Tangu mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya vyama ufanyike WAPO Radio ilionekana kuweka urari sawa wa taarifa zake kuhusiana na hali na mambo ya kisiasa ndani na nje ya vyama. Hata hivyo, tangu mikutano ya kampeni ifikie nusu ya muda wake wamiliki wa redio hiyo wameanza kushutumiwa kwamba wanaonekana kumwuunga mkono mgombea wa urais kupitia CCM.
Hivi karibuni, takribani wiki mbili, askofu Rwezaula na askofu Gamanywa (wote ni wa BSIC) wametawala vipindi vyote vya Meza ya Busara wakifafanua suala la amani. Mfano,askofu Rwezaula amezungumzia sana suala la amani akionesha kwamba eti amani huanza ndipo haki huja. Msimamo huo umeonekana kutokubalika na wasikilizaji waliowengi.
Kwa upande mwingine, inaonekana kama askofu Rwezaula amesahau au amejisahaulisha historia ya ukombozi wa mataifa ya Afrika. Historia inaonesha kwamba kukosekana kwa haki ndiko kuliko ibua Vita vya Majimaji. Afrika kusini chini ya ANC na PAC waliingia vitani dhidi ya weupe wachache kwa kuwa walinyimwa haki zao.
Askofu Rwezaula amesahau haraka mno kwamba redio yao ilikuwa ikiripoti taarifa za migomo ya madaktari, walimu, wafanyakazi mbali mbali, wanavyuo na migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji; makundi hayo yote kwa ujumla wake kila moja linadai kunyimwa au kupokwa haki zake. Aidha, migogoro hiyo imeishia kwa uvunjifu wa inayoitwa amani.
Aidha,Mungu ameonesha kwamba anakerwa na watawala wasiotenda haki. Na haki ilipokosekana kwa waebrania ( wayahudi) huko Misri walipomlilia Mungu wao; akasikia kilio chao. Akamtumia Musa kuwakomboa waebrania toka kwa wamisri waliowanyima haki waebrania.
Jambo la msingi hapa ni kwa redio WAPO kutoa elimu ya uchaguzi p wa amani pasipokuegemea upande wowote.
Pamoja na hayo, askofu Gamanywa siku ya juzi alijitahidi kubainisha falsafa ya redio yake (WAPO Radio) kwamba haina mafungamano na makundi au vyama vya kisiasa ingawa bado baadhi ya wasikilizaji waliopiga simu studio walionesha mashaka kwa ufafanuzi wake.
Ni suala la kufahamu kuwa wasikilizaji wanapoanza kuwa na mashaka na kutokubaliana kwa udhahiri na chombo cha habari ni dalili mbaya.
Kwa ufupi tu, uongozi wa WAPO redio unafahamu fika kwamba vipindi vyao vya Meza ya Busara, Linalo Nishangaza, Upanga wa Roho ni miongoni mwa vipindi vyenye wasilikilizaji wengi; ni vipindi ambavyo vimekuwa ni majukwaa ya mijadala huru na wazi tofauti kabisa na mijadala mingi ya mitandaoni.. Hebu waweke kando ushabiki na upenzi wao kwa chama fulani.
Mithali 24: 24-25
===================================
Update: 13 Oct 2015
Habari hii imekanushwa kwenye hii thread=>Wapo Redio, wakanusha habari zinazodai Wamenunuliwa Kisiasa