SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,841
- 1,843
Wakati CCM ikisisitiza kuandaa mkutano wao wa kisiasa tarehe 23 July huko Dodoma, Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni kada wa CCM amesema ni marufuku kufanyika kikao chochote cha kisiasa ndani ya mkoa wake na wapinzani hata wakiwa watatu ndani ya nyumba, atatumia polisi kuwatoa huko ndani na kuwashughulikia.
Kwa kauli hii, wale makada wa CHADEMA wenzangu ambao ndani ya nyumba mke, mme na watoto ni wanachama wa CHADEMA jiandaeni kuvamiwa, kwani mmezidi watatu na mko katika jengo moja, hivyo ni kikao cha kisiasa.
Huu ni udikteta wa kiwango cha rami? Au demokrasia ya kiwango cha aina gani?
Chanzo: Redio one - Nipashe