Nimeisikiliza kwa umakini mkubwa sana hotuba ya Kikwete kuhusu suala la wahamiaji haramu, kwa hakika Kikwete alisema vizuri kabisa, tena hakumfukuza mtu hata mmoja. Inashangaza sana kwamba wanyarwanda wameondoka nchini kwa lawama kibao na malalamiko ya kwamba walihamia tangu mwaka 1959, ilihali Kikwete hakuwaambia waondoke.
Inashangaza sana namna ambavyo hawa wenzetu ni wazuri katika kukuza migogoro ambayo haipo. Sikiliza hii video kuanzia dk 22.
Dah, yaani kwakweli kama ni vyombo vya habari basi vilivuruga mambo kwa hakika. Maana hoja ya Kikwete ipo tofauti kabisa na namna jambo lenyewe lilivyokaliwa kidedea.Magazeti ndugu yangu! Yaliaandika sana kuhusu wiki 2, yaliandika sana yakisema ndoa na wahamiaji haramu zivunjwe, yalipotosha kauli ya rais, TV zikachambua magazeti, watu wakaogopa sana, wakakimbia! Wanakijiji na watendaji wanaotaka vya bure pia wakawatisha wakasema: "Rais amesema muondoke, mnataka jeshi liwakute hapa?" Vyombo vya habari jamani
Wanyarwanda wachokozi wanatafuta kitu.. Kwani dunia nzima ni wao tu? Mkulu alisema wahamiaji haramu maana raia wa nchi yoyote duniani wanaoishi bila vibali..sasa wao wakatimua eti tumefukuzwa Wanyarwanda mbona Waburundi hawajalalamika au Waganda au Wakongo ni wao tu. Hawa wasitunyime usingizi wakitaka kurudi kwao ruksa nanyi si mna kwenu tuachieni Tz. yetu.
Namtetea Rais wa nchi yangu waende wasiende lakini wawe na adabu sio kukurupuka na matusi ya nguoni kwa Rais wetu.kwenye picha we dada unaonekana una unyafuzi, wakiondoka utaneemeka unenepe? tumia kauli nzuri sio kusiliba watu wengine, sawa dada.
Namtetea Rais wa nchi yangu waende wasiende lakini wawe na adabu sio kukurupuka na matusi ya nguoni kwa Rais wetu.
Nimeisikiliza kwa umakini mkubwa sana hotuba ya Kikwete kuhusu suala la wahamiaji haramu, kwa hakika Kikwete alisema vizuri kabisa, tena hakumfukuza mtu hata mmoja. Inashangaza sana kwamba wanyarwanda wameondoka nchini kwa lawama kibao na malalamiko ya kwamba walihamia tangu mwaka 1959, ilihali Kikwete hakuwaambia waondoke.
Inashangaza sana namna ambavyo hawa wenzetu ni wazuri katika kukuza migogoro ambayo haipo. Sikiliza hii video kuanzia dk 22.
Ni bahati mbaya kwamba hajatuambia kama Mkapa na Mwinyi waliwapa wangapi? Na kama Mwinyi na Mkapa hawakutoa uraia kwa yeyote, hiyo itakuwa inamaanisha nini? Na inamuelezeaje yeye ukilinganisha na hao wenzake?Hivi ni kwanini anapenda kujilinganisha sana na nyerere, eti "Mzee nyerere aliwapoa uraia 30,000 mimi nimewapa 100,000".
Je ni sifa kuwapa uraia wageni wengi hivyo kutoka nchi nyingine?. du
Ni bahati mbaya kwamba hajatuambia kama Mkapa na Mwinyi waliwapa wangapi? Na kama Mwinyi na Mkapa hawakutoa uraia kwa yeyote, hiyo itakuwa inamaanisha nini? Na inamuelezeaje yeye ukilinganisha na hao wenzake?
Walioondoka wote wanajijua kuwa ni HARAMU!,vinginevyo kulikuwa hakuna haja ya kujistukia.
Kipi kibaya alichokisema?? Kuwaambia wahamiaji haramu waondoke kwenye nchi yake ni kosa? Ulitaka nani aseme..Rais ni sauti ya Watanzania ambao ni mimi na wewe (endapo ni Mtanzania) kundi hili linajumuisha wananchi wa dini zote vyama vyote makabila yote halali ya Tanzania sasa kipi kisichoeleweka. Mwenye kupenda kuishi Tanzania basi afuate taratibu ni hilo tu mkuu aliagiza..Wanyarwanda wameondoka wenyewe hawakufukuzwa kama ni wahamiaji halali kama ni wahamiaji haramu warudi kwao wakafuate taratibu kipi kisichoeleweka hapo?Unamtetea wakati anafanya maamzi alikushirikisha? Kuna wa kumtetea, msemaji wake, waziri, mkuu wa mkoa, na anawalipa. Hapa ni ku-discuss ussues na points, sio kuleta fallacies hapa... sawa