Makusudically
JF-Expert Member
- Feb 3, 2014
- 2,203
- 1,235
Kitendo kilichofanywa na Wabunge wa Upinzani kudai eti wamemumiss kinaleta ukakasi kwa Wananchi tuliowachagua Wabunge hawa, kila Mwananchi anajua na hatujasahau kabisa kwamba ni Wabunge hawa hawa ndiyo waliokuwa wakishupaa bungeni na kutokwa povu kwa kudai kuwa JK ni Rais mdhaifu, ameharibu Uchumi, amevuruga Demokrasia na ni Dikiteta, na anasafiri nje kupita kiasi na hajali masuala ya nchi.Walisema kuwa JK ni mpole, anacheka Cheka Ovyo. Leo tena hao hao Wapinzani wanamshangilia kama "mazuzu" tena bungeni. Haya bwana Wapinzani mmemumiss JK, tena aliruhusu kukua kwa Demokrasia. Hongereni kwa kuwashangilia wana CCM.