Wapi Dr.Mvungi na Prof.Baregu?

MJIMPYA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
506
Reaction score
273
Wandugu,
Baada ya kupewa kazi na Mh Rais ya kuwa wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba, wapinzani hawa wamekuwa kimya kabisa.
Je ina maana kabla ya kazi hiyo walikuwa "loose" na kupata muda wa kupiga siasa ambao kwa sasa hawana?

Je ni ile posho nzuri ya kufa mtu wanayopokea kwenye tume ndo imewafanya wafunge mdomo?

Je ina maana hata wanasiasa tunaowaona wakipiga domo kila siku wakipata kazi kama hizi ndo basi tena?

Nina wasiwasi na hatima ya siasa zetu kama watu wale wanaoaminiwa kupita kiasi wanageuka wananchi pale wanapopata masrahi yao. Tujikumbushe enzi za mzee Seif wa CUF, Mrema n.k
 
Labda hawapewi majukumu na vyama vyao kwa sasa. siasa za bongo ni biashara tu wazalendo wa kweli ni adimu sana.
 
Huenda wamepata walichokuwa wanataka. Si unajua ulaji
 
Njaa mbaya, hata wasomi wanaumbuliwa na njaa mkuu.
 

Samahani nikukumbushe ile ni tume ya mabadiliko ya Katiba ya Nchi siyo ya Chadema au CCM..Masharti yake ni pamoja kuwa nje ya mipaka ya kichama. Wakimaliza kazi utaona watazungumzia kila kitu hata yale mapungufu pia. Ujue wanafanya kazi kwa kiapo sio kwa political interest..hivyo tuwavumilie kidogo watarudia tu hali zao hao wengine waliopo pamoja na wewe "Great Thinker?" katika kuongelea mambo yalivyo na siasa za Tanzania.
 
Huwezi kuchanganya mambo wakati unapokea mawazo ya aina mbalibali na watu mbalimbali. Mbona huulizi kuhusu Warioba? Au wengine? Fikiri kabla ya kuandika sio kusukumwa na utashi wako au kebehi.
 
njaa mbaya hata slaa alikubar kugombea urahisi na kuacha kugombea ubonge baada ya kuambiwa atapewa mshahara kama mbonge hata akishindwa urahisi na sasa kajikopesha mkopo kama wa wabonge
 
Sasa hivi wako kitaalam zaidi, wanafanya kazi chini ya kiapo maana yake ni kuwa wanayoyasikia na kuyaona wayaweke kwenye maandishi na sio midomoni mwao na kuanza kuyasema. Baregu sio wa kunyamazishwa na pesa. Wala sio mpesapesa kama maprof wenu wa siku hizi. Yule ukitaka kumfurahisha ni wewe toa hoja nzito yenye takwimu na mifano hai hapo utakuwa umemaliza kabisa lakini sio number of zeros in his account. NO. Anapenda usomi kuliko hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…