Wapenzi wangu wa zamani wamepigwa na bwana zao, wote wamejikuta wapo kwangu usiku wa manane

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,809
6,081
Habarini Chiefs

Kiukweli mimi Kudo,mara nyingi huwa sipendi ugomvi na mwanamke niwae kimahusiano,na tabia hii imepelekea wanawake niliodate nao kushindwa kuelewa kama nimewaacha au bado nipo nao,ila ukweli huwa ninao Moyoni kujua huyu anifaa au nimempiga chini
Binafsi siamini katika kupigizana kelele mwanamke maana huwa nahisi kama hawajaumbwa kutukanwa au kupigwa hasa kama wamekosea,naamini katika kukaa kimya au kumwelekeza katika lugha nyepesi tu asipoelewa basi huwa nipo kimya sana jambo gumu linakuja pale nikinyamaza wengi hudhani nimewadharau basi kimbembe kitaanza ila nakula buyu hadi mambo yataisha.

Mara nyingi mimi huwa sikai mkoa mmoja kulingana na shuguli zangu lakini hata kama nikizunguka najua lazima nitarudi mkoa niupendao ambapo ndipo yalipo makazi yangu kiujumla.

Katika huu mkoa ninao ishi nilikutana na binti flani nikampenda nae akakubali kuwa na mimi,nilimpa kila alichotaka na nilipokosa nilimwelekeza akaelewa,lakini nikaja kugundua hakuwa mkweli kwangu,hilo sikujali na nilichoamini mimi ndie napaswa kuhakikisha nafanya niwezavyo awe wangu bila kumbugudhi katika mahusiano yake mengine,lakini jitahada zikawa zero,bado aliendelea kusaliti,sikumwambia chochote,wala sikumwambia kama najua sio mwaminifu,hivyo nikaanza kumwepuka bila kelele,hilo nilifanikiwa nusu mana aligundua nimebadilika,akaniuliza nikamwambia ukweli wa maovu yake,hakujali japo aliomba msamaha lakini aliendelea na tabia yake.
.nikaona isiwe kesi,namimi nikaanzisha mahusiano na mtu mwengine.

Likawa kosa,hasa alipogundua ninae toka nae,vikawa vitimbwi,mara wapigane,wasutane yani fujo kila kukicha,nikawaita wote siku moja,nikawaeleza tabia zao sio njema na kila mtu ana mapungufu yake,ila yule wa kwanza nikamwambia achague machaguo mawili tu kuachana na mimi au nimtwange makonde,ooh akaona bora ajiondokee lakini akiebaki nae nikampa onyo asije kupigana au kufanya fujo popote kwa ajili yangu,akakubali yakaisha.

Yaliisha kwangu ila kumbe wanavinyongo vyao.

Huyu niliebaki nae akatangaza ana mimba yangu.
Katika maisha yangu naamini mtoto hata kama sio wako ni baraka kuwa nae,lakini pia huwa najiuliza nikikataa mimba Leo kesho akazaliwa na kweli ni damu yangu nitamtazama vipi huyo mtoto,sipendi hayo yatokee,lakini kubwa zaidi sitaki mwanangu alelewe na baba mwingine,hivyo nikamwomba nipeleke posa kwao mtoto azaliwe ndani ya ndoa,.

Baada ya posa tu,wiki la kwanza mimba ikatoka,hee bundi kaingia mapema kabisa,na baada ya hapo nikasikia mengi kuhusu tabia ya yule binti na mengi hayakuwa ya kufurahisha.
Mwezi mmoja baada ya kutoa posa na mimba kutoka, nikawa nimetoka kidogo siku narudi sikumwambia,hivyo nilipofika tu nikaenda mitaa ya kwao kuonana nae,ee bana we nikakuta kabambiwa na njemba,sikufanya kitu,nikarusu njemba asepe na kisha nikamwita,akakimbia kwenda kwao kisha akaniandikia text
"naogopa utanipiga,nakuogopa B,we upo kimya sana utaniua"

Sikumjibu nikasepa,lakini nikawapa taarifa home,mwanamke hafai kuwa mkwe wao,na mimba katoa.

Alikaa kimya na mimi nikakaa kimya,kawasimulia wa kwao,na mashoga zake,wakampa ujanja,ya kuwa aje kwangu abebe vitu vyake na vyangu hivyo naweza kwenda kwao tukasuluhisha yakaisha.

Nilitoka safari yangu narudi Home,nakuta nyumba nyeupe,hata shuka hamna,imajini vyumba viwili na sebule,vimekombwa vitu vyote nikaachiwa mabegi ya nguo tu.
Majirani wakanitonya ni mchumba wako na dada yake wamesomba vitu na Guta.
Dunia yoote nikaona ipo kwangu
Nikatuliza akili nikaona nikienda kwao nitaua mtu,nikaondoka hadi gesti,ahsubuhi nikatafuta chumba mtaa wa kumi huko,nikaanza upya.

Miezi kadhaa baadae nikawa naona picha tu instagram akiwa na bwana mpya,nikasema yote heri.

