majata
JF-Expert Member
- Oct 7, 2010
- 431
- 179
Pamoja na uwezo mzuri wa kusimamia serikali ambao mnajitahidi kuuonyesha, inabidi sasa mbadiliashe mbinu za siasa, maana siasa zenu zimejaa ulalamishi, na ukinzani tu wala hamuakisi kama ndio waendesha serikali mbadala, kwa zaidi ya miaka 10 tunazungumzia RICHMOND, EPA, BUZWAGI NK, Mambo ambayo yamekwishatokea, hatuwaoni mkisimamia serikali kuhakikisha hayatokei tena badala yake mnasubiria yatokee ili mpate la kuongea.
Tunapoteza muda kwa mambo yaliyopita kwa kulaumiana badala ya kujipanga yasitokee tena, sina maana hatupaswi kuyazungumzia ila maana yangu ni umuhimu wa yaliyopita ni mdogo zaidi kuliko yajayo, hakuna sababu ya kutumua miaka mingine zaidi tukizungumzia mambo yaleyale na tukasahau kudhibiti mengine yasitokee.
Mnawafanya watanzania nao wakwamie katika fikra zenu ambazo mnawaaminisha.
Badilisheni mbinu anzeni kutuonyesha kweli nyie ni akili kubwa,tengenezeni mifumo elimishi katika nyanja zote, kuanzia kilimo mpaka tekinolojia, msiishie kwenye kupiga kelele ambazo tayari watanzania washaanza kuwaona ninyi hamna tofauti na hao mnaowaongelea maranyingi, tuonyesheni upinzani ni maendeleo nasio kupingana tu.
Wasaidieni watanzania kuwaonyesha ni nini wafanye ili maisha yao yaboreke nasio kuwadumaza kiakili Wakae wakisubiria mgao wa epa au richmond ambao uliishakuwa zilipendwa, tutumie nguvu kubwa kujadili mbinu mpya zitakazotutoa hapa tulipo.