"Wapenda vita hebu someni hili andiko kwanza"

mukulupapaa

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
2,930
1,731
VITA SIYO ENTERTAINMENT!

Na; Noel C Shao

Team [HASHTAG]#USA[/HASHTAG] na Team [HASHTAG]#Nkorea[/HASHTAG], ndivyo wengi mnavyo jenga fikra zenu. Mkidhani vita ni sawa na mchezo wa soka ambao ukianza utamalizika baada ya dk 90, au 120 au kwa njia ya penati. La! Hasha, vita si hivyo. Kuianza vita ni rahisi mno, mgonga kengele akisha igonga vita ianze hata rejea tena kuigonga kwamba malizeni vita!

Kuna watu wanadiriki kuomba vita hii itoke, wengine wanatamani hata waende kwa mhindi "kubet" kwamba Mimi naweka upatu upande huu. Wenye mitazamo hii siwapingi ila na wasisitiza vita siyo burudani, si sawa na mchezo wa mieleka. Siku Zote wahanga wa vita ni watoto, wanawake, na wazee.

Endepo mtaruhusu mioyo yenu na kushangilia USA iingie vitani, na mwishowe Marekani ikapata mdororo wa uchumi, uwe na uhakika nchi za daraja la Tatu kama Tanzania hatutakuwa salama. Ni sawa na mtoto anaye tegemea wazazi wake kwa chakula, malazi, shule n.k, ikatokea wazazi wake kupata ama maradhi, matatizo au hata kifo, ni hakika mtoto naye atashiriki gharama za matatizo ya wazazi wake. Kumbuka nchi za bara la Afrika Baba yetu ni sawa na Marekani, mama yetu ni sawa na washirika wa Marekani. (Hapa "wajamaa" watanipinga)

Hii vita kama ikitokea madhara yake yatakuwa makubwa ukilinganisha na yale ya vita ya pili ya dunia. Huyu rais wa N, Korea 'Kim Jong Un' ni kiongozi mwenye kiburi na dawa yake ni jeuri ila Marekani anashindwa leta jeuri moja kwa moja kutokana na ideal situation (hali muafaka) ilivyo.

Si kwamba hana uwezo wa kumpiga North Korea, uwezo na uhakika huo upo, Marekani hakuwahi shindwa vita ya moja kwa moja (yaani ya actual field ile ya kumuona adui kavaa kabisa mavazi ya kijeshi) hapa usifafananishe na vita ya Somalia au nchi zenye misimamo mikali. Ila akifanya tathimini ya haraka anaona kuna matatizo hasa ya kiuchumi yanaweza wakabili.

Na wala si anamuogopa China au Russia, kwanza ifahamike Russia hana mabavu sana ya kupambana na USA, nchini Russia wananchi wanaishi maisha ya tabu sana, wengi wanaishi kama watanzania wa manzese, hawana uhakika wa maisha ya kila siku. Maisha ya Russia ni ya kawaida mno, ndio maana hata baadhi ya watanzania wanapenda kusoma Russia, na kuoa wanawake wa huko. Ukimwambia mwanamke wa kirussia unataka kumuoa, Yeye kwake ni Neema. Kwahiyo nchi hii kuingia vitani ni kuruhusu matatizo zaidi Kwa wananchi wake na ikumbukwe kuwa tayari mrussia yupo vitani tena Syria.

Hao China ambao asili yao ni u-communist, hawana background ya vita ingawa wana nguvu ya Sana ya kijeshi, wao kwa sasa wanawaza namna gani atamiliki uchumi wa dunia. Bado nasisitiza hii vita China hawezi shiriki kwa asilimia 100%.

Kwa maana hii Marekani anaweza ingia katika vita na uhakika wa Vita anao. Ila athari za vita ndio bado kikwazo kwake. Anaweza anzisha vita kwa urahis ila mwisho wake ukawa ni mgumu.

Hapa kumbuka silaha zinazo tumika si bastola au bunduki, hii itakuwa vita ya "atomic bombs, au nuclear bomb's" na za sasa hivi ni tofauti na zile za miaka ile ya vita ya pili ya dunia.

Ambapo atomic bomb za wakati ule kwa mfano zile zilizo dondoshwa kule Japan (Nagasaki na Hiroshima) zilikuwa na takribani tani elfu 12 (kg12) ila ya sasa yana tani takribani elfu 60. (Hakuna Lori Tanzania linaweza beba huu mzigo)

Sasa fikra Yale ya Japan ya tani elfu 12 yalipigwa ardhi ikageuka na kuonekana mfano wa uyoga. Fikiria madhara ya vifo zaidi ya laki 3 vilivyo tokea. Fikiria zile radiation ambazo hazikuwa na madhara Kwa wanadamu tu Bali kwa wanyama, samaki, na hata mimea. Mpaka kesho Japan kuna watu hawarefuki kwa sababu ya mabomu yale, kuna watu wanazaliwa na kansa Kwa sababu ya mabomu yaliyo pigwa zaidi ya miaka 80 iliyo pita, Haya ya sasa yatakuwaje?

