Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni Tanzania tu miongoni mwa nchi za Afrika ambapo wapinzani wanaweza kukaa meza moja na kubadilishana mawazo na Serikali.
Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anaweza kumtusi Rais na bado akaendelea kutamba mitaani.
Ni Tanzania tu ambapo mpinzani anaweza kuingia barabarani na kuandamana pasi na kibali cha polisi
Ni Tanzania tu ambapo wapinzani wanaitwa Ikulu na kunywa juice na Rais
Ni Tanzania tu mtu anaweza kutangaza kuwa nchi haitatawalika na bado akaendelea kudunda mitaani
Ni Tanzania tu ambapo mtu ametangaza kutaka kuiangusha serikali kule Zanzibar na bado analelewa tu na kupewa heshima zote..
Hakika Serikali ya CCM imekuwa na upole sana kiasi ambacho sasa wapinzani wanaona kuwa ni halali yao kuvunja sheria na serikali isiwaguse na kwamba wakiguswa tu inaonekana kwamba wanaingiliwa uhuru wao wa kufanya siasa. Niwaambie wapinzani wa Tanzania, huyu Rais tuliyenaye ni mkali wa kusimamia sheria na kwamba mambo ya kuleana, kuvumiliana na hata kulindana hayapo kwenye utawala wake. Kama unavunja sheria hakika utachukuliwa hatua stahiki bila kujali wewe ni nani na una wadhifa gani.
Wapinzani wa Tanzania mlideka sana. Hakika ilifika wakati mpaka tukamuona Rais na taasisi yake ni kama mshkaji wetu ama mtu mwingine yeyote yule. Tulifikia hatua ya kumuita Rais ni dhaifu na bado alituvumilia. Sasa mnaelekezwa jinsi ya kufanya siasa mnaanza kulia lia tena mapemaa hata kabla ya mwaka haujaisha
Hakika nawahakikishia kuwa msipobadilika mtahangaika sana utawala wa Magufuli na mtalimia meno. Magufuli huyu ninayemjua hakika hamtatoboa. habadiliki na yupo tayari na ameapa kuwa ataondoa uozo wote ili mradi tunyooke. yupo tayari kuitwa majina yote manaya ila msimamo wake ni kwamba hatayumbishwa na hatakata tamaa kwani kukata tamaa maana yake ni kuharibu nchi. Hamtakuwa na muda tena wa kushughulikia kero za wananchi kwenye majimbo yenu badala yake mtahangaika na Magufuli tu.
Huu ni ukweli ambao unapaswa kusemwa waziwazi ili yakiwakuta msije kusema kuwa Lizaboni hakutushauri jinsi ya kuenenda na zama za Hapa Kazi Tu.