nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
SIASA
Na Mwandishi Wetu
Posted Jumatatu,Decemba24 2012 saa 11:24 AM
KWA UFUPI
Aprili 18 na 20 mwaka huu madiwani hao walitangaza kujivua uanachama wa CCM na kuhamia Chadema kwa kuwatuhumu baadhi ya madiwani wenzao wa CCM kuwa ni wasaliti wakubwa katika kuwatetea wapigakura wao.
WALIOKUWA madiwani wa Kata za Lugata na Nyampulukano kupitia tiketi ya CCM kabla ya kujiunga na Chadema katika Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza wamedai kuwa wataendelea kuwa madiwani kwa kuhudhuria vikao vyote vya baraza la halmashauri hiyo.
Madiwani hao, Adrian Tizeba wa Kata ya Lugata na Hamis Tabasamu, aliyekuwa diwani wa Kata ya Nyampulukano, wamedai kuwa hatua hiyo inalenga katika kumshinikiza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza kata hizo kuwa wazi ili kutoa nafasi kwa tume ya uchaguzi kutangaza uchaguzi mdogo.

Hatua iliwaondolea sifa ya kuwa madiwani kwani walishakihama chama kilichowaingiza madarakani.
Akizungumza katika mkutano wa Chadema uliofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Sengerema, Tizeba alisema na sheria kutamka wazi kuwa diwani yeyote anapoachia nafasi hiyo na kata husika kuwa wazi, tume ya uchaguzi itatangaza uchaguzi mdogo ndani ya siku 90.
Alisema kanuni ya kudumu ya 69 ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema pia inaitaja sababu ya kukihama chama kilichomdhamini diwani kama sababu mojawapo inayomwondolea sifa ya kuendelea kuwa diwani.
"Ikishatokea hivyo, mwenyekiti wa halmashauri anamjulisha Waziri wa Tamisemi ambaye kwa kuzingatia sheria Na.7 ya 1982 kifungu cha 42(1) anatangaza kuwa nafasi ya udiwani ya kata fulani iko wazi, tunamshangaa waziri mkuu kwa nini ameshindwa kutangaza kuwa kata hizo ziko wazi,''alisema Tizeba