Wapinzani ni wapi tumejikwaa?

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,854
1,776
Baada ya kile kilichoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi kusambaratika kwa kipigo kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kuna kila dalili kwamba bado tuna miaka 40 mbele kwa Upinzani(kama upo ) kuchukua Dola.

Sababu za kutochukua Dola kwa sasa ni pamoja na:-

(a) Kukosekana kwa ajenda wanayosimamia. Kila chama kiko bize kupigania maslahi binafsi ya Chama badala ya Taifa. Sera za baadhi ya Vyama haziwashawishi wapiga kura kuviamini;

(b) Ubinafsishaji wa Vyama Vya Siasa has a Upinzani ambapo Vyama vimekuwa Mali ya Viongozi badala ya Wanachama. Matokeo take ni migogoro isiyokwisha;

(C) Vyama kukosa misimamo ya Kisiasa na tabia ya ugeugeu. Leo wanasimamia hiki na kesho wanasimamia kingine;

(d)Kukosekana kwa Viongozi makini na ukosefu wa uzoefu wa kuongoza Nchi. Viongozi wengi waliokimbilia huko ni makapi ya CCM ambao hawana credibility mbele ya jamii.

Hizo ni sababu chache ambazo zitawafanya Wapinzani wasubiri hadi 2055
 
Pia upinzani umekosa ideology na badala yake unafuata personalities.
 
Miaka ya 2007,2008,2009 nilipigania sana kuukosoa upinzania na nilisema, kama tunataka mbadala wa CCM lazima tuwe na

1.upinzania unaoweza kukosolewa
2.kuonywa
3.kushauriwa
4'upinzania wenye kuweza kuchukua maoni na kuyafanyia kazi
5.upinzania wenye ajenda na ideology iliyosimama, isiyoyumbishwa na rahisi kueleweka kwa kila raia
6.upinzani unaomilikiwa na wananchi muda wote bila kujali upepo wa chama tawala
7.unaowaza namna tu ya kuindoa ccm kutoka kwenye basic principles kama kuwa na tume huru ya uchaguzi

sasa some of us we had guts ya kuwanyoosha na kuwakosoa wapinzani, mpinzani akiweza kukubali kukosolewa akiwa mpinzani likely hata akiwa mtawala atakuwa kanyooka

upinzani usioweza kukosolewa, kuchukua ushauri kama wapinzani hawataweza hata wakiwa watawala!!

Tuna upinzani uliokuwa shielded/protected kwa gharama zote hata ukiwa na wewe mpinzani ukatoa ushauri utaonekana ni ccm tu

ulikiwa vile, iko hivyo p
 
Kukaribisha watu walishatuhumiwa na hata viongozi wa upinzani huko nyuma waliwataja katika mikutano kama mafisadi papa. Mwishowe mafisadi papa wanakaribishwa na kugombea nyadhifa kichama na kitaifa,sasa chama kinapoteza muelekeo na kinashindwa kisimamie nini .
 
Hii nchi haina upinzani ina vibaraka wa wenye saccos za vtama ndo hao wanaoitwa wapinzani ndani ya vyama vya siasa.ukiwa na akili timamu huwezi kushabikia chama kama CUF na Chadema. Hivi sio vyama vya siasa bali ni saccos za seif na sasa Lipumba anataka kumnyanganya seif. Na Chadema ni cha Mtei, ndesamburo na mbowe.

Nani anayebisha ajitokeze hapa sasa hivi.
 
Utayakoga mkuu.
 
Baada ya kile kilichoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi kusambaratika kwa kipigo kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kuna kila dalili kwamba bado tuna miaka 40 mbele kwa Upinzani(kama upo ) kuchukua Dola.

Sababu za kutochukua Dola kwa sasa ni pamoja na:-

(a) Kukosekana kwa ajenda wanayosimamia. Kila chama kiko bize kupigania maslahi binafsi ya Chama badala ya Taifa. Sera za baadhi ya Vyama haziwashawishi wapiga kura kuviamini;

(b) Ubinafsishaji wa Vyama Vya Siasa has a Upinzani ambapo Vyama vimekuwa Mali ya Viongozi badala ya Wanachama. Matokeo take ni migogoro isiyokwisha;

(C) Vyama kukosa misimamo ya Kisiasa na tabia ya ugeugeu. Leo wanasimamia hiki na kesho wanasimamia kingine;

(d)Kukosekana kwa Viongozi makini na ukosefu wa uzoefu wa kuongoza Nchi. Viongozi wengi waliokimbilia huko ni makapi ya CCM ambao hawana credibility mbele ya jamii.

Hizo ni sababu chache ambazo zitawafanya Wapinzani wasubiri hadi 2055
Upinzani wa Tanzania ulikufa Mwaka Juzi 2015.

Biashara ishafanyika tulieni Dawa ya JPM iwaingie
 
Watu mnaishi sayari ingine na sio Tanzania.
1. Kwa sasa mnatakiwa mhujue kuwa serikali imebeba bunduki, marungu, mabomu na kila siraha kupitia kwa kila aina ya jeshi na makamanda yao kuhakikisha RAIA hawapati chochote kutoka kwa wapinzani na wapinzani hawafikishi chochote kwa RAIA. Wote ni mateka wakubakia na yanafanyika ndani ya nyumba moja yawe mazuri au yawe mabaya.
2. Vyombo vyote vya habari hata hii mitandao imebanwa vilivyo kusifia na kusifia yanayo toka ndani ya nyumba hii.
3. Fitina zote zinaelekezwa kusema kama mleta Uzi alivyosema.

