Wangojani kumuacha?

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284
WANGOJANI KUMUACHA?
1)
Usichelewe kuacha, mpenzi anosumbua,
Kiumbe mwenye makucha, midomo aibinua,
Kiama usiku kucha, moyoni una ugua,
Mpenzi ano sumbua, usisite kumuacha.
2)
Akupe vilivyo chacha, vizima anapojua,
Nyama akupe mchicha, na sima iloungua,
Uwe mithili ya vocha, atupa akikwangua,
Mpenzi ano sumbua, usisite kumuacha.
3)
Ya kwake anayaficha, yako ataka yajua,
Husema alochekecha, kwa hila huyabagua,
Njia panda akuacha, ushindwe piga hatua
Mpenzi ano sumbua, usisite kumuacha.
4)
Akughuri kwa chakacha, kumbe ataka kwapua,
Ama roho kuchikicha, kwa dhamira ya kuua,
Kwa lumbesa na pakacha, ulochuma tachukua,
Mpenzi ano sumbua, usisite kumuacha.
5)
Mapenzi sio kuchocha, kupika na kupakua,
Fahamu hayana kocha, hayahitaji bukua,
Niliyonena chekecha, yalo maana chukua,
Mpenzi ano sumbua, usisite kumuacha.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0622845394 Morogoro.
 

Attachments

  • 12991100_1285854588096043_1360347356183494780_n.jpg
    12991100_1285854588096043_1360347356183494780_n.jpg
    12.6 KB · Views: 37

Similar Discussions

Back
Top Bottom