Wanazuoni na mustakabali wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanazuoni na mustakabali wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalunguine, Apr 30, 2011.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Salaam!
  Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa jumuia za wanachuo na hasa Chuo Kikuu Dar. Makongamano, mihadhara, vigoda vya kitaaluma na kadhalika kujadili na kuchambua mambo mbalimbali ya kisiasa na kijamii vimekuwa vikiashiria dalili za kurudi kwa mwamko wa miaka ya 70 na 80 ambyo ilishuhudia ujasiri mkubwa wa wasomi wa kukosoa mienendo iliyokuwa ya kiunafiki ya viongozi na watawala wa nyakati zile akiwemo Rais wa kwanza wa nchi hii, Julius Nyerere. Lakini nyakati zile, hoja kubwa ya wasomi iliyokuwa ikisemewa kwa nguvu ilikuwa ni 'unafiki' wa wanasiasa waliokuwa wakijiita wajamaa kumbe walafi tu! Miaka ya baadaye moto ule wa kuyapigia kelele mambo kama haya ukafifia haswa nchi ilpoingia katika mfumo wa 'huria soko'! Heshima ya Chuo cha Dar iliishuka sana pale ambapo wahadhiri wengine walipojiingiza kwenye kutafuta masilahi na kugeuza taaluma kuwa biasahara. Ni sawa maana yoyote mtu ana haki ya kuuza kile anachokijua kuliko wengine. Lakini cha kusikitisha zaidi ni pale ambapo wahadhiri walipogeuza usomi wao kuwa mtaji wa kisiasa wa kujitafutia maslahi binafsi kwa kisingizio cha kuwatumikia wanananchi kupitia nafasi za kisiasa. Ndipo tukawapata wabunge wengi kutoka vyuoni na waliogombea uongozi wa chama. Is it the "If you can't beat them join them" factor that came into effect! Hata hivyo wengi bado tulikuwa tukizitegemea sana jumuia za wanavyuo kuwa ndio zingeongoza mapambano dhidi ya dhuluma, unafiki na wizi wa mali ya umma kwa njia za ufisadi kama huu tunaoshuhudia leo. Aidha utetezi wa wanyonge katika kupata haki zao ungeonekana kupitia wasomi hawa baada ya Bunge kugeuka msaliti mkubwa kwa wananchi waliowachagua! Mbaya zaidi baada ya Vyama vya Wafanyakazi kunyamazishwa kwa vitisho vya Kikwete mwaka jana nao wamebaki wakijiuliza watetewe na nani tena. Ni wakati muafaka kwa wanavyuo na hasa wahadhiri kuchukua tena hatamu za kuongoza kuelekea kwenye mabadiliko tunayoyatamani kwa kutoa ushauri muafaka na kwa ujasiri kwa jamii pamoja na makongamano mazuri wanayoyaandaa ambayo wakati mwