Wapi Nitapata Mkopo wa TZS 10M Haraka?

ziko bank ambazo unaweza pata mkopo fasta kama Access, Equity na Advanc (sina uhakika nao saana) na Akiba (hawako fast saana), wanaangalia cash flow yako, balance sheet,
 

Kuna jamaa anakopesha kwa 20% per month!!! Una surrender hati na gari kwake na unaandika kabisa ukishindwa atajichukulia mali zako bila masuala ya mahakama!! Hati ni lazima ifanyiwe search na kufungwa ili usiweze badilisha maana wengi hamchelewi kusema imepotea na unapewa nyingine!! gari lazima iwe na thamani na ichekiwe TRA!!
 
be careful but better uende kwenye bank institution usije ukalizwa.Kama issue ni kupata mkopo faster jaribu<br />
1.BANC ABC<br />
2.PIA EQUITY BANK<br />
3.AFRICAN MICROFINANCE hawa wako survey
kama sijakosea ABC wanahudumia wafanyakazi wa serikalini
 
Big Lady, ulishafanikiwa?

Kama bado, kuna hawa jamaa pia, niliwahi kuongea na Director wao, lakini alikiri kuwa riba yao ni kubwa kiasi, sikumuuliza ni %ngapi... wanaitwa Superior Financing Solutions, wapo Kinondoni 58 Uporoto, Ursino Estate. Simu +255 736 502 026. Email: info@sfs.co.tz
Wavuti: www.sfs.co.tz (personal mobile no. ya Director wao ni +255 713 250 830). Waweza jaribu kucheck nao kama watakidhi kusudio lako.

Kila la kheri.
 
Nenda benki ya Akiba au Mkombozi pamoja na business plan yako. Ukitimiza masharti unapewa.
 
Siku hizi watu hawaamini sana so yaweza Kuwa ngumu sana kumpata mtu atakayekukopenda hiyo amount. Kama mwenzetu alivyo kushauri hapo juu, ni vyema uende bank, nadhani kuna bank ambazo process yao ni ya kama 2 days (24hrs) unapewa mkopo

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Asante sana wadau.

Nimejaribu Equity; CRDB; FNB; Azania; Barclays; KCB; DCB kote wanalietea mapause! So nimewapotezea!

Kuna Mdau kanipatia TZS 5M bila masharti namrudishia January 2013. So bado natafuta TZS 5M.

Shida ni kuwa Hati haiko katika jina langu japo nyumba ni yangu. Niko katika Mchakato wa kuibadilisha almost 9)% done!
 

Umeona eeh! Chezeya wenye pesa weye?

Nyumba ina thamani ya around TZS 300 Milion.

Ni vile tu katika maisha kuna kupanda na kushuka. Nikijua terms zake kwa uwazi naweza kuchukua hata January au February nikamrudishia.

sasa nnaanza kukuelewa kumbe shida yako upewe bila mashart!!!!
bank zote kuna mashart na vigezo + riba ila wewe yawezekana unataka kutumia mali za urithi kuchukulia mkopo! Bank wanakuita Problematic client, kuweni makini wadau
 
Big Lady unauzoefu na Micro Finance? Nenda pale Sinza Mapambano jengo la mwanamboka kuna EFL watakupa mara moja,Uwe na mdhani na salary slip na hizo securities zako.Ni PM kwa maelezo zaidi
hahahaha,,mimi ni mdau mkubwa wa pale
 
Yah, lakini nafikiri kwa bank kiasi hicho ni lazima awe na business plan ambapo pia watahitaji bank statement yake kuonyesha transactions za huko nyuma. Hivyo suruhisho ni kukopa toka kwa wajasiliamali ila masharti yao ndo kama hayo ya kusaini deed of transfer na kama hujalipa katika muda mmekubaliana property ndo inakwenda tena.
KAMA UNA SECURITY YA HATI YA KIWANJA NA KADI YA GARI ambavyo havina mashaka KWANINI USIENDE BANK?
 
Big Lady huwezi kupewa hela zote hizo bila masharti. Benki wanakopesha pesa ambazo sio zao ni za wateja wao hivyo lazima wawe na uhakika kuwa hiyo pesa wanayokupa itarudi. Usiogope kutimiza masharti. Mbona wenzio tunakopa huko na kuzirudisha? Benki ndio mahala pekee utakapopata hela yoyote uitakayo ila lazima wajiridhishe kabla ya kukupa. Usiogope mamy.
 
Asanteni sana.

Kuna Wadau wamenikopesha tena bila masharti na January nazirudisha. In fact nimepata zaidi ya nitakazo:

$ 10,000 + TZS 3.5M + TZS 2.5 M + TZS 2M.

Kumbe Mujini napaweza.

Mbarikiwe wote mliotoa michango yenu hapa.
 
Biglady, umenikumbusha M-mama mmoja hapa ofisini. Anaweza kuja anahaha kutafuta pesa kwa njia yoyete na kwa gharama yoyote lakini kumbe zote zinaishia kwa ka Serengeti! nalaani sana tabia hiyo. Najua wewe unazitaka kwa kitu cha maana.
 
KAMA UNA SECURITY YA HATI YA KIWANJA NA KADI YA GARI ambavyo havina mashaka KWANINI USIENDE BANK?


Mkulu

Hapo ndipo wengi wanapokosea,
benki wanakopesha biashara, collateral siyo biashara.....kimantki ni kwamba collateral kama ilivyo hai-generate kitu.....

S
ize ya mkopo inategemea zaidi na economic viability ya project plan uliyowasilisha...

Hata uende na hati ya ghorofa...bila project....hupati kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…