Wapendwa nimfanyaje huyu X husband

Pole sana ila wote mna makosa.
Kikubwa hakikisha mwanao anapata elimu iliyo bora.
 
Nenda na huyo baba mkapime DNA ya mtoto kumthibitishia kuwa ni wake, huenda anahisi huyo mtoto ulimchakachua. Katika hali ya kawaida hakuna mwanaume anayeweza kufanya ubazazi wa kuharibu maisha ya baadaye ya mwanae. Au hilo janaume lina udhaifu fulani ambao linataka kuuficha kwa kumkomoa mtoto.
 
Funga safari nenda kwa yule father wala hana neno....lol sipati picha ingekuwa mimi, baba gani asiyekuwa mstaarabu shule ile inawindwa na watu kibao embu fikiria watoto 6000 tanzania nzima wamefanya wamechaguliwa 120 tu huwezi kuwa proud na mtoto wako???pole sana maskini ka kwangu pia kamepata
Asante sana Shantel ilam nilipiga simj kwa muhusika wa Marian Boys akanieleza nafasi zimejaa na wao hawana makosa na hawakujua kama hatuishi pamoja je nikienda kwa Father jibu litakuwa tofauti? na je Father yupo pale Kerege au Marian Girls
 
Pole sana mama, na pongezi kwa kulea mwana bila ya msaada wa baba.

Next time hapo kwenye baba andika "deceased" isije kuwa tabu tena. Sasa mtu mzima unasema mwanao nafasi yake ya shule apewe mtu mwingine una tofauti gani na mfu asiye msaada? Tena bora hata mfu wangempigia simu isingepokelewa labda wasingeitoa hiyo nafasi.

Hivi kuna kitu kina miss hapa? Kwa nini huyu baba afanye hivi? Au aliogopa kulipia shule?

Nasoma WSJ la leo kuna story baba yake marehemu Steve Jobs alimtoa mwanawe katika adoption wakati akiwa mdogo sana, wazazi wa adoption wakamsomesha, wakampa support, baadaye Steve Jobs katokea kuwa bilionea mogul, baba yake wa kumzaa akawa anamtafuta, Steve Jobs akamchunia tu.

Sasa sio kwamba nasema mwanao atakuwa Steve Jobs, lakini jitihada huzaa matunda, msomeshe vizuri anaweza kufanikiwa. Utaliona joka la mdimu linajisogeza lenyewe "mwanagu huyu".

Hapo ndipo unakumbushia "ulivyokataa aende shule je?"

Kama story kamilifu inatuonyesha watu wengine wanavyofanya mifarakano kati yao na wapenzi wao iende kuathiri mtoto ambaye hahusiki kabisa.
 
Nenda ongea na huyo jamaa kwanza...
Reaction yake nadhani inatokana na uweli kwamba hukumhusisha na maamuzi yako kabla.
BTW: Hii ni kama unataka ushauri wa jinsi ya au jinsi ya kumalizana na mzazi mwenzio......na sio cha kufanya ili mtoto aende marian?
 
Unajua nimejiuliza kitu, kwenye ile form kuna kuweka namba mbili ya mama na pia baba ina maana hata hawakujaribu yako? na walibandika majibu pale msimbazi jtatu hukwenda?
nilimtuma mdogo wangu alipita nakukuta jina lake, simu zangu mbilit zana moja ya ofisini ,lakini nashangaa sikupata simu hata moja, nimeshangaa sana
 
nilimtuma mdogo wangu alipita nakukuta jina lake, simu zangu mbilit zana moja ya ofisini ,lakini nashangaa sikupata simu hata moja, nimeshangaa sana
pole naona umepata bahati mbaya sana mie alipigiwa simu baba mtu jpili usiku tukaambiwa kesho yake tuende kulipa hatukwenda tulikuwa tunabishana mtoto aende huko au kuna shule ingine alipata aende hiyo tukaminya mpaka alhamis akapiga padri huyo father mzungu na kutusisitiza tena na hapo alipiga kwangu sasa, nikaamua nikalipie ijumaa, sasa nashindwa kuelewa kwako ni bahati mbaya kiasi gani umepata,embu nenda hukohuko shuleni ukaongee
 
Kuna watu wana visasi, miaka sita bado tuu? Au chanzo cha ugomvi wenu jamaa alihisi kuwa ulimchakachua mtoto si wake?
 
We ulichemka umeshaachana naye unatumia namba zake za nini au bado unampenda? Au mliachana kiholela bila kuainisha hatma ya mtoto . Pia mtazamo wangu kuachana na mtu uliyezaa naye nasema hivyo kwa sababu kuzaa na watu tofauti au kufanya mapenzi na watu tofauti ni swala la aibu sana. Mwisho samahani nimeishiwa ushauri
 
Kwangu mimi huyo baba alifanya vibaya.

Sasa suala la wewe umfanye nini, nadhani ni kumuacha tu matatizo ya wazazi kuachana ni mengi tu tena hilo lako dogo. Kuna wazazi wakiachana wanaenda kutorosha watoto shuleni na kuwahamishia shule nyingine.

