mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Tangu uchaguzi mkuu wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi vya siasa mwaka 1995 hadi uliopita wa mwaka 2015, vyama vya upinzani vimekuwa vikiingia kwenye uchaguzi vikivizia kushinda urais na siyo kukishinda Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa kuwa vinaingia kwa kuvizia, matokeo yake vimekuwa vikishindwa kupata matokeo bora. Kwa kawaida mviziaji hufanya mambo yake kwa kubahatisha. Kuvizia ni kamari, kupata au kukosa yote ni majibu.
Baada ya miaka 20 ya kuvizia, sasa ni wakati wa vyama vya upinzani kufanya siasa za uhakika. Kujielekeza kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 vikiwa vimejipanga kwa matokeo bora, kisha kujielekeza mwaka 2025 kwa uhakika wa kuibadili CCM katika uongozi wa nchi.
Hesabu za kumng’oa Rais wa sasa, Dk John Magufuli kwenye uchaguzi ujao zinaweza zisifanikiwe, hata hivyo wakiwa na dhamira ya kweli ya kufanya siasa za uhakika, mwaka 2025 wataweza kuiondoa CCM madarakani.
Kuing’oa CCM madarakani inahitaji mipango yenye kusukwa kisayansi. Uwekezaji mzuri wa kisiasa unatakiwa kufanyika. Mtu akitoka nyumbani kwake akiwa barabarani aone mazingira ya usawa kati ya CCM na upinzani.
Sasa hivi wapinzani huingia kwenye uchaguzi kwa kutegemea miujiza ya Daud kumpiga Goliath. Wanajiona kabisa ni dhaifu lakini wanajipa matumaini ya kushinda kwa miujiza. Ni hesabu zenye kurandana na ndoto za alinacha.
Kama vyama vya upinzani vitaachana na tabia ya kutegemea miujiza ya Daud na Goliath kisha kuamua kuanza kujitengeneza kama washindani wa kweli dhidi ya CCM, inawezekana wasimuweze Rais Magufuli mwaka 2020, ila waiweza CCM 2025.
Vigumu kumng’oa Rais Magufuli
Kabla hata Rais Magufuli hajatimiza mwaka mmoja madarakani, alipiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa. Alisema shughuli za kisiasa zisubiri mwaka 2020. Akajenga hoja kuwa hataki kuongoza taifa ambalo watu wake muda wote wanawaza siasa.
Baadaye ulifuata uamuzi wa kuzuia vikao vyovyote vya kisiasa hata vya ndani. Rais Magufuli aliahidi kuwa yeye ni wa tofauti na kweli ameonesha utofauti. Awamu zilizopita, Rais Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa, walipoona joto ni kali, walikutana na wapinzani na kulipoza.
Tofauti iliyopo sasa hivi ni kuwa wapinzani wakitia presha kwa maneno na harakati ndivyo na Serikali inavyoongeza makali. Kikwete na Mkapa waliamini dawa ya moto ni kuumwagia maji upoe, Rais Magufuli msimamo wake ni kuwa dawa ya moto ni moto.
Ujasiri wa wapinzani hauonekani kama ilivyokuwa wakati wa Rais Kikwete. Hivyo, jinsi ambavyo wanapoa ndivyo na nguvu yao kisiasa inavyopungua. Kwa kasi iliyopo sasa hivi, ni vigumu kujipa matumaini ya kumweka kando Rais Magufuli katika uchaguzi ujao.
Tume na wasimamizi wa uchaguzi
Kumng’oa Rais Magufuli katika uchaguzi ujao ni ndoto kubwa lakini ni ya alinacha. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), mwenyekiti wake na timu yote, anayeteua ni Rais. Hivi karibuni Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Jaji Semistocles Kaijage kuwa mwenyekiti wa Nec pamoja na wasaidizi wake.
Katika halmashauri za miji, wilaya, manispaa na majiji kuna wakurugenzi ambao huteuliwa na Rais. Wakurugenzi hao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi kwenye maeneo yao. Hutangaza matokeo ya wabunge na yale ya urais huyawasilisha makao makuu ya Nec kwa ajili majumuisho na matangazo ya jumla.
Katika uteuzi wa wakurugenzi mwaka jana, ilishuhudiwa Rais Magufuli akiteua makada wengi wa CCM kushika nafasi hizo kwenye maeneo mbalimbali nchini. Ni watu hao ambao watakuwa wasimamizi wa uchaguzi mwaka 2020.
Muundo wa tume na wasimamizi wa uchaguzi ni kiwakilishi tosha cha mazingira magumu ambayo wapinzani watakabiliana nayo, hivyo ni lazima kuwapa ujumbe kuwa wajiandae kisaikolojia kipindi hiki ambacho wanapiga hesabu za kumng’oa Rais Magufuli.
Swali dogo la hisia; mtu anapokuwa kwenye cheo cha kuteuliwa, je, unadhani asingependa aliyemteua aendelee kuwepo madarakani ili cheo chake abaki nacho? Kama ndivyo na ikitokea fursa ya kumsaidia aliyemteua, je, hataitumia ili kwa kumsaidia kwake ndipo na yeye aweza kujihakikishia usalama wa nafasi yake?