Hawa watu si wa kuamini hata kidogo, Albert Einstein mmoja wa aliye omba tenda ya kutengeza Yale mabomu baada ya kumaliza kazi alishauri kwa kusema "Those bombs should not be used" ila wakampuuza. Kwa kumwambia Mabomu siyo yako ni ya serikali, "wew umefanya kazi yako, umelipwa ujira wa kazi yako, haya mabomu ni ya serikali"

Marekani wakaenda yatumia Japan wakati huo ujerumani ilisha kubali kushindwa, kwahiyo isingechukua hata wiki kadhaa Japan nae angekubali, ila nani alijali hilo.

Fikiria wale waliodondosha Yale ya Japan mmoja wao alienda kujiua, kwa majuto, naye hakutegemea madhara makubwa namna ile.

Mtengezaji, Albert Einstein mwanasayansi, bingwa wa mathematics duniani, wakati anakaribia kufa moja ya maneno yake ya mwisho alisema, angependa kuja kuzaliwa upya ila siyo kma mwana sayansi Bali Kama "Plumber". Ni baada ya kuona madhara ya kazi ya akili na mikono yake.

[HASHTAG]#Mwisho[/HASHTAG]:
Narudia kusema, Vita siyo entertainment. Na mshindi wa Vita hushangilia kwa majonzi na maombolezo.
 
ki ufupi wanaosubiri vita ya marekan vs korea haiji tokea endeleeni kusubirr ee!?
unadhani hao wanao miliki nuclear hawajui madhara yake!? mnadhan hawaogopi nao!? mtasubiri sana
 
Mwandishi anakurupuka bila kusoma historia, anasema marekani hajawahi kushindwa vita na wavaa uniform kule Vietnam walikuwa hawavai uniform?

Anasemaje China hawana historia ya Vita wakati vita ya Korea ya miaka ya 50 , Korea Kaskazini alikiwa na China na Urusi ili hali Korea ya Kusini alikuwa na nchi 20 pamoja na UN Forces?
 
Hahahhaha..
Mkuu wewe ni Cartoon umekuja hapa kujifanya unatuambia madhara ya vita badala yake unatuambia nguvu za Marekani..

Unasema Marekani Hajawahi Kushindwa Vita Adui akiwa amevaa Sare., Vietnam walivaa kanzu kama Somalia.???

Ukitaka kujua shabiki wa Marekani lazima ataongelea Heroshima,..
Marekani hajawahi kushinda vita kuu ya 2 ya dunia alichofanya ni kupiga bomu japan ambayo ilikuwa haina uwezo wa mabomu hayo, Walioshinda vita ni wale waliopigana muda wote kama Russia..
AJARIBU KURUSHA HILO BOMU HUKO NK HATA KAMA ATASHINDA ILA MADHARA ATAKAYOYAPATA HAJI KUYASAHAU MAISHA..

Alafu unaonesha kabisa unataka tukuunge mkono kwa kuogopa eti Marekani Atapata mdororo wa uchumi ambao na sisi utatukumba,hii ina maanisha tukubali kuwa wanyonge au mwingne aonewe kisa marekani atadhurika kiuchumi...
(Inaonesha wewe ukiwa hauna ela akija mwanaume mwenzio na kukupa ela ili alale na mkeo utakubali)..

Ninavyofahamu Marekani walivyo maharamia zaidi ya Al Qaeda angekuwa na uwezo wa kumpiga Russia au NK kama unavyodai asingehitaji mikwala ya namna hii anayoonesha..
 
Nimeamini propaganda ni mbaya mno, yaani kuna watu wanaiabudu Marekani badala ya MOLA ambaye hataki uonevu/uharibifu anaoufanya Marekani kwa nchi zingine. Ndiyo hizohizo propaganda zinawaaminisha watanzania kuwa bila ccm nchi haitatawalika, huku wengine wakiaminishwa kuwa bila chadema hakuna upinzani Tanzania. Ishi uhalisia.
 
Mkuu mtoa mada naomba ubadili kauli yako kuwa USA hajawahi shindwa conventional warfare. Japan wakati wa vita ya pili walimuelemea USA in the battleground. The japanese army outsmarted the US army in terms of field tactics. Nakumbuka wanajeshi wa marekani (prisoners of war) waliotekwa na japan peke yake walifika 70,000.
 
