Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,974
- 45,850
Kwakua Bunge ndio silaha pekee ya wapinzani katika michakato yao, hawana namna nyingine zaidi ya kupigana kwa namna yoyote ile ili bunge lioneshwe live.
Wapinzani hawana mbinu za kuishi kama wapinzani nje ya bunge, ni kama risasi yao ya mwisho. Ni sawa na kumtoa samaki nje ya maji, hana ujanja.
Kwanini Bunge linakua ndio silaha yao ya mwisho kabisa? Uwezo wa kuleta changamoto katika majimbo yao ni mdogo sana, hawana ubunifu wala maono ya kushiriki na wananchi wao kubadili maisha ya wanaowawakilisha.
Wapinzani wameshasoma saikolojia ya watanzania wengi kua tunapenda kuishi kwa habari za udaku, kwamba kila siku tunapokutana hua tunakua na jambo fulani la kujadili, kwa kua tunapenda kujadili na kubishana, hivyo uwanja mzuri wa kutengeneza headlines ni bunge, kwamba ukishaingia bungeni na kusema jambo flani dhidi ya serikali, basi kutakua na jambo la kujadili kesho yake kwamba flani kasema hivi.
Awamu hii ni ya uchapakazi zaidi,, misingi inayotaka kutengenezwa ni ya maneno machache lakini utendaji ukiwa na tija zaidi.
Kwa asilimia kubwa zaidi, kwakua bunge sasa litakua linaendeshwa bila kua na fikra kwamba sasa naonekana ili nitumie fursa, hoja nyingi zitakua na tija, na mijadala itakua endelevu.
Tabia hii ya kutafuta umaarufu bungeni imekua ikizalisha wanasiasa ambao ni maarufu tu na umaarufu wao umekua ukiwanufaisha wao binafsi ilhali hali za wananchi wao iko dhaifu kabisa.
Hali hii ya sasa, naamini kabisa mihemko ikiwekwa pembeni, bunge litakua na tija zaidi ya lile la kishabiki, na mbunge atakayekua maarufu ni yule ambaye ataonekana jimbo lake sasa likifanya vizuri kimaendeleo.
Mwisho wa siasa za umaarufu wakati hali za wapiga kura zikiwa dhoofu umefika.