KABIDI BODO
Senior Member
- Jan 19, 2017
- 184
- 252
Nimekuwa nikitafakari juu ya uamuzi wa serikali kufuta fao la kujitoa na kuongeza makato bodi ya mikopo kwa wanufaika kinyume na mikataba ya wanufaika bila majibu stahiki.. Mwisho nimegundua kuwa wanazuoni wengi wa nchi hii ni waoga wakuichagiza serikali pindi inapofanya maamuzi yakuumiza.
Hata wanasheria wamekubali kirahisi tu kuwa wahanga wa mambo haya, unabaki unatafakari kuwa kama ukoloni ungerudi leo hii sidhani kama tungeweza kujikomboa, maana vijana wa leo wamekuwa sio jasiri kama walivokuwa mashujaa wetu walotutoa katika ukoloni..
Mpaka muda huu bado sina imani na sitaweza kuwa na imani hata siku moja na chama cha wafanyakazi ndani ya nchi hii, naona kipo kisiasa zaidi na kimeshindwa kujipambambanua kama mtetezi wa kweli wa wafanyakazi..
Hili limeonekana hata kwenye swala la vyeti feki, kuna waliokuwa fake kweli na kuna walioonewa, lkn sijaona chama cha wafanyakazi kikisimama kuwatetea walioonewa..
Ni kweli na niwajibu wa kila mnufaika wa mkopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu ni sharti alipe maana dawa ya deni ni kulipa, lkn ktk kipindi hiki kwa nini umtoe mtu aliyekua kishaanza kulipa kutoka 8% hadi 15% nje ya mkataba aliosaini mnufaika wakati anajaza fomu za kuomba mkopo na hata alipokubaliwa.. Cha kusikitisha zaidi TUCTA walituhadaa wanaenda mahakamani kupinga lakini sioni hili likitendeka maana wanakula kwa urefu wa kamba yao..
Wanasheria nao ni wahanga wa haya mambo lakini wapo kimya na wamekubali tu haki ipindishwe kotekote..
Katika kipindi hiki ambapo makampuni mengi yanapunguza wafanyakazi, watu wanaenda mtaani na hawawezi kuchukua mafao yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ili japo waweze kufanya miradi mingine katika kujikwamua kimaisha, lakini hakuna ambae anathubutu kulihoji wala kulichokoza popote pale..
kama chama cha wafanyakazi kingekuwa mtetezi wa kweli wa wafanyakazi, haya yasingefanyika na kumuacha mfanyakazi katika hali ngum.
Kiukweli wanazuoni wengi wa Tanzania ni waoga na laiti mkoloni angetawala zama hizi ingekua ngumu sana kumng'oa...