Wapenda magari jiandaeni kupaa..!!!

Wapenda magari jiandaeni kupaa..!!!

IrDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2010
Posts
745
Reaction score
361
Haya wadau jiandae kupaa sasa na muondokane na foleni,sikuhizi barabara hazina maana na matrafiki watakufa njaa
car+2.jpg

Tukae mkao wa kula, wanasayansi wanazidi kufanya mambo yao, sasa wanatuletea magari yanayopaa a.k.a Flying Cars. Usipate tabu kuunga foleni pale ubungo, wewe washa Engine yako ya ndege kisha ruka mwezini kama njiwa, au siyo!!
Magari hayo bado yanakaguliwa, endapo kila kitu kitakwenda sawa, yataruhusiwa kwenda angani mwaka 2012
 
bei yake wataimudu mafisadi tu kwa hapa tanzania
 
Wapeleke matangazo yao pale magogoni kuna mteja.
 
sasa yakija hapa nchini....TCAA itahusika.....?
 
Hakyanani hizo ajali huko angani tutapopoana si mchezo. Kama barabarini tu ajali ni za kumwaga, huko angani ambako hakuna hata barabara, taa za kuongozea magari, wala askari wa usalama barabarani, itakuwaje kweli?!
 
Hii gari mbona ina Indicator Lamps Nyingi sana? au ndo Kuepusha ajali?
 
Back
Top Bottom