Wanetu hawajui gololi kila kitu ni ready made!

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,561
19,056
Ulikua ni mchezo maridhawa wenye taratibu na kanuni zilizosukwa vizuri sana. Kuna kiduara kinachorwa zikawekwa gololi zikiitwa kwenye mchezo "mali", ambazo wachezaji wote wanachangia kwa idadi sawa kinaitwa KIDU. Mbele ya kidu kama mita nne au tano unachorwa msatati mrefu ambapo wachezaji watarusha gololi zenye ukubwa tofauti na zile walizowekwa kwenye kidu ili kuamua nani atakua wakwanza kucheza, gololi hizo tofauti zinaitwa BENTO.

Wakati wa kurusha bento kwenye ule mstari mnakua wote mmesimama usawa wa kidu na yule ambae bento lake litaukaribia zaidi mstari bila kuuvuka ndio anaanza kucheza. Bento likivuka mstari unaambiwa umetoka PAKE na kama kutakua hakuna aliyetoka pake basi wewe utakua wa mwisho kucheza. Wakati wa kucheza unarusha bento kuelekea kwenye kidu ili ule "mali" kwa kuzipiga gololi zitoke nje ya duara la kidu. Ukifanikiwa kuzitoa basi unaendelea wewe kucheza hadi umalize mali zote au ukose ndio aje mwingine. Bento likikwama kwenye kidu unaambiwa ume SITI na unarudisha kwenye kidu mali zote ulizokula. Pia unaweza usirushe bento moja kwa moja kwenye kidu kutokana na umbali hivo ukalirusha tu karibu na kidu halafu akasubiri mwingine acheze ili akikosa wewe uwe karibu na mali, hiyo inaitwa ume CHUNGI. Lakini anaekufatia kucheza atakua pamoja na kukusudia kupiga kwenye kidu pia atakua analenga bento lako na akikugonga anachukua mali zote ulizokula. Hii inaitwa KUTINYA au KUTINYISHWA

Pia kabda hujacheza hakikisha una nuia kwanza maneno yafutayo , "KIDU NA MALI NA BENTO VYOTEVYOTE" halafu unaendelea kucheza vinginevyo una tinya mali zote kama huja nuia. Kama umekula mali za kutosha na hutaki tena kuendelea na mchezo unasema SALATI na wenzako ama wanaendelea au wanagawana mali zilizobakia

Nimekaa kwenye mapumziko haya ya mwisho wa mwaka nikaona watoto wanachezea toys zao ambazo kila kitu kiko inbuilt hakuna skill yoyote wanayotumia zaidi ya kujua ku oparate toys, nikajikuta najiwazia tu tulipotoka. Lakini wakati ukuta, kila zama na kitabu chake na huu ni wakati wao
 
Hahahaaa, hawana cha kutinyishana siku hizi
Ni kweli saiv mtoto anajifungia ndani pekee anawatch movies au anaplay video game pamoja na kunyolewa viduku huku wazazi wao wakifurahia, wakati ule sie tumenyolewa na nyembe utakuta kijiji kizima mnyoaji mmoja au wawili kama mzee wako hana pesa anatake risk ya kuwa mnyoaji..
 
Kiduku_dance.jpg
 
Siku zetu utotoni hatukuwa tunaitwa baba au mum. Tulikuwa tunajiona kina Chuck Norris na Bolo Young tunauwana kwa bunduki za mbao utadhani ni kweli. Siku nzima ilikuwa na masaa matatu tu enzi hizo hata hatujui jua lilitua saa ngapi. Likizoni ukiamka asubuhi hata hujui uende wapi, misheni kibao.
 
Duh.. Tulicheza huo mchezo ila tulikua tunaita " MSOKO"

Kati ya misamiati tuliyokua tunatumia ni

Kupuna/Kupunwa= Kula/kuliwa

Last

Killer

Fag zako

Dead

No kwa kwa no kwinhio=hapo ni kwaajili ya yule anaekua amekula sana sasa kwa kujihami asije akapuluswa zote alizokula anaamua kuimba kwakwakwinhio ni kama anajiuzuru.

Mnyukwa

Jaa

Banju

Over...

Dungu

Kingwasu= Hili ni jina analopewa nguli/mbobezi.

Nimekumbuka hayo... Ila process za mchezo ni kama hizo ulizosema.
 
Back
Top Bottom