Nguvu ya Rais aliye madakani
Siyo Tanzania tu, Afrika yote, sehemu kubwa ya Asia, Amerika Kusini na baadhi ya maeneo ya Ulaya, uchaguzi unaomshirikisha kiongozi wa nchi aliyepo madarakani huwa mgumu mno kwa wapinzani.
Katiba na mazingira mengine ya kisheria yaliyowekwa pamoja na mfumo wa kiutawala katika nchi, ni sababu ambayo hufanya uwanja wa kisiasa usiwe tambarare hata nyakati za kampeni.
Ni kipindi ambacho wapinzani hujikuta wakikabiliana na usumbufu mwingi wakati kiongozi aliye madarakani hupata upendeleo kutokana na woga wa vyombo vya nchi, vilevile na mazingira ambayo kiongozi hujiandalia. Isisahaulike kuwa ni asili ya kila binadamu kujipa kipaumbele.
Uchaguzi Mkuu 2020 kama Mungu atatuweka hai, Rais Magufuli ataingia kwenye uchaguzi kama Mkuu wa Nchi ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu. Majeshi yote yanamtii kama mkuu wao, ile nafasi ya ukuu wa nchi inamfanya kuwa sauti yenye mamlaka kuliko raia mwingine yoyote nchini.
Unapokumbuka ile sauti iliyozuia mikutano ya hadhara ya kisiasa mpaka mwaka 2020, ni rahisi kuutabiri ugumu ambao wapinzani watakutana nao. Katiba ya nchi iliyopo na ambayo imekuwa ikilalamikiwa, inampa nguvu nyingi Mkuu wa Nchi, nguvu ambazo Rais Magufuli anapenda kuzitumia kikamilifu.
Wapinzani wameingia kwenye awamu ya tano chini ya Rais Magufuli baada ya kukamilika kwa miaka 10 ya JK. Wapinzani walideka kipindi cha JK si kwa sababu ya Katiba na sheria nyingine zilizopo, bali deko lao lilitokana na aibu ya kidiplomasia aliyokuwa nayo JK.
Katika kipindi chake JK alijizuia mara nyingi kutumia mamlaka yake ambayo yanatolewa na Katiba. Wakati huu, Rais Magufuli yeye hataki kujizuia kutumia mamlaka aliyopewa. Hii ndiyo sababu wapinzani wanaakisi ugumu wa kufanya siasa kipindi hiki, vivyo hivyo haitakuwa rahisi kwenye uchaguzi ujao.
Uimara wa CCM
Uchaguzi Mkuu 2015 ulithibitisha kuwa CCM ni imara zaidi ngazi za chini. Mtikisiko ambao ulitarajiwa kutokea baada ya Waziri Mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa kuhama na kujiunga Chadema haukuwa mkubwa kama hofu ilivyokuwepo awali.
Pamoja na hivyo, kwa kutathmini nguvu binafsi aliyokuwa nayo Lowassa, unaona kuwa isingekuwa rahisi kwa Rais Magufuli kumshinda kama siyo kutegemea mtandao imara wa CCM kuanzia juu kwenda chini kabisa ambako wapinzani hawafiki.
Uchaguzi kama bahari eneo la kina kirefu, CCM kura zao huzikusanya kuanzia juu mpaka chini kabisa palipo na sakafu ya bahari, maana kimeenea mijini mpaka vijijini na kote huko huvuna kura. Wapinzani hujionesha ni wakubwa kwa juu lakini huelea baharini, hawafiki sakafuni. Maana yake hawana mtandao mzuri wa kuvuna kura mpaka vijijini.
Utakapowadia Uchaguzi Mkuu 2020, nguvu ya Rais Magufuli kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kujumlisha na uimara wa kimtandao wa CCM, inajenga picha ngumu kwa kushinda urais.
Hesabu za mwaka 2025
Vyama vya upinzani vinatakiwa kujipanga na kuanza kupiga hesabu ya kuishinda CCM katika Uchaguzi Mkuu 2025, maana hilo linawezekana na lipo ndani ya uwezo wao.
Ikiwa watajiweka sawasawa kufanya mabadiliko, Uchaguzi Mkuu 2025 wapinzani hawataingia kwenye uchaguzi kwa kutegemea miujiza ya Daud kumpiga Goliath, bali watakuwa wanayasaka matokeo ambayo watakuwa wameyaandaa.
Jambo la kwanza, vyama vya upinzani vinatakiwa vihakikishe vinafika kwenye sakafu ya bahari, siyo kuelea juu. Vifike vijijini na kila eneo ambalo kuna wananchi. Kila palipo na kura navyo viwepo.
Kufika huko ni kazi ya kutengeneza mtandao. Vyama vifanye kazi ya uenezi kuelekea mwaka 2019 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Endapo wapinzani watapata matokeo mazuri kwenye mitaa, itakuwa rahisi kutengeneza madiwani na wabunge wengi 2020.
Wapinzani wakishakuwa na mtandao mzuri wa wanachama mpaka vijijini, kisha wakawa na madiwani pamoja na wabunge wengi katika ya mwaka 2020-2025, wataweza kuchochea mabadiliko mengi ya sheria za uchaguzi, itakuwa rahisi kuidai Katiba mpya na itapatikana. Ni hapo ndipo wataweza kuiondoa CCM 2025.
Chanzo: Maandishi Genius