simba29
Senior Member
- Jun 22, 2011
- 193
- 67
-S1mba
Nakuhitaji rafiki,
Ulienifaa kwa dhiki,
Nasema bila unafiki,
Safari bado hata kesho hatufiki,
Nilikuhitaji ili kusema,
Kukosoa au sifia mema,
Kuandika na watu kusoma,
Bila wewe nisinge jenga hema,
Tabia zako nzuri,
Zenye wingi umahiri,
makini mwenye Moyo jasri,
Rafiki wa kweli linifaa si siri,
Wengi hawakuelewi,
Maneno maswali hawaishiwi,
Dhihaka na makwazo hawakawii,
Wanashangaa huna roho ya kiwi,
Wapi umekwenda? ,
Niko peke ninawanda,
Rafiki gani hukumpenda?
Au ni mimi chanzo mbali ukaenda?
Sikukuthamini kukutunza,
Uwepo wako kuukwanza,
Mie mjuaji ndo unanifunza,
Nijute kwa nilivyojiponza,
Nilikupata kwa jasho,
Hata damu na mingi michosho,
Na sasa maumivu yangu posho,
I dhaifu nafsi kama jeans mdosho,
Nalia sauti inazimwa,
Nikisema maneno yanaumwa,
Nikijenga mafundi wanakunwa,
Rudi rafiki nimechoka huu utumwa.
?2015
Nakuhitaji rafiki,
Ulienifaa kwa dhiki,
Nasema bila unafiki,
Safari bado hata kesho hatufiki,
Nilikuhitaji ili kusema,
Kukosoa au sifia mema,
Kuandika na watu kusoma,
Bila wewe nisinge jenga hema,
Tabia zako nzuri,
Zenye wingi umahiri,
makini mwenye Moyo jasri,
Rafiki wa kweli linifaa si siri,
Wengi hawakuelewi,
Maneno maswali hawaishiwi,
Dhihaka na makwazo hawakawii,
Wanashangaa huna roho ya kiwi,
Wapi umekwenda? ,
Niko peke ninawanda,
Rafiki gani hukumpenda?
Au ni mimi chanzo mbali ukaenda?
Sikukuthamini kukutunza,
Uwepo wako kuukwanza,
Mie mjuaji ndo unanifunza,
Nijute kwa nilivyojiponza,
Nilikupata kwa jasho,
Hata damu na mingi michosho,
Na sasa maumivu yangu posho,
I dhaifu nafsi kama jeans mdosho,
Nalia sauti inazimwa,
Nikisema maneno yanaumwa,
Nikijenga mafundi wanakunwa,
Rudi rafiki nimechoka huu utumwa.
?2015