Wapinzani msione soo kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli

Mpunilevel

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2015
Messages
3,149
Points
2,000

Mpunilevel

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2015
3,149 2,000
Toka aingie madarakani, mheshimiwa Rais amekua mwiba kwa viongozi wazembe na wabadhirifu serikalini.
Rais amedhamiria kwa dhati kuona maisha ya wantanzania yanakua bora na si bora maisha.
Cha ajabu akiendelea kusafisha uozo huo wamejitokeza wapinzani na kulalamika kwamba anaonea watumishi wasio na hatia.

Wakati wa utawala wa awamu ya nne ya jakaya kikwete walilalama sana kwamba serikali hiyo imejaa wapiga deal.
Sasa magufuli anazitoa kero hizo wenyewe wamekaa kimya bila ya kupongeza juhudi hizo, matokeo yake ni kuvunja moyo juhudi hizo.

Na hisi wanaotumbuliwa itakua ni jamaa zao ambao walipokua wakipora fedha toka serikalini, waliwafadhili Ndio maana wanapata kigugumizi kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais.
Nahii inathibitisha jinsi wanasiasa si wote walivyonahadaa wanapokua wanasaka mamlaka.

Ni jukumu letu sote sasa kupima kauri zilizotamkwa hapo nyuma na zinazotamkwa sasa, Nani ni mzalendo kati ya hawa wanasiasa.
Namshauri mheshimiwa Rais asichoke kutumbua haya majipu, kwani hawezi kujenga uchumi imara huku juhudi hizo zinahuhujumiwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu ambao wamo ndani ya serikali yake.

Bila viongozi waadirifu, hata kuwe na mipango madhubuti na imara kiasi gani nchi haitasonga mbele.

Tuache mtindo wa siasa za matukio, tufanye siasa za kuleta umoja wa kitaifa na kutatua kero za wananchi.
Uchaguzi umekwisha tujenge nchi yetu kwa pamoja.
 

Forum statistics

Threads 1,389,930
Members 528,059
Posts 34,038,932
Top