Wapinzani hawajashindwa kuing'oa CCM, tatizo ni mfumo

Wapinzani hawajashindwa kuing'oa CCM, tatizo ni mfumo

Hakuna popote duniani ukute mshinda atengeneze mfumo wa kushindwa. Kila kitu kinaenda kwa sheria, sheria hupitishwa na bunge kwa kupigiwa kura na walio wengi hushinda. Hakuna nchi yoyote duniani inayoamini upigaji wa kura ukute eti wenye kura chache washinde.

Kwenye Bunge la Katiba, ni wazi tangu siku nyingi CUF wanataka serkali mbili baadaye Muungano ufe tuwe na Serkali ya Mkataba.

CHADEMA wakaona nafasi nzuri ya kutawala wakajaza watu wao kwenye Tume, wakaja na hoja ya serkali tatu iwe rahisi kugawana, CUF kule na wao huku.

Lakini ni jambo la msingi la tangu zamani na ndiyo maana damu ilimwagika Zanzibar, haiwezekani hoja ipite hivi hivi bila kuzingatia maoni ya wengi. Wakajiunga Ukawa washinikize "maridhiano" eti CCM wakubali "muafaka" ili Muungano uvunjike, CCM wakakataa. Zikapigwa kura, CCM wakashinda Ukawa wakatoka nje.

Tusitegemee CCM kutengeneza Katiba mezani iwasaidie CUF waliowashinda vitani, au CDM waliowashinda uchaguzi. Dunia ndivyo ilivyo, na CUF wakipata hawatoachia.
Ndugu yangu hawa watu wanaojiita UKAWA nafikiri uwezo wa kufikiri mdogo sana. Wanalalamikia Tume huru ya Uchaguzi, Katiba Mpya nk. Swali ni kwamba nani awape? CCM ni Chama Tawala eti kijiandalie kuondoka madarakani kwa hiyari yake!! Ilitokea Nchi gani hiyo?
 
Wew
Mkuu kuna factors mbili, ''internal and external''

External: Ni kweli kuwa wakurugenzi wanaochaguliwa na mwenyekiti CCM hawaweza kutenda haki. Tuliona hili pale jina la mtu lilipoondolewa na kisha kurudishwa

Tume ya uchaguzi: Hili tumeliongelea sana. Tunakumbuka Lubuva alivyoyumbishwa kila mara, leo tutatumia vifaa vya kisasa, kesho hili keshokutwa lile
Ukitazama, tume ilikuwa inafanyia kazi maagizo ya serikali ya CCM

Wajumbe wa tume kubadilishwa siku za mwisho wa uchaguzi kwasababu Rais(mwenyekiti wa CCM) ana mamlaka hayo.

Wajumbe hao sasa wana nyadhifa nyeti. Inaeleza kitu

Polisi na vyombo vya dola kutosimamia haki, hilo halina mjadala

Internal
CDM hawakuwa na mgombea mwenye ushawishi.
Dr na Mbowe wameongoza 'failures' za kutosha ni unlikely wangekuja na kitu tofauti

Focus ya CDM ilikuwa kupata abunge wengi na pengine kudhibiti 2/3. Ingewezekana

Kubadili mgombe dakika za mwisho ilileta sintofahamu miongoni mwa wapiga kura.
Na kwa bahati mbaya mgombea hakuwa na muda wa kujieleza

Tumaini la wabunge kwa jitihada likafa ikitumainiwa mgombea angekuja na wenyeviti20. Hawakuja na waliokuja hawakuwa na impact

Kwa hilo wakapoteza focus ya Bunge na kujikita kwa mgombea waliyetegemea

Mgombe aliyekuja hakuwa na ushawishi. Kuzindua kampeni ilikuwa failure ya kiwango cha juu. Watu walitegemea mafuriko zaidi ya message. Hakukuwa na message yoyote

Pamoja na kutokuwa na message mgombea hakuwa tayari kujisafisha

Ilikuwa mikutano ya dakika 5 ikitegemewa wingi wa wahudhuriaji ungetosha.
Wahudhuriaji waliondoa bila message na hilo liliawaathiri sana

Ukichanganya factors zote utaona kwanini walishindwa.

Moja za nje ambazo hawakuzizuia tangu awali. Huwezi kwenda uchaguzi ukijua ni unfair

Pili, kwa kutumia nguvu ya umma, hakukuwa na ushawishi kutoka kwa mgombea

Tatu, focus ya jitihada ikaondoka na kutegemea majaliwa ya mgombea

Suala ni kuhakikisha walioongoza 'failures' za siku za nyuma wanakaa pembeni.

Hapa nina maana Mwenyekiti wa CDM na timu yake

Halafu timu mpya ndiyo itaangalia nini cha kufanya mbele ya safari
Uzembe wao wa kutomuandaa Mgombea kwa matarajio ya kusubiri makapi ya CCM!
 
..huyu anayewaambia wananchi "MWAFAA " nadhani ni mbaya zaidi.
Hata uchaguzi ungerudiwa kesho cdm wakamweka lowasa au sumaye, kura yangu nitampa huyo mwafa japo mimi ni cdm member tangu 1998.
Ninawachukia aina ya wanachadema wanaosema cdm hata ikiweka jiwe watalipigia kura. They've given mbowe & co a free ride, and hopefully you're not one of them.
 
Yote Tisa ila JECHA ni kielelezo cha kuwa CCM haiwezi kutoka madarakani kwa njia ya sanduku la kura ...
 
Hata uchaguzi ungerudiwa kesho cdm wakamweka lowasa au sumaye, kura yangu nitampa huyo mwafa japo mimi ni cdm member tangu 1998.
Ninawachukia aina ya wanachadema wanaosema cdm hata ikiweka jiwe watalipigia kura. They've given mbowe & co a free ride, and hopefully you're not one of them.

..naheshimu msimamo wako.

..lakini binafsi siwezi kumpigia kura mtu abusive, katili, mbaguzi, na fisadi, kama huyu.
 
Back
Top Bottom