Mkae mkijua NORTH KOREA, sio mwarabu ambaye anatumia mashambulizi ya kuvizia, wale wanajitegemea ktk kila kitu ktk maswala ya kisayansi, alafu usijidanganye eti US anawanasayansi bora kuliko wote duniani kwani akili na vipaji anatoa mungu, kwa hiyo hujui ana silaha gani na amefikiria nini. Usizisikilize hizi propaganda za US eti ana mitambo ya Kuzuia nyuklia, kama una knowledge kidogo ya radioactive material, nyuklia huwezi kuiziuia, mionzi yake na mabaki yake ni sumu ambayo inaweza ikaua hata vizazi zaidi ya kumi, hii vita kwa fupi mmarekani hawezi ingiza pua yake la sivyo atajuta na makovu yake hayatafutika milele.
 
Russia ni mdogo kiuchumi ukilinganisha na USA lakini kijeshi Russia si mdogo hata kidogo, ni ukweli usiopingika kuwa kipindi cha na baada ya cold war Russia alijikita zaidi katka viwanda vya silaha kuliko uchumi ndyo maana uchumi wa russia n mdogo kuliko USA.
 
VITA SIYO ENTERTAINMENT!

Na; Noel C Shao

Team [HASHTAG]#USA[/HASHTAG] na Team [HASHTAG]#Nkorea[/HASHTAG], ndivyo wengi mnavyo jenga fikra zenu. Mkidhani vita ni sawa na mchezo wa soka ambao ukianza utamalizika baada ya dk 90, au 120 au kwa njia ya penati. La! Hasha, vita si hivyo. Kuianza vita ni rahisi mno, mgonga kengele akisha igonga vita ianze hata rejea tena kuigonga kwamba malizeni vita!

Kuna watu wanadiriki kuomba vita hii itoke, wengine wanatamani hata waende kwa mhindi "kubet" kwamba Mimi naweka upatu upande huu. Wenye mitazamo hii siwapingi ila na wasisitiza vita siyo burudani, si sawa na mchezo wa mieleka. Siku Zote wahanga wa vita ni watoto, wanawake, na wazee.

Endepo mtaruhusu mioyo yenu na kushangilia USA iingie vitani, na mwishowe Marekani ikapata mdororo wa uchumi, uwe na uhakika nchi za daraja la Tatu kama Tanzania hatutakuwa salama. Ni sawa na mtoto anaye tegemea wazazi wake kwa chakula, malazi, shule n.k, ikatokea wazazi wake kupata ama maradhi, matatizo au hata kifo, ni hakika mtoto naye atashiriki gharama za matatizo ya wazazi wake. Kumbuka nchi za bara la Afrika Baba yetu ni sawa na Marekani, mama yetu ni sawa na washirika wa Marekani. (Hapa "wajamaa" watanipinga)

Hii vita kama ikitokea madhara yake yatakuwa makubwa ukilinganisha na yale ya vita ya pili ya dunia. Huyu rais wa N, Korea 'Kim Jong Un' ni kiongozi mwenye kiburi na dawa yake ni jeuri ila Marekani anashindwa leta jeuri moja kwa moja kutokana na ideal situation (hali muafaka) ilivyo.

Si kwamba hana uwezo wa kumpiga North Korea, uwezo na uhakika huo upo, Marekani hakuwahi shindwa vita ya moja kwa moja (yaani ya actual field ile ya kumuona adui kavaa kabisa mavazi ya kijeshi) hapa usifafananishe na vita ya Somalia au nchi zenye misimamo mikali. Ila akifanya tathimini ya haraka anaona kuna matatizo hasa ya kiuchumi yanaweza wakabili.

Na wala si anamuogopa China au Russia, kwanza ifahamike Russia hana mabavu sana ya kupambana na USA, nchini Russia wananchi wanaishi maisha ya tabu sana, wengi wanaishi kama watanzania wa manzese, hawana uhakika wa maisha ya kila siku. Maisha ya Russia ni ya kawaida mno, ndio maana hata baadhi ya watanzania wanapenda kusoma Russia, na kuoa wanawake wa huko. Ukimwambia mwanamke wa kirussia unataka kumuoa, Yeye kwake ni Neema. Kwahiyo nchi hii kuingia vitani ni kuruhusu matatizo zaidi Kwa wananchi wake na ikumbukwe kuwa tayari mrussia yupo vitani tena Syria.