Hivyo, kusema wapinzani hawana linatoka wapi? Unapofuga RAIA unafahamu matokeo ya RAIA waliofugwa tabia zao huwa zikoje hasa ktk mazingira ya kuminywa Uhuru wao.

Uhuru ni kitu tunu, ni kitu kisicho na mlinganishi ambacho kwa sasa kimya kimya ni siraha za Wapinzani.

Mkoloni ndie aliyewahi kuwafanyia mambo mengi kuliko yeyote hapa Tanzania/Tanganyika. Vyote uvianavyo Barabara, Reli, Ndege, Meli, Maji, Bandari, Hospitali, Shule, nk nk mkoloni alivifanya sana. Lakini alivifanya kwa kuminya Uhuru wa Watanganyika kukiwamo na kuwapiga viboko.
Hilo la Uhuru wa Watanganyika ilibidi waondoke come what may.
Gadafi aliwafanyia makubwa wa Libya kuliko kiongozi yeyote hapa Afrika, lakini la kufuta Uhuru wa Walibya, kwa wakati huo walisau kila kitu. Gadafi alibidi ajifiche chini ya cravat.

Uhuru wetu Tanzania unapotezwa ktk maneno, narudia maneno, hiku kukiminywa Uhuru wetu.

Mbele ya Uhuru mengine ni utopia

Siku filimbi ikilia ya siasa lurch siwa mtashangaa. Utashindwa kurudia kuwa hawa watu ni makapi. Kuna walio isha weka mapenzi fulani rohoni mwao, utawaona siku hizo. Viwavi jeshi jua uwakapo hujichimbia chini ya ardhi pindi mvua inyeshapo utashangaa huwa wako wapi, hata kama miaka ni 100.
Siku siasa ikiruhusiwa hamutaamini wapinzani kama ni mamilioni ya watu kama mtakavyo waona.
 
Hii nchi haina upinzani ina vibaraka wa wenye saccos za vtama ndo hao wanaoitwa wapinzani ndani ya vyama vya siasa.ukiwa na akili timamu huwezi kushabikia chama kama CUF na Chadema. Hivi sio vyama vya siasa bali ni saccos za seif na sasa Lipumba anataka kumnyanganya seif. Na Chadema ni cha Mtei, ndesamburo na mbowe.

Nani anayebisha ajitokeze hapa sasa hivi.
It's true na hamna anayebisha mkuu.
 
Wapinzani na wasiowapinzani ni jamii mmoja ya watanzania,kama kuna mapungufu sio tu ni ya wapinzani bali hata watawala nao wanamatatizo.
Mkuu kitu cha kuwawezesha wapinzani kuchukua dora,ni kuwa na katiba iliyo transparent kwa vyama au kundi la siasa vinapogombea nafasi ya uingozi kuepuka magoli ya NAPE.
 
Dora?
 
CCM wepesi...kinachowabeba katiba ya chama kimoja...ikiwepo katiba mpya yenye kujali misingi ya vyama vingi....CCM inapotea kwenye dunia tunayoishi...wanalijua hilo
 
Baada ya kile kilichoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi kusambaratika kwa kipigo kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kuna kila dalili kwamba bado tuna miaka 40 mbele kwa Upinzani(kama upo ) kuchukua Dola.

Sababu za kutochukua Dola kwa sasa ni pamoja na:-

(a) Kukosekana kwa ajenda wanayosimamia. Kila chama kiko bize kupigania maslahi binafsi ya Chama badala ya Taifa. Sera za baadhi ya Vyama haziwashawishi wapiga kura kuviamini;

(b) Ubinafsishaji wa Vyama Vya Siasa has a Upinzani ambapo Vyama vimekuwa Mali ya Viongozi badala ya Wanachama. Matokeo take ni migogoro isiyokwisha;

(C) Vyama kukosa misimamo ya Kisiasa na tabia ya ugeugeu. Leo wanasimamia hiki na kesho wanasimamia kingine;

(d)Kukosekana kwa Viongozi makini na ukosefu wa uzoefu wa kuongoza Nchi. Viongozi wengi waliokimbilia huko ni makapi ya CCM ambao hawana credibility mbele ya jamii.

Hizo ni sababu chache ambazo zitawafanya Wapinzani wasubiri hadi 2055
Mkuu Gangongine umesikia matokeo ya uchaguzi mdogo huko uyui Tabora? Chadema wamesepa na vijiji.
 
Miaka ya 2007,2008,2009 nilipigania sana kuukosoa upinzania na nilisema, kama tunataka mbadala wa CCM lazima tuwe na

1.upinzania unaoweza kukosolewa
2.kuonywa
3.kushauriwa
4'upinzania wenye kuweza kuchukua maoni na kuyafanyia kazi
5.upinzania wenye ajenda na ideology iliyosimama, isiyoyumbishwa na rahisi kueleweka kwa kila raia
6.upinzani unaomilikiwa na wananchi muda wote bila kujali upepo wa chama tawala
7.unaowaza namna tu ya kuindoa ccm kutoka kwenye basic principles kama kuwa na tume huru ya uchaguzi

sasa some of us we had guts ya kuwanyoosha na kuwakosoa wapinzani, mpinzani akiweza kukubali kukosolewa akiwa mpinzani likely hata akiwa mtawala atakuwa kanyooka

upinzani usioweza kukosolewa, kuchukua ushauri kama wapinzani hawataweza hata wakiwa watawala!!

Tuna upinzani uliokuwa shielded/protected kwa gharama zote hata ukiwa na wewe mpinzani ukatoa ushauri utaonekana ni ccm tu

ulikiwa vile, iko hivyo p
Hatutaki kushauriwa na CCM
 
Back
Top Bottom