kwenye night club zao
mimi binafsi kama mtanzania niliyebeba mzigo mzito wa nchi yangu sikubaliani na wewe,najua utalazimisha lakini nakuahidi utajutia uamuzi wako
nyie ndio watoto wa mafisadi mnaotaka kuendeleza ufisadi wa baba zenu ndani ya nchi yetu kwa nia ya kuja kukandamiza watoto wetu
tutapambana na nyie kuhakikisha hicho kizazi chenu cha nyoka kimeondolewa kabisa kama kizazi cha gaddafi kilivyoondolewa KULE LIBYA
naandika hii sio mimi peke yangu nawakilisha mawazo ya mamilioni ya watanzania wanyonge
chagua kusuka au kunyoA