Hao China ambao asili yao ni u-communist, hawana background ya vita ingawa wana nguvu ya Sana ya kijeshi, wao kwa sasa wanawaza namna gani atamiliki uchumi wa dunia. Bado nasisitiza hii vita China hawezi shiriki kwa asilimia 100%.

Kwa maana hii Marekani anaweza ingia katika vita na uhakika wa Vita anao. Ila athari za vita ndio bado kikwazo kwake. Anaweza anzisha vita kwa urahis ila mwisho wake ukawa ni mgumu.

Hapa kumbuka silaha zinazo tumika si bastola au bunduki, hii itakuwa vita ya "atomic bombs, au nuclear bomb's" na za sasa hivi ni tofauti na zile za miaka ile ya vita ya pili ya dunia.

Ambapo atomic bomb za wakati ule kwa mfano zile zilizo dondoshwa kule Japan (Nagasaki na Hiroshima) zilikuwa na takribani tani elfu 12 (kg12) ila ya sasa yana tani takribani elfu 60. (Hakuna Lori Tanzania linaweza beba huu mzigo)

Sasa fikra Yale ya Japan ya tani elfu 12 yalipigwa ardhi ikageuka na kuonekana mfano wa uyoga. Fikiria madhara ya vifo zaidi ya laki 3 vilivyo tokea. Fikiria zile radiation ambazo hazikuwa na madhara Kwa wanadamu tu Bali kwa wanyama, samaki, na hata mimea. Mpaka kesho Japan kuna watu hawarefuki kwa sababu ya mabomu yale, kuna watu wanazaliwa na kansa Kwa sababu ya mabomu yaliyo pigwa zaidi ya miaka 80 iliyo pita, Haya ya sasa yatakuwaje?

Hawa watu si wa kuamini hata kidogo, Albert Einstein mmoja wa aliye omba tenda ya kutengeza Yale mabomu baada ya kumaliza kazi alishauri kwa kusema "Those bombs should not be used" ila wakampuuza. Kwa kumwambia Mabomu siyo yako ni ya serikali, "wew umefanya kazi yako, umelipwa ujira wa kazi yako, haya mabomu ni ya serikali"

Marekani wakaenda yatumia Japan wakati huo ujerumani ilisha kubali kushindwa, kwahiyo isingechukua hata wiki kadhaa Japan nae angekubali, ila nani alijali hilo.

Fikiria wale waliodondosha Yale ya Japan mmoja wao alienda kujiua, kwa majuto, naye hakutegemea madhara makubwa namna ile.

Mtengezaji, Albert Einstein mwanasayansi, bingwa wa mathematics duniani, wakati anakaribia kufa moja ya maneno yake ya mwisho alisema, angependa kuja kuzaliwa upya ila siyo kma mwana sayansi Bali Kama "Plumber". Ni baada ya kuona madhara ya kazi ya akili na mikono yake.

[HASHTAG]#Mwisho[/HASHTAG]:
Narudia kusema, Vita siyo entertainment. Na mshindi wa Vita hushangilia kwa majonzi na maombolezo.
Mleta madaa ulianza vizuri sana ila ukaja kubolonga baada ya kuanza kumtaja RUSSIA.
RUSIA ni miongoni mwa nchi nane ambazo zinatengeneza G8.
Sasa usitake kuwaaminisha watu ya kuwa uchumi wa Russia ni mbaya kiasi hicho kiasi kwamba wanawake wao kuolewa na vijana wa Tz iwe ni big deal.
Kama hujawai ishi na warusi ni wazi kuwa hutoweza kuwaelewa kamwe.
Ukae ukijua pia RUSIA hadaiwi deni la aina yoyote lile tofauti na USA ambaye anamadeni kibao tu.
Kama huijui RUSIA ni bora kunyamaza tu.
Nimependa ulivyoshauri kuhusu vita ila umepotoka kwa propaganda za magharibi za kusema hayo uliyoyasema kuhusu RUSIA.
Jambo la pili pia nadhani hujui historia ya kina kuhusu utengenezaji wa bomu la kwanza la nyuklia (Manhattan project).Robert Einstein ni mzaliwa wa Ujerumani, sehemu ambayo kanuni/fomula ya kutengeneza bomu lile ilitokea,kabla ya wanasayansi wa Ujerumani wenyewe hawajaipeleka fomula ile Uingereza na hatimaye USA(Manhattan) na Kanada.
Bwana Einstein alishiriki pale kama wanasayansi wa Ujerumani, waingereza,warusi,wakanada na wa USA wenyewe walivyo shiriki kulitengeneza bomu hilo.So kumpa sifa bwana Einstein peke yake ni kuwakosea heshima wanasayansi wengine.
Jambo la tatu lazima uwe na uwezo wa kutofautisha kati ya vita na Military operation.
Usa huwezi kusema kuwa ni nchi ambayo imewai kupigana vita yoyote ile ukiacha vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Dunia hii unapoongelea vita basi unataja nchi hizi: MONGOLIA,UFARANSA, UJERUMANI NA URUSI.
Kumtaja USA kwenye upande wa vita ni kupotosha uma ila kwenye Military operation unakuwa upo sawa.
Vita kuu ya pili ya dunia USA hakupigana ile vita ila alifanya finishing kwa watu ambao alikuwa na visasi nao kama JAPAN.
vita ya pili ya dunia ilianza 09/01/1939 na kumalizwa 05/1945.Uo uzushi unaosema ya kuwa ni 02/09/1945 basi ujue tarehe hiyo ilikiwa ni mambo ya makaratasi tu na si watu kumaliza shughuli kwenye uwanja wa kivita.
Ukija kwenye swala la Japan na USA basi ujue kuwa vita ilikuwa ishaisha mana hitla(muhusika mkuu) alikuwa keshasalenda tayari,kilichotokea ni kwamba USA alikuwa na hasira na japan kwani japan ilishawai kushambulia USA.
So USA ikaona ngoja imuadabishe japan kwa makombora hayo,ila vita kwa maana ya uwanjani wajerumani walishakubali kishindwa tayari.
 
