Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,874
Vyama vya upinzania Tanzania vilianzishwa mwaka 1992 ni miaka 24 sasa. Lakini cha kushangaza vyama hivi vya upinzania bado vichanga kama mtoto mdogo anayenyonya anayevalishwa nepi.
Nadhani sifa za watoto wachanga wengi wetu tunazijua.
Hii ninasema kwasababu zifuatazo:-
1. Kila chama duniani kilicho na tija kwa maendeleo ya nchi huwa kina sera na inajulikana. Kwa vyama vya upinzani Tanzania havina sera huwa vinadandia dandia tu matukio na mara nyingi vinaongozwa kwa mihemuko ya matukio.
2. Vinaendeshwa kwa ulaghai na uongo kwa kuwadanganya na kuwalaghai wananchi kupitia shida zinazowazunguka kwa kuwadanganya.
3. Kauli mbali mbali za viongozi wa chama hiki huwa zinapingana zenyewe. Kwa mfano Msigwa, Lema na hata Mbowe. Mara ya kwanza walimpinga Lowassa kwa nguvu zao zote na wakazunguka nchi nzima wakitangaza kuwa ni fisadi. Lakini kwa sasa hao hao ndio wenye kupokea mafisadi na kuwanadi kwa wananchi kuwa viongozi.
4. Mtu mmoja tu kukiongoza chama kwa mda wote. Ni kitu cha kushangaza sana miaka zaidi ya ishirini wenyeviti a vyama vya upinzani hawanaimani na wanachama wengine kushika nyazifa za uenyekiti. Ni hatari sana ina maana mwenyekiti ni kama mmiliki wa chama, ni kana kwamba chama hicho ni kampuni kwamba mmiliki huwa habadiliki mpaka aamue yeye.
5. Je ukawa sasa hivi inaendeleaje? Je ulikuwa muhemko wa kutaka kuwagawa watanzania ili kusaidiana kupata raisi? Je siasa za namna hii si upuuzi mkubwa. Inamaana ukawa tangu uishe uchaguzi mbona hakuna kikao cha wana ukawa. Maalim Self kaumwa wenyeviti wa vyama vya ukawa hata kwenda kumuona tu hakuna. Ukawa ipo haipo?
6. Kutoka bungeni na kupiga kelele hovyo hovyo. Ni ujinga unapozila wenzako wanaendelea. Ni bora sasa kubadilika. Ni kitu cha kushangaza sana kwanini hawakatai kuchukua posho za ubunge. Ni vyema sasa bunge litunge kanuni kuwa mtu akitoka bungeni mara moja apewe onyo, mara ya pili anafungiwa kupata pesa kutoka bungeni kwa mda wa miezi mitatu, mara ya tatu anafungiwa kupata pesa kwa mda wa mwaka mmoja, mara ya ninne anakuwa muhujumu uchumi anakatazwa kugombea ubunge na anakuwa hapewi pesa mda wote wa ubunge wake.
Upinzani wa namna hii unadumaza maendeleo ya nchi. Ni wakati sasa vyama vya upinzani kujitazama upya na kuanza upya maana step wamekosea.
Waangalie nchi zingine zilizopiga hatua kisiasa au waige kutoka CCM waache kubweka hovyo hovyo na kupiga kelele ambazo hazina tija kwa maendeleo ya nchi.
Ni bora kwenda na alama za nyakati na kusoma majira. Kulia lia ni tabia za kitoto na zina mwisho wake.
Wapinzani Tanzani ni wachanga sana bado wananyonya maziwa kwa mama yao CCM