Wangwe(RIP),Shilembi (RIP) mawe ya CDM yaliyopotea. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wangwe(RIP),Shilembi (RIP) mawe ya CDM yaliyopotea.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Apr 28, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hakika Chama kimepoteza watu muhimu ambao waliweza kuleta changamoto ndani na nje ya Chama.Binafsi nikiwa si MwanaCDM lakini nilivutiwa sana na viongozi hawa.Hawa ilikuwa ni tunu ya Taifa kwa maana walikuwa tayari kutetea misimamo yao pasipo kuteteleka.Wengi tumemshuhudia Chacha Wangwe akiwa bungeni kamwe hakuteteleka.Wangwe alisimamishwa Umakamu Mwenyekiti wa Chama lakini bado alikuwa akipambana katika siku za mwisho za uhai wake kutetea kwa nini asisimamishwe mbali na hapo alikuwa na hoja binafsi aliyokuwa akihitaji kuiwasilisha bungeni juu ya jimbo lake.RIP Wangwe.

  Shilembi ni mfano wa Wangwe,kipenzi cha watu ndani na nje ya Chama alikuwa mnyenyekevu na mwenye kutetea msimamo wake.Wote tumeambiwa ni jinsi gani aliweza kusimama kidete kumtetea Wangwe asisimamishwe wala kuondolewa katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa Chama.Msimamo wa Shilembi japo ulijenga uadui kwa Mbowe lakini aliamini msimamo wake ulikuwa sahihi.

  Kiza kimeeingia ghafla,ni nani mwenye uwezo wa kurithi ya watu hawa ndani ya Chadema sasa?.Nimeambiwa Shibuda karithi mikoba ya mpiganaji Shilembi(Mwenyekiti wa Mkoa),bila shaka anaweza kusukuma gurudumu la msimamo ndani ya chama na nje.Kumkabili Mbowe si suala dogo,yahitaji busara na waliokuwa mawe bila shaka maadui zake wakubwa wote wamepotea.
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180

  mbowe is not our enemy! Tuwe makini tusipoteze nguvu zetu na kupambana na walio wetu!

  Unaweza kusema nina uelewa finyu, lakini hata mimi nimeishafanya siasa.....tulipotoka chama kichanga na kilicho determined kama chadema kisingeweza kukua kwa kuendeshwa kwa hisia za wengi wape.....

  Labda tujiulize ni kwa nini nccr, tlp, appt dovutwa nk wamekuwepo kwenye game muda mrefu lakini bado wanachechemea?

  Mabadiliko ni lazima...muda utapofika....kukua kwa haraka ni detrimental....

  Mnadhani kwanini nyerere alibaki hazina kwa ccm hata baada ya kung'atuka kote kote??

  Tunataka pia ifahamike kuwa chadema ina rasilimali wanachama NA VIONGOZI kubwa sana...hawa wanaoonekana kwenye majukwaa, na wasiopanda majukwaani...naomba hili la kufariki shelembi na wangwe lisikutie hofu.....
   
Loading...