Mwandishi anakurupuka bila kusoma historia, anasema marekani hajawahi kushindwa vita na wavaa uniform kule Vietnam walikuwa hawavai uniform?

Anasemaje China hawana historia ya Vita wakati vita ya Korea ya miaka ya 50 , Korea Kaskazini alikiwa na China na Urusi ili hali Korea ya Kusini alikuwa na nchi 20 pamoja na UN Forces?
Ni kweli, ile vita hakushindwa ila aliihairisha.......
 
Ni kweli, ile vita hakushindwa ila aliihairisha.......

Kaka pale Kulikuwa na Vietnam mbili, ya Kaskazini wajamaa na wakusini Mabepari, kabla ya hapo hizo nchi zilikuwa moja sawa na Korea na Ujerumani

Vietnam Kaskazini wakaivamia Vietnam ya kusini wakiwa na lengo la kuiunganisha nchi yao iwe moja kama awali, Wamarekani wakaingia vitani kupinga hilo, mwisho wa siku walishindwa na sasa Viet Nam ni moja ya Kijamaa sasa utasemaje hawakushindwa vita?
 
Mtoa mada naona umeamua kuelezea mahaba yako kwa Marekani,

Ila hapo kusema Urusi wana maisha magumu kama Manzese, hebu fanya utafiti kidogo. Warusi kwa raia moja moja wana maisha mazuri kuliko US ambako kuna watu ambao wanakula kwa stiker huko Marekani kwenu.
Wanawake wa Kirusi sio wanapenda kuolewa na foreigners kwa kuwa kwao maisha ni magumu, ni kwamba Wanawapenda zaidi Mablack kuliko warusi wenzao.

Mimi nimesoma kule, nimekaa kule muda kidogo na hizo propaganda mnazolishwa na Marekani ni uongo mtupu.
Kuna siku nilienda cruise trip as mtalii na kulikuwa na watalii wengi toka Marekani na Ulaya tulikuwa kwenye meli moja inaitwa Ms Konstantin Korotkov tukitoka Moscow hadi St. Petersburg kwa hiyo cruise boat. Wamarekani walishangaa sana kwamba jinsi walivyokuwa wakiaminishwa jinsi Russia ilivyo ni tofauti na walivyoiona. Na walishangaa zaidi St. Petersburg maana waliona kama wako kwenye miji yao mikubwa.

Kwa hiyo kaka acha kutumika na wamarekani.
 
Mara nyingi vita huzaa vita.
Angalia Iraq,Somalia baada ya Siad Bare,Afghanistan,Libya,etc.
Sasa vita kubwa kama hiyo ya U.S na Korea itatuachia crisis kubwa kiasi gani kule Mashariki ya mbali?
Tunahitaji muda wa kulea vizazi vyetu kiuchumi,kiutamaduni na kisiasa kwa ajili ya kujenga dunia ya kesho,how can you do that in a war zone?
Dunia haitaweza kuhimili crisis nyingi mahali mahali,we will all go down together.
Ni yule mwenye ufahamu mdogo juu ya uchumi na geopolitical effects za vita ndio atashangilia bila kujua Tanzania na dunia vitaathirika vipi wakati na baada ya vita ya Mashariki ya mbali.
 
Back
Top Bottom