MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,350
- 40,118
Habari JF. Nimeona leo nami nichangie mawazo kuhusu siasa za hapa nchini. Wakati tulio nao ni ule wa kila mtanzania kutaka mabadiliko kwa mfumo mzima unaoongoza maisha ya kila siku. Niseme pia mabadiliko yanayohitajika hayana ulazima wa CCM kutoka madarakani maana wapinzani wengi hudhani mabadiliko watu wanayoyataka ni upinzani kuingia ikulu. Kwa fikra hizo tu wapinzani wanafeli. Ninasema wapinzani hawawezi kuupata uongozi wa nchi maana bado mikakati yao sio imara na uminyaji wao wa demokrasia ni wa hali ya juu. Kwa sasa Tanzania nzima tunaongelea mchakato wa uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM ambapo UKAWA ni kimya na inavyoonekana mgombea wao hatapatikana kwa demokrasia iliyo wazi. Huko arusha hakuna tena mambo ya CHADEMA ni CCM hasaLowassa. Nahitimisha kwa kuwakumbusha wapinzani kubadilisha fikra zao ili kuikabili CCM yenye mbinu nyingi sana za ushindi.