Wapiganaji wa UDSM wapiga hodi Bungeni

Wapiganaji wa UDSM wapiga hodi Bungeni

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Baada ya majina ya wagombea wa CCM na UKAWA kutolewa,majina yaliyochomoza yamenikumbusha miaka kadhaa ya nyuma. Yamenikumbusha kuanzia mwaka 2005 nilipojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya Shahada ya Kwanza ya Sheria. Ndani ya UDSM kuna Serikali ya wanafunzi chini ya kivuli cha Dar es Salaam University Students Organisation (DARUSO). DARUSO ina Rais,Makamu wa Rais, Waziri Mkuu,Mawaziri,Wabunge na kadhalika.

Hapo UDSM nilikutana na majina ya wagombea Ubunge wa sasa. Wapo waliokuwa viongozi wakuu katika serikali ya DARUSO na hata waliokuwa wanaharakati/wapiganaji. Hawa wanaharakati walikuwamo serikalini DARUSO au hata nje ya Serikali na walikuwa na ushawishi mkubwa. Walikuwa ni hata 'king makers'. Hapa chini nitawaelezea baadhi ya wapiganaji wa UDSM ambao wamepiga hodi Bungeni kwakuwa ni Wabunge watarajiwa. Wanakumbukwa kwa siasa na upambanaji wao UDSM.

Mwaka huo 2005, nilimkuta Kamanda Mwita Mwikwabe Waitara akiwa Rais wa DARUSO. Alikuwa ni kiongozi mwenye kujiamini,mjenzi wa hoja,mahiri wa kujibu maswali na mthubutu. Mwikwabe aliitumia vyema Revolutionary Square (mahali pa mikutano UDSM) kujibia hoja na hata kutoa taarifa nzuri na mbaya kwa wanachuo. Leo hii,Mwita Mwikwabe ni mgombea Ubunge wa CHADEMA/UKAWA jimboni Ukonga.

Waziri wa Mikopo wa Rais Magesa Mwita (Wizara iliyohusika moja kwa moja na boom na hata migomo mingi) alikuwa Ndugu Julius Mtatiro. Mtatiro atakumbukwa kwa upiganaji wake hasa kuhusu maslahi ya wanafunzi. Mtatiro hakusita kutangaza na kusimamia migomo ya wanafunzi UDSM kama maslahi yao yameguswa na hivyo alikuwa mtetezi hasa. Mtatiro alikuwa Waziri Mkuu wa DARUSO katika Serikali ya Rais Deo iliyofuata na baadaye alijiunga CUF alipo hadi leo.Anagombea jimbo la Segerea kwa CUF/UKAWA.


Unapotaja wapambanaji na king makers wa UDSM, huwezi kuwaacha akina Kamanda David Silinde na Stephen Owawa. Hawa walikuwa wanaharakati hasa. Silinde alikuwa Mbunge wa Bunge la DARUSO akiwakilisha Faculty of Commerce (FCM) ambayo kwasasa inaitwa UDSM Business School (UDBS). Owawa naye alikuwa Mbunge wa DARUSO kutokea FCM huko huko.

Hawa walikuwa na nguvu ya ushawishi kutokana na ujenzi wa hoja zao ndani na nje ya Bunge la DARUSO. Silinde alishakuwa Mbunge wa Bunge la Tanzania wa Jimbo la Mbozi Magharibi-CHADEMA na sasa anagombea Jimbo jipya la Momba. Stephen Owawa ameteuliwa na CHADEMA/UKAWA kuwania jimbo la Rorya.

CHADEMA/UKAWA pia imemwamini mwanadarasa wangu wa UDSM-2005/2009,Jonas Kalinde kuwania Ubunge Mpanda Vijijini. Ingawa hakuwa mwanasiasa hasa chuoni, Kalinde naye yuko vizuri. Kimsingi, hawa wote ni mazao ya siasa za UDSM. Wameivishwa pale na sasa wako tayari kuwatumikia wananchi wa Tanzania. Wanazo sifa za kuwa viongozi hapa nchini. Kila la kheri Mwikwabe, Mtatiro, Silinde, Owawa na Kalinde!
 
Badae ulikuja Mwamba mmoja kutoka Uganda Odwong Odwaa nakumbuka alirudishwa kwao na Serikali.
Was Great Old Gold days, kuna Jamaa yao Bush yeye aliajiriwa UDSM utawala.
 
Masahihisho...Julius Mtatiro alikuwa Waziri wa Mikopo kwenye Serikali ya Mwita Magessa 2006/2007(kutoka COET) ambaye alimpokea Mwita Mwikwabe Waitara. Waziri wa Mikopo wa Deo (Mtatiro akiwa Waziri Mkuu) alikuwa Buhenyenge Josphat maarufu kama Bush.
 
Masahihisho...Julius Mtatiro alikuwa Waziri wa Mikopo kwenye Serikali ya Mwita Magessa 2006/2007(kutoka COET) ambaye alimpokea Mwita Mwikwabe Waitara. Waziri wa Mikopo wa Deo (Mtatiro akiwa Waziri Mkuu) alikuwa Buhenyenge Josphat maarufu kama Bush.

Asante Mkuu
 
Back
Top Bottom