Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Hao wamarekani ambao wamesitisha utoaji wa fedha za MCC, wakazi wake wengi wanafanya kazi zaidi ya moja kwa siku. Mmarekani analala saa sita usiku na saa kumi na moja na nusu anakuwa tayari bafuni akioga kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini.
Tazama matukio mengi kwenye taarifa za habari yanavyoonyesha jinsi wazungu wanavyopishana asubuhi au mchana wakiwa njiani kwenda kazini au kurudi majumbani, huwa hawana hata muda wa kukodoleana macho, kila mtu anatembea kwa mwendo wa haraka, akili yake ipo kazini.
Sisi walengwa wa fedha za MCC na nyinginezo zitolewazo na wazungu, kwa nguvu kubwa tunatetea uchezaji wa pool saa mbili asubuhi!. Tunahalalisha umasikini kwa kutumia hoja nyingi nyepesi. Tunahalalisha maisha ya mazoea kwa kutetea uvivu haswa miongoni mwa vijana wanaoishi kwenye majiji makubwa.
Halafu Mungu alivyokuwa wa ajabu, ndani ya mwaka mzima jua linawaka na mvua zetu nyingi ni za wastani. Matunda ya aina nyingi tu yanapatikana nchini mwetu. Madini, mito na maziwa, ni vitu tulivyonavyo. Kuna nchi nyingi duniani haswa za ulaya na amerika, jua huwa halionekani ndani ya miezi yote kumi na mbili ya mwaka mmoja, lakini nchi hizo ambazo hazijabarikiwa maliasili ndizo zinazotulisha sisi!.
Walio busy kwa kufanya kazi zaidi ya moja kwa siku, wanaolala masaa machache kwa siku, ndio ambao wanatenga fedha kwa ajili ya misaada ambayo kwa kweli inaambatana na dharau pamoja na kebehi, na ukitazama mambo kwa undani wazungu hawa wanatudharau kwa sababu wanaujua utajiri wetu na uvivu wetu pia.
Ufike wakati ambapo tuanze kujihurumia, tuanze kujinyooshea vidole sisi wenyewe kabla hatujatafuta mtu wa kumtwisha mzigo wa lawama kama chanzo cha umasikini wetu.