BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,186
Date::6/27/2008
Wapigakura wamtaka mbunge wao akae kimya bungeni
Frederick Katulanda, Sengerema
Mwananchi
BAADHI ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza, Jimbo la Buchosa, wamemtaka Mbunge wao, Samwel Chitalilo, aliyeibuka bungeni kumtetea aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, kukaa kimya kwa vile alichosema hakiwakilishi mawazo yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa Mwananchi wilayani jana, baadhi ya wananchi hao walisema kuwa kitendo cha mbunge huyo kumtetea Chenge kinaonesha kuwa anatetea asichotumwa na wananchi.
Mkazi wa jijini Mwanza, Sikujua James alisema katika kipindi cha bunge kuupiga vita ufisadi, baadhi ya wabunge akiwemo Chitalilo wameonyesha kutokuwa na nia njema nchi hii na wapo bungeni kwa ajili ya kutetea mambo yasiyofaa.
Alisema kuwa kauli iliyotolewa na Chitalilo na wabunge wengine, imeonyesha kuwa majimbo mengi hayana waakilishi wa wananchi bali wanakwenda bungeni kwa matakwa yao badala ya kuwatetea wapiga kura wao.
"Hivi kweli Mbunge kama Chitalilo anaweza kusema hajui maana ya mwizi mpaka atueleze kuwa ni yule anayevunja mlango tu?" alisema na kudai Chitalilo amedhihirisha yuko bungeni si kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi..
Naye Kamalamo Nasatu mkazi wa wilayani Sengerema alisema kuwa amesikitishwa na kauli hiyo na kumuomba mbunge huyo kuomba radhi wananchi na hasa wa jimbo lake kwa sababu kauli yake haikuwasilisha mawazo yao.
"Inafahamika kuwa mbunge anapozungmza bungeni huwa anawakilisha mawazo ya wanapiga kura wake na kwa kauli hiyo anataka kutuhusisha wakazi wa Buchosa na ufisadi na kwambwa tulimtuma bungeni kutetea ufisadi. Hiyo ni kauli yake na tunaomba atuombe radhi na kufafanua kuwa hayo yalikuwa mawazo yake na si yetu," alieleza Nasatu.
Naye Jane Dickson alidai kuwa kinachotokea sasa bungeni kudhihirisha kuwepo kwa nia ya dhati ya baadhi ya wabunge kupambana na ufisadi na wanaotetea ufisadi, hali ambayo alieleza kuwa inaweza kusababisha kuhatarisha amani ya nchi hii.
Alisema hali hii ikiendelea italigawa taifa katika makundi mawili yanayoweza kuwa ni mabaya kwa vile anaamini watetezi wa ufisadi wamejipanga kikamilifu kulinda ufisadi wao na wako tayari kuutetea hata kwa kumwaga damu.
Aidha Frank Barnabas alisema kuwa kuibuka kwa makundi yanayotetea ufisadi kunatokana na aina ya wabunge waliopo ambao alisema wameteuliwa kutokana na vigezo vya kujua kusoma na kuandika, kushauri vigezo hivi vimepitwa na wakati kutokana na dunia kukuwa kiteknolojia.
Mbunge Chitalilo Juni 24, mwaka huu wakati akichangia katika hotuba ya Waziri Mkuu bungeni, alisema aliwataka wabunge wenzake kuacha kumsakama Chenge kwa vile yeye si mwizi na hajawahi kuvunja nyumba ya mtu kwa lengo la kuiba.
Chenge alijiuzulu uwaziri baada ya kudaiwa kuweka kiasi kikubwa cha fedha huko Kisiwa cha Jersey ambazo alikiri kwamba ni zake, lakini hazihusiani na ununuzi wa rada.
Mbunge huyo akimtetea alisema kwamba, alizitaka benki ambazo zimekuwa na tabia ya kutoa siri za wateja kuacha kufanya hivyo.
Sambamba na kumkingia kifua Chenge, mbunge huyo pia alidai kuwa ni jambo la kushangaza kuona kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimzungumza vibaya Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakimhusisha na masuala ya ukiukwaji wa maadili.
Vilevile, Mbunge huyo alipongeza juhudi za aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye alijuzulu kutokana na sakata la Richmond, akidai aliwajibika kwa sababu za kisiasa.