Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,613
- 12,896
Ndicho wanachokifanya wazungu kwa viongozi wa Africa.
Wanaupamba utamaduni wa kimagharibi kisha huwaonjesha viongozi wa Africa ambayo hutokwa udenda kwa walichoonjeshwa.Wazungu huwaonjesha viongozi wa Afrika utamaduni wa magharibi hasa material possession ambao wengi hawawezi kumudu.Wanabaki kutamani majumba mazuri kwenye visiwa vya pacific, magari ya kifahari, plots kwenye majiji makubwa ya ulimwengu wa kwanza, akaunti zilizonona kwenye mabank ya magharibi n.k.
Hapa ndipo wazungu wanapotimiza tamaa ya viongozi wa Africa na kutumia kama bargaining tool ya kupata wanachotaka. Mzungu akishamlaghai kiongozi, yeye anapewa mwanya wa kufanya analonuia kwa njia za kimagendo lakini zilizopakwa rangi ya 'uhalali' zenye kumnufaisha yeye mwenyewe.
Utashuhudia nchi inauza rasilimali zake kwa bei ya nyanya sokoni ufikapo msimu wa nyanya.Ndipo tunaposhuhudia nchi nyingi za Africa zikifanya manunuzi mabovu, aidha kwa kuuziwa bidhaa zilizopo chini ya kiwango ama kwa bei maradufu ya bei stahili.
Matokeo yake ni umasikini kwa nchi husika ambao huwaumiza raia wake wasiokuwa na uhalisia mwingine wa maisha tofauti na umasikini.Ndipo tunaposhuhudia na kushangaa ni kwa namna gani nchi zenye utajiri asilia kama za kiafrika bado zinaishi kwenye umasikini? matatizo kama umasikini, magonjwa, miundombinu mibovu, huduma mbaya za kijamii n.k hayakustahili kuendelea kuwepo Afrika.
Wakati huohuo mzungu anaendelea kuwa mtu mnafiki sana.Wanachukua sehemu kidogo mno ya wanachotuibia na kutupatia kama misaada.Wanavaa makoti ya usamaria mwema kwa nia kuu mbili, kwanza kufunika historia ya uchafu wote walioutenda Africa kama vile ukoloni, ubakaji, wizi wa rasilimali, mateso kwa mababu zetu, ubakaji pamoja na biashara ya utumwa.Kazi ya pili ya hili koti la usamaria mwema linalofunika hawa chui, ni kuwapumbaza waafrika ili waamini kuwa wazungu ni watu wema na wenye kututakia mema. Toka lini mzungu akamtakia mwafrika mema?
Mzungu yupo tayari kuua, kuvamia nchi za watu, kuanzisha vita na kufanya kila aina ya uovu ilimradi apate na kulinda maslai yake. Hatuhitaji nabii wa kutuambia kwamba vita zote kuu duniani zilianzishwa na mzungu.
Kwa upande wa Africa, nafasi ya uongozi inaonekana kama njia ya kukwaa utajiri na kuishi maisha ya daraja la ulimwengu wa kwanza. Mtazamo huu unawavutia wanasiasa watamani kuongoza si kwa lengo la kuwaendeleza raia bali kwa maslai yao wenyewe.Siku hizi vijana wengi wanakimbilia kwenye siasa maana wanajua ndio njia rahisi ya kutokea.Wanajua siasa inamuweka mtu kwenye nafasi nzuri ya kuwa kiongozi.Ikitokea amekuwa kiongozi na siyo mzalendo[kama walivyo wengi] huhongeka kirahisi na kuyatoa kafara mataifa yao.
Tuungane na Rais Magufuli kuzuia ziara za nje maana huko ndiko dili zote haramu hafanyika.Kiongozi anaweza kusafiri nje na kusema ni ziara ya kikazi ama anakwenda mapumzikoni kumbe anakwenda huoneshwa dau analoweza kuhongwa, kupanga dili lenyewe, kuhongwa, na kuhakikishiwa usalama wa hongo aliyopewa.
Kwa Afrika njia ya kuondokana na huu umasikini ni uzalendo, ueledi, uchapakazi, na ushirikiano usiojali tofauti zetu.