Baba Erick
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 483
- 75
Mkuu hapo kwenye red uko 100% right. Na ndio maana wengi tunashindwa kukupa ushauri wa maana kwa sababu tusilolijua ni sawa na usiku wa giza. Lakini kadri tunavyokubana ndivyozidi kutoa more info. Kama alishakutangaza kama wewe ni marehemu kwa nini bado unatumia namba zake tena kwenye masuala yanayohusu wanao? Mkuu unapoamua kutafuta ushauri ni lazima ukubali kudiclose all the relevant information, otherwise hutapata ushauri unaohitaji. Inaonekena kuna zaidi ya tuyajuayo.
unajua kaka mi siamini kama kweli huyu mama ndiye mwenye watoto wakubwa hivi alafu anajicontradict kama mtoto. Sasa ukawachukua kwa kujitia unaweza kuwa somesha alafu ukaandika namba za baba ili nini? Wewe huna simu? Au bado unajigonga kwake ile hali umeshabwagwa? Nonsense
inawezekana mimi nimelichukulia jambo kirahisi au sijaelewa topic. Huyu mama kilichomuuma na kumkera ni baba kuharibiwa mpango wa shule wa mtoto, inawezekana kabisa walikuwa na ugomvi mingi kabla ya hili lakini hajataka kutushirikisha. Issue iliyopo mezani ni hiyo ya shule, anauliza huyo baba amfanye nini? Watu mmekazana kuuliza ooh ndoa ina miaka mingapi, hapo nyuma alikuwa ana upendo? Umuhimu wake ni nini kwa sasa? Ndoa kama ilikuwa na miezi 3 au miaka miwili itataleta tofauti ya ushauri utakaompa? Kama ndio, kivipi?
Halafu kama hutajali naomba uniwekee link ya threads ya theone na huyo mkewe. Nahisi zilinipita.
Mara nyingine huwa sielewi tunakuwaje sie akina mama.... unajua kabisa ribwana rako harina akiri, mnashindana kuonyeshana ubabe, halafu, bado unatoa mwanya kwa hayo mauza uza kuwafikia watoto.... hapo ndipo sikuelewi. Kwani wewe huwezi kulea mwenyewe ukae kimya hadi awe tayari mwenyewe kuwafuatilia? Sikukuelewa kabisa, kabisa kwa nini uliweka namba zake za simu shuleni. Unajidai unamwaga mboga, yeye anavuta sahani ya ugali anamwaga anakojolea hata kuwapa mbwa haiwezekani. Nani anakuwa amekomeshwa hapo? Please weka watoto mbali na hizo game zenu... I hate it! Nimepita huko na sikutoa hiyo ruhusa.
Wewe ndiye unamakosa mumy kwani umetoa personal contacts bila idhini ya muhusika pia hukumshirikisha muhusika. Pia we umemweleza mwanao ya nini sasa. Inaonyesha una-depression
Kate sweetie pole mydia ulivyoimalizia post yako imenigusa sana.ashilikishwe kwa nini mbona mnamtetea sana huyu baba mkwepa majukumu,wakati anazaa alitegemea zitakuwa zinaandikwa information za nani kuhusu watoto wake, mtoto ni wake ndo maana mama akaandika number za baba na mama wa mtoto, RIP baba ningekuchunia mpaka ukajinyonga
alikwepa majukumu kama huyu,bahati yako sikuwi kukujua
pole dada.Wapendwa, Salaam poleni na majukumu, tatizo langu ni kwamba nimeachana na mume wangu takribani miaka sita sasa, mtoto wangu wa kawnza ndio alimaliza darasa la saba mwaka huu, katika kuhangaika kumtafutia shule ili ajiunge na kidato cha kwanza nilimchukulia fomu Marian Boys ya Bagamoyo.
Kwenye fomu niliandika jina la baba na namba ya simu kwa kutambua kwamba ni baba wa mtoto, alifanya mtihani na akafaulu, tatizo illilonisikitisha sana ni kitendo cha huyu baba mtu pindi alipopigiwa simu ili atambue hilo aliwajibu kwamba, huyo mtoto yupo kwa mama yake mimi hanihusu hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine.
Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.
Asanteni nakaribisha ushauri wenu
Pole sana kwa matatizo dada yangu..
Nyote naona mmechangia kwenye hili tatizo.
kwanza ulitakuwa kumjulisha ex mumeo kuwa umejaza namba zake kwenye form za shule ya mtoto.kwa kufanya hivyo msingefikia hapo.
Pia hata kama mmeachana mlitakiwa kukaa chini na kujipanga namna ya kulea watoto...ina kwa kuendekeza ugomvi wenu mmemuumiza mtoto na kakosa fursa ya kwenda shule...nyie mna akili gani...nadhani utakuwa umemweleza mwanao ukweli ndio maana umesema amejua ana amekosa amani...sio yote twawaeleza watoto..
Fanyeni yote ila watoto wasiwe wahanga na 'utoto' wenu.
Tafakari chukua hatua...
Huwezi kupata ushauri wa tija hadi hapo X wako atakapotoa maelezo yake kuhusu kadhia hiyo na mazingira ya kutengana kwenu na mapatano ya kuishi na kuhudumia watoto baada ya kutengana....inawezekana ulishamkandia kuwa hata huyo mtoto hakuwa wake (biological father) bali alisaidiwa na mwingine..or similar provocationsVin D, Baba alikuwa anaelewa kila kitu, hata mtoto alipofaulu nilimweleza, ila nadhani yeye ndio anaamua kumwumiza mwanae kupitia mimi akijua ananikomoa mimi, suala la mtoto kujua alifatilia mwenyewe pale msimbazi na kuambiwa hivyo baada ya kuona mimi namchenga kumwambia ukweli, tatizo hapo sio utoto tunatofautiana uelewa
Pole lakini wewe ndio uliemnyima amani huyo mtoto, kilichokufanya ujipendekeze kwahuyo baba nini mpaka uweke namba yake ya simu kwenye hiyo fumu? Kwanini usingeweka namba yako'hayo ndio madhara yakufatafata wanaume ambao mlishaachana naoWapendwa, Salaam poleni na majukumu, tatizo langu ni kwamba nimeachana na mume wangu takribani miaka sita sasa, mtoto wangu wa kawnza ndio alimaliza darasa la saba mwaka huu, katika kuhangaika kumtafutia shule ili ajiunge na kidato cha kwanza nilimchukulia fomu Marian Boys ya Bagamoyo.
Kwenye fomu niliandika jina la baba na namba ya simu kwa kutambua kwamba ni baba wa mtoto, alifanya mtihani na akafaulu, tatizo illilonisikitisha sana ni kitendo cha huyu baba mtu pindi alipopigiwa simu ili atambue hilo aliwajibu kwamba, huyo mtoto yupo kwa mama yake mimi hanihusu hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine.
Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.
Asanteni nakaribisha ushauri wenu
pole sana. Tumia hilo kama fundisho, wakati mwingine usiandike namba ya huyo baba mtoto. andika details zako mwenyewe
Mara nyingine huwa sielewi tunakuwaje sie akina mama.... unajua kabisa ribwana rako harina akiri, mnashindana kuonyeshana ubabe, halafu, bado unatoa mwanya kwa hayo mauza uza kuwafikia watoto.... hapo ndipo sikuelewi. Kwani wewe huwezi kulea mwenyewe ukae kimya hadi awe tayari mwenyewe kuwafuatilia? Sikukuelewa kabisa, kabisa kwa nini uliweka namba zake za simu shuleni. Unajidai unamwaga mboga, yeye anavuta sahani ya ugali anamwaga anakojolea hata kuwapa mbwa haiwezekani. Nani anakuwa amekomeshwa hapo? Please weka watoto mbali na hizo game zenu... I hate it! Nimepita huko na sikutoa hiyo ruhusa.
Huwezi kupata ushauri wa tija hadi hapo X wako atakapotoa maelezo yake kuhusu kadhia hiyo na mazingira ya kutengana kwenu na mapatano ya kuishi na kuhudumia watoto baada ya kutengana....inawezekana ulishamkandia kuwa hata huyo mtoto hakuwa wake (biological father) bali alisaidiwa na mwingine..or similar provocations