Umetumia dawa kwa mda gani.? Kwanza itabidi ujue hiyo HTN yako ni primary au secondary. Kama ni primary itabidi ufanye lifestyle change kama kupunguza chumvi,stress,mafuta,kahawa na kufanya mazoezi.
kama ni secondary itabidi watreat kwanza pathology inayokuketea hiyo shida then ndio waendelee kudeal na pressure yenyewe.
Kwa hiyo issue sio dawa tu kuna factors nyingine za kuangalia, ikiwa unameza dawa lakini mambo mengine hayajawekwa sawa hiyo ni sawa na kujaza tumbo tu.
Mi naona ushauri wa kumfuata daktari kwenye clinic yake ya nje ni mzuri maana ukimfata muhimbili pale kunakua na wateja wengi sana hawezi kukusikiliza kwa urefu kiasi hicho.