Wapinzani wa Tanzania mbona mnajimaliza wenyewe

NTIGAHELA

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
362
254
MVUVI HALISI MITEGO HAKOSI.

Mjadala mzito wa chuki, kiburi, ujuwaji na tambo unaendelea kupamba moto mitandaoni.

Si kuwa tayari kupitwa kwa vile dhulma sio tu kama naichukia, bali napambana nayo kwa nafasi alonijaalia Mwenyezi Mungu.

Ninachokiona mimi naona ni yale yale Ujinga Mtamu kwani wapinzani wameshindwa kukwepa mitego ya mahasimu wao na sasa tayari wameshanasa, sijategemea wasomi, wanasheria mahiri na wanaharakati machachari kunasa kwenye dema kirahisi kiasi hichi.

Jiulizeni hivi, sasa mijadala muhimu ya ukombozi wa taifa la Tanzania mumemkabidhi nani?

Mumebakia kulumbana wenyewe kwa wenyewe, huku hasimu yenu mukizidi kumuonesha mapungufu yenu ili nafasi hiyo aitumie vyema kukuburuzeni.

Wallahi ni jambo la kuhuzunisha na kusikitisha, baada ya mateso, manyanyaso, kejeli, dharau, kufilisiwa, kuibiwa, kushikiliwa, kujeruhiwa na kuuliwa hamujapevuka kiakili tu.

Mumekubali kuingizwa demani na kuvuliwa kirahisi kiasi hichi kuliko hata samaki, madhalimu kweli wana mbinu kuliko hata Ibilisi.

Hivi hamujielewi kama nyote ni waathirika wakubwa wa mfumo CCM? Nyote mulumbanao hakuna asiyeonja bakora za CCM, kwa njia moja au nyengine, na ndio kwanza wanazidi kutucharaza.

Sasa nyinyi tulotarajia ndio waombezi mumeamuwa kutuvua nguo ili bakora za CCM zituingiye vizuri, sioni faida yeyote ya malumbano yenu zaidi ya hasara, na kuwapa mafanikio ya kuendelea kujiamini watawala kwenye madaraka.

Mungelisoma kutoka Zanzibar, na mungejiuliza kwa nini walifanya siasa kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu tu, na waliweza kuwagaragaza na kuwasambaratisha CCM vibaya sana.

Siri kubwa ni kuwacha tofauti zao zote na kujuwa kuwa adui wao mkubwa ni CCM, na CCM wao waliona njia ni kuwagawa ili waendelee kuwatawala, kwa kulijuwa hilo wazanzibar walishikamana na kuaminiana hatimaye waliipiga mwereka.

Na kama si unafiki na umimi wa wapinzani wa Tanganyika na nguvu za dola tungeshaisaha CCM.

Umoja, kuaminiana, kuvumiliana, na dhamira njema na ujasiri ndio siri kubwa ya kufanikiwa.

Hakuna mpinzani yeyote kama yeye na kundi lake, atafanikiwa kuwaondosha watawala madhalimu madarakani na ingekuwa hilo lawezekana wazanzibar, na watanganyika wangeiyondosha CCM kipindi hicho CUF haijasambaratishwa.

Upinzani Tanzania lazima tuifanye timu ya mpira kila mchezani ana umuhim na uhitaji wake, na lengo ni ushindi kwa hiyo mabeki kuzuiya maadui, viungo kuwaunganisha na washambuliaji kusaka magoli.

Lakini timu imara inacheza bila kujali makosa ya mchezaji mmoja mmoja, na pale katika jitihada za kuokoa, beki tumaini anaweza kujifunga katika harakati za kuokoa, tusimuhesabu kauza mchezo kwa kula pesa.

Na tunapomuona golikipa kaliwacha goli lake kenda kwenye kushambulia musimshtumu bali wengine rudini golini kulinda yeye ana mbinu mbadala tuliwahi kumuona golikipa wa Liverpool akiipatisha ushindi timu yake katika dakika za majeruhi.

Hebu wapinzani wacheni malumbano yaso na tija tuweke mikakati ya kuliokoa taifa kwani jua linazama.
 
njaa na harakat havikai chumba kimoja anyway kwan polepole yeye anasemaje
 
Back
Top Bottom