Wapi nitapata daktari mzuri wa meno?

nimuchu

Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
30
Reaction score
4
Wapendwa naomba msaada wa wapi nipate Dr mzuri wa meno? Nasumbuliwa na meno ya juu ya mbele kuweka weusi na baadae kumeguka ila hayana maumivu. Nilienda hospitali moja ya meno Dr aliyasafisha tu na kuziba ila tatizo bado na mengine yanaendelea kumeguka. Nataka suluhisho la kudumu hasa ukizingatia meno ya mbele ndio mapokezi ukicheka au kutabasamu. Msaada wenu ni muhimu sana kwangu. Ubarikiwe
 
mpendwa nenda Muhimbili kitengo cha meno ukiingia tuu getini upande wa kulia .Muulizie Dr George au Dr Agrey wapo vizuri sana
 

mdau usihangaike mitaani nenda pale muhimbili school of dentistry kuna wataalam wa uhakika kabisa
 
nimekuja mbio nilipoona kichwa kinasema daktari wa meno, mi nilifikiri meno ya tembo, kidogo nikuarest
 


mkuu arusha kuna hospitali ya Wasabato iko vizuri sana.
 
Wapendwa nawashukuru wote kwa msaada na ushauri wenu. Nitaufanyia kazi. Mungu awabariki sana
 
nenda dodoma kuna sehemu inaitwa ntyuka kuna mission hospital moja hakuna tanzania nzima kwa mambo ya meno nakwambia hakuna
 
Dodoma, panaitwa DSYC kama sijakosea.
 
Meno ni matunzo tu. Kumbuka kupiga mswaki mara 2 au tatu siku lakini mara mbili tu naona kwangu mimi inatosha sana, baada ya kuamka na kabla ya kulala. Tumia dawa nzuri ya meno kwangu mimi triple action colgate naona imenipunguzia sana matatizo ya meno. Hapo awali nilikua naatend clinic ya meno Dar group, kwa sasa nimeacha na baada ya kuanza kutunza meno vizuri shida zote zimeisha. Unapopiga mswaki usitumie dawa kidogo sana tumia dawa ya kutosha kucover mswaki wote hapo juu ya brush. Hakikisha baada ya kula mabaki ya chakula hakibaki katikati ya meno au kwenye meno kwa ujumla. unaweka maji kinywani na dawa halafu unachezea mixture hio mdomoni mpaka uhakikishe kila kitu kimetoka baada ya kula. Kinyume na hapo, meno pasipo matunzo hata uende marekani kutibiwa ni bure.
 
Jamani kwa DSM zaidi ya muhimbili niwa kwingine, nami nina mtoto wangu meno hayapo vizuri.
Naombeni msaada pls.
 
Ila bei yao imechangamka kung'oa jino moja ni 90,000.
 
Mi nilimpeleka mtoto wangu wameng'oa jino mtoto hakulia hata kidogo na baada.ya dk 45 aliweza kula nyama kama kawaida
 
Jamani kwa DSM zaidi ya muhimbili niwa kwingine, nami nina mtoto wangu meno hayapo vizuri.
Naombeni msaada pls.
Hindu mandal hospital.. Anaitwa Dr.Kenny.. Ni around 35- 60k gharama. Na bima wanapokea nadhani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…