Waraka kwa viongozi wetu wa zama hizi za utumbuaji majipu

bomouwa

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,149
800
Wanajamvi kwema?

Mimi ni mtanzania ambae ninatamani kuona Tanzania mpya yenye maendeleo ya hali ya juu sana mpaka watu watamani kuhamia kama tunavotamani kuwa paka ulaya(utani wa kidhana).

Katika awamu ya tano ya Rais wa JMT bwana JPM ambae ameingia kwa kasi ya kuridhisha na lengo la kupunguza matumizi ya serikali pamoja na taasisi mbalimbali za kiserikali hususani mashirika ya umma. Kimsingi kasi yake inafurahisha wengi hasa ikizingatiwa enzi za kaka msoga yeye alichekelea na hakujali kiihivyo.

Lakini mimi ninaangalizo moja tu, tangu JPM aingie kazini na mtazamo huo,wamo walioachishwa na kusimamishwa kazi (nakubali kusahihishwa) kwa makosa aidha yao binafsi ama kwa uzembe wa wale ambao wanasimamiwa(subordinates).

Kutokana na nchi ya Tanzania kua mwanachama wa UN na inajipambanua katika medani za kimataifa kama ni nchi inayosimamia utawala bora na utawala wa sheria,ninajiuliza ni kwanini taratibu za kusimamaisha kazi mtumishi hazifuatwi kama sheria ya kazi inavoelekeza?

Kumekua na declaration kadha wa kadhi toka kwa viongozi waandamizi wakisema "nitawatumbua nyie majipu kabla sijatumbuliwa".Hili ni tatizo kubwa sana kwa maana kiutendaji inaonyesha wakubwa wanaupenyo mkubwa sana wakufukia madhambi kisa tu wana meno ya kufanya wanachotaka.

Katika utumvuaji huu ndio dhama ya "msafara wa mamba na.kenge wapo" ndipo unapojidhihirisha,kwa maana hata kama ulikua unawajibika kwa kiasi gani,ila kwakua wakuu wetu wanapenda CAMERA basi itakula kwako.
Ebu tujiulize kwa mfano huu,

Ikiwa unamtoto ambae haumuwajibikii kwa lolote katika masomo yake,hivi akifeli utaweza mlamba viboko?Itoshe kusema kwamba,dhana ya kupunguza matumizi ya serikali ni nzuri sana maana itaimarisha uchumi wa ndani na utegemezi wa fedha za nje,lakini dhana hii isitumike kuumize wengine kwa maana tu yakuonekana wewe ni mtendaji mzuri kwa kuwajibisha wengine pasipo kua na ushahidi wa kutosha. Ninauhakika kama wakurugenzi waliosimamishwa kazi wakafungua mashtaka katika mahakama ya kazi basi baadhi yao itadhibitika wamesimamishwa kimakosa sana na fidia watalipwa.

My take;
Rais kwa nafasi yako,simamia utawala wa sheria na utawala bora kuondokana na maamuzi yasiyo na tija maana ikumbukwe,kumuondoa mtu kazini ambae anategemewa na jamii ya watu zaidi ya 5 unaleta masononeko nafsini mwa hawa waliodhulumiwa na hivo laana zao zitapatilizwa katika kikazi chako.

Mungu ibariki Tanzania tuwe na maamuzi mema na ya busara.
 
Nchi hii ilikuwa imefikia pabaya watumishi haswa wa serikali walikuwa wamejiona Miungu watu...Hakika kwa kuanzia anachofanya Magufuli ni safi kwa kufikisha msg kwa watumishi legelege na wasio na maadili...
 
Nchi hii ilikuwa imefikia pabaya watumishi haswa wa serikali walikuwa wamejiona Miungu watu...Hakika kwa kuanzia anachofanya Magufuli ni safi kwa kufikisha msg kwa watumishi legelege na wasio na maadili...
Upo sahihi saana,lakini my observation ni kwamba taratibu za kiutumishi zifuatwe kama tunavojiaminisha hii ni nchi ya utawala bora na sheria.
 
Back
Top Bottom