Wangalizi wa Uchaguzi Kutoka Umoja wa Ulaya (EU)

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) wamekosoa namna ambavyo uchaguzi mkuu wa Uganda ulievyoendeshwa na kusema mabadiliko makubwa yanahitajika.

Wakizungumza na wanahabari nchini humo, viongozi wa ujumbe kutoka Muungano wa Ulaya wamesema kulitokea kasoro nyingi kuhusiana na shughuli nzima ya uchaguzi.


Dkt Besigye alivyokamatwa majuzi.

Mwangalizi mkuu wa Umoja wa Ulaya, Eduard Kukan amewaambia wanahabari kwamba ni dhahiri Tume ya Uchaguzi ya Uganda haikujifunza kutokana na mapendekezo yaliyotolewa umoja hu baada ya uchaguzi mkuu wa 2011.

Aidha, amesema haikuwa haki kufunga uandikishwaji wa wapiga kura Mei mwaka jana, huku akisema hatua hiyo imewanyima haki ya kupiga kura raia waliotimiza umri wa miaka 18 baada ya tarehe hiyo.


“Tume haina uwazi na wadau hawana imani nayo. Tume haina uwazi katika kufanya maamuzi na katika kuwafahamisha wapiga kura kwa wakati na kwa ufasaha,” alisema Kukan.

Bw Kukan akaendelea kueleza kuwa, kucheleweshwa kwa karatasi na vifaa vya kupigia kura pamoja na kuchelewa kuanza kwa upigaji kura siku ya uchaguzi kuliathiri imani ya watu katika zoezi hilo.


Ameshutumu pia kukamatwa na kuzuiliwa kwa kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye ambaye pia ni mgombea urais kwenye uchaguzi huo, pamoja na kufungwa kwa mitandao ya kijamii. Dkt Besigye alikamatwa na polisi mara tatu ndaniya wiki hii.

Mwangalizi Mkuu wa Bunge la Ulaya, Jo Leinen kwa upande wake amesema wagombea wote hawakupewa nafasi sawa katika vyombo vya habari na wanasiasa pamoja na raia waliounga mkono upinzani walipatwa na misukosuko kutoka kwenye vyombo vya usalama nchini humo.

Amesema pia kwamba fedha za serikali na chama lazima kutenganishwa. “Kuna mengi sana ambayo yanafaa kurekebishwa,” alisema Leinen.

Waangalizi wa Jumuiya ya Madola, wanaoongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, pia wameeleza kutoridhishwa kwao na baadhi ya mambo yaliyotokea wakati wa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom