habari wanajamii. Naomba kufahamu mahali alipo mgombea ubunge wa jimbo la mtama huko lindi kwa tiketi ya ccm?? Maana ni muda sasa yapata kama wiki ya tatu sijamsikia harakati zake kwenye kampeni. Kwa mnaofahamu alipo naomba mtujuze. Asanteni
Jana alikuwa Mbeya, walikuwa wakikusanya watu kwa vitisho kwenye masoko na kuambiwa eti wasipoenda kumsikiza watafukuzwa kwenye masoko wanakotafutia Riziki zao.
Alikuwa akihutubia Kata ya Iyela, uwanja wa Ndege wa zamani, akawa anaponda Ukawa ila kwa hofu kubwa.
Nape hana chake tena.
Nnape anajiandaa kuingia bungeni kuliwakilisha Jimbo la Mtama, hahitaji kufanya kampeni kwani ameshapita na wananchi wanamkubali, mnadhani mnatusumbua na Hao vijana wenu mnaowalipa waonyeshe kuwa Nape hakubariki? Wangefanya hivyo wazee na akina mama tungejiuliza nini kinaendelea sio Hao vijana wenu, mbinu na hila zenu zote zimeshindwa, Nape ndiye mbunge wa Mtama