Sasa oneni jana ilivyokuwa

Nilikuwa ndo nimefika nikitokea Mwanza,nikachelewa kulala na sababu ya kuchelewa nilikuwa naandaa kitu flani kwa sababu ya kazi ya ahsubuhi,lakini mtaani kwetu pia kulikuwa na sherehe si mbali na nyumba ninayo ishi,sasa katikati ya sherehe mida ya saa sita hivi wale mabinti wakakutana vyooni,mmoja akaanza kumnanga nwenzie kuhusu mimi,e bana ukazuka ugomvi wa karne,watu huku na huku wakaingilia,kujua sababu wananitaja mbele za mabwana zao waliokuwa nao usiku huo,mabwana nao wakaona huu ujinga wakashusha kibano.
Sasa huku na huku masela wakawadaka kama kutaka kumsaidia binti mmoja aliekuwa ameelemewa na kichapo,nae akakimbia vijana wawili wakatoka nyuma yake.

Nikiwa ndani nikasikia sauti kwa mbali ya mtu ninaemfahamu,sauti ikazidi kusogea,nikamfahamu mwongeaji alikuwa anajaribu kujinasua vijana walitaka kumla mande,haraka nikatoka nje,ile natoka tu nje akakimbilia ndani ya geti wale vijana nikawavaa maana walikuwa saizi yangu,kisha nikawaacha waondoke wakatii bila mbwembwe.
Wakati nataka kufunga geti nikasikia tena kelele,ila sauti naijua pia,na punde kelele zikafika nilipo alikuwa ex wangu mwingine anakimbia kipigo cha bwana wake.
Aliponiona nje bila kujua akakimbilia kwangu ili nimpe msaada nikampisha akaingia ndani ya geti,punde wakaja mambwana zao,hadi pale Home,mabinti ndani wanataka kukimbilia ndani huku jamaa nimewazuia getini,kisha wakatoka wapangaji wenzangu,tukayaweka sawa jamaa wakatuliza mzuka,ikabidi niulize sababu maana walikuwa wameumia sana wale mambinti na walihitaji huduma ya Kwanzaa.
Jamaa mmoja akaeleza kuhusu ugomvi ulivyokua na kila mara alikuwa akitaja jina langu,sasa demu akamuuliza unae mtaja unamjua?
Jamaa akasita kujibu,demu mwingine akaropoka ndie huyu(akioneshea mimi)
Jamaa alimanusura wapasuke kwa gadhabu,kama kawaida nikawambia ukweli ya kuwa wasijidanganye kuleta fujo kwangu nitawazika wakiwa wazima na kingine wanapaswa kuwa wapole,wakatii japo kishingo upande.
Nikatumia busara kusema nao wote wanne,uzuri nimejaliwa kipawa cha kushauri mtu,wakaelewa na wakaombana msamaha,nikawaingiza ndani kwangu na mara nyingi huwa nakuwa na dawa za maumivu nikawapa huduma ya kwanza wale mabinti mbele ya bwana zao.
Kisha nikawapa kitanda walale kwa sababu usiku ulikuwa mnene na sikuona haja ya wao kuondoka kwa kuwa hata usafiri wao ulishaondoka na watu wengine.

Ahsubuh nikawamsha nikawataka waondoke maana nina safari,kama utani yule aliebeba vitu vyangu ndani akakaataa kuondoka akisema anatak tuzungumze,mwingine nae akagoma bila sababu huku wakiwakataa wale jamaa mbele yangu kisa wamepigwa.
Jamaa wakamaindi wakasepa nikabaki na msala.
Hadi mchana wa leo wote wapo kwangu,nikaenda safari yangu nikawaacha ndani,jioni nimerudi nimekuta wameshirikiana kufua nguo zangu na kufanya usafi.

Nimewachekiii sijasemesha sasa sijui usiku ndo wanataka iweje na wameumia usoni wote,kila nikiwashawishi watoke hawataki huku kila mmoja akisema flani akitoka na mimi natoka la sivyo hadi utusamehe,

Sasa niko hapa nawaza kuita polisi waniondolee hawa watu maana siwahitaji kabisa,sasa nimemwomba pia mama yake na mmoja wa mabinti hawa aje kwangu,maana namba yake nilikuwa nayo,na nimemwomba kaka wa mwingine nae aje wote wapo njiani

Duniani kuna vituko sana jamani
 
Inatufunza nini hii hadithi yako?

Mara nyingi hata neno fupi lenye maana ni busara kuliko,neno refu lenye kejeli sijui unataka nani akuone,au uonekane Kwa nani chief
 
Mkuu unajua 3some

Anyway tuache masihara hao madada kwanza anza na mmoja aliyechukua vitu vyako mwambie avilete fasta sana la sivyo unampa shambulio la aibu...

Yule atakayebaki mchimbe bonge la mkwala la kumkata pua huku ukiwa serious unanoa kisu...

Mikwala yote ikishindikana hama nyumba (kama umepanga) uwaache waishi wao tu humo gheto kwako maana kama vile wamepapenda
 
Back
Top Bottom