Mie pia yalinikuta kama hayo kwa namna tofauti. Tulipotengana na wife (miaka 6 kama wewe) watoto walikuwa wanasoma St mathews. Muhula ulipotimu walikuwa kwake hivyo akawapeleka. Wakati wa kuandikisha watakaojulishwa wakati wa ajali akamuandika bwana anayeishi nae (wakati tuko pamoja alijenga, tulipotengana akahamia huko, AKAOA). Nikanyamaza mpaka leo. Watoto wameenda vyuoni, nilipomuuliza mmoja wao amepewa shilingi ngapi na mama, akasema 5,000 (mama ana uwezo kidogo wa kunywa bia na kuchagua kiburudisho cha siku).

Hivyo kimsingi vumilia. Ni-pm tuliwazane.
Sijakuelewa hadithi yako, ila labda mhusika kakuelewa. Pole.
 
sasa kilichokufanya uandike namba ya baba mtoto ambaye ndani ya miaka 6 hajashiriki malez ya mtoto ninini? Pole. Mtaftie mtoto shule nyingine.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
MESTOD mtoto niwake kabisa wako watatu na huyu na first born wake na ujauzito wake niliupata nikiwa shule na ndio ilikuwa mwisho wa kusomana kuolewa nimetooka kwenye ndoa, kutokana na vipigo na mabo mengine ambayo siwezi kuyaeleza ni historia ndefu sana
 
MESTOD mtoto niwake kabisa wako watatu na huyu na first born wake na ujauzito wake niliupata nikiwa shule na ndio ilikuwa mwisho wa kusomana kuolewa nimetooka kwenye ndoa, kutokana na vipigo na mabo mengine ambayo siwezi kuyaeleza ni historia ndefu sana

Pole sana, ila cha muhimu sana ungemshirikisha before na kama angeendelea kugoma ungeandika hata number ya wajomba zake! Au na ada yeye ndo alitoa /anatoa?
 
Kwangu mimi huyo baba alifanya vibaya.

Sasa suala la wewe umfanye nini, nadhani ni kumuacha tu matatizo ya wazazi kuachana ni mengi tu tena hilo lako dogo. Kuna wazazi wakiachana wanaenda kutorosha watoto shuleni na kuwahamishia shule nyingine.

Mie pia yalinikuta kama hayo kwa namna tofauti. Tulipotengana na wife (miaka 6 kama wewe) watoto walikuwa wanasoma St mathews. Muhula ulipotimu walikuwa kwake hivyo akawapeleka. Wakati wa kuandikisha watakaojulishwa wakati wa ajali akamuandika bwana anayeishi nae (wakati tuko pamoja alijenga, tulipotengana akahamia huko, AKAOA). Nikanyamaza mpaka leo. Watoto wameenda vyuoni, nilipomuuliza mmoja wao amepewa shilingi ngapi na mama, akasema 5,000 (mama ana uwezo kidogo wa kunywa bia na kuchagua kiburudisho cha siku).

Hivyo kimsingi vumilia. Ni-pm tuliwazane.
Mkuu tena? Naona kichina tuu hapa!
 
Pole sana. Usipoteze muda wako kushindana na huyu mpumbavu asiyejali maendeleo ya mtoto wenu maana kumfuatafuata itazidi kukupa majonzi wewe na mtoto wenu.

Jitahidi mwenyewe ili umsomeshe mwanao. Wako wanaume kama hawa ambao huwatelekeza kabisa watoto wao na kutojishughulisha na lolote lile katika maendeleo ya watoto wao kisha mtoto akiwa mtu mzima na kuwa na mafanikio katika maisha ndio huwakumbuka watoto na kuanza kujisogeza sogeza ili wapate misaada toka kwa watoto waliowatelekeza.
 
Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.

Pole sana ..Wanaume wengi ambao akili zetu zimebadilishwa kwa kutolewa na kuwekwa makamasi tunafanya kama huyo baba ambaye hana tofuti na chizi..

Ushauri.. Endelea kumtafutia kijana shule... Msamehe huyo chizi kwani hajui atendalo.. Kumfikiria chizi ni kujiumiza moyo bure bila faida!
 
huyo baba ana akili za viatu,sasa hapo anafikiri anamkomoa nani na wewe mama sio kila jambo la kumueleza mtoto tena kwenye umri huo.
inaonyesha hamna mawasiliano mazuri na mwenzako hata kama mmeachana jaribuni kuwa mnawasiliana kwa ishu muhimu kwa maendeleo ya watoto wenu,haina maana kuharibu future za watoto wenu kwa ugomvi/chuki zinazohusu wazazi.

Baba wa mtoto hana kosa wewe ndo una makosa huwez tu kukurupuka kwenda kutoa details zake bila kumjulisha na kuona utayari wake. Mmmh mara nying akina mama mmeharibu maisha ya watoto kwa kuleta mambo yenu/maugomvi kwa watoto...
 
Back
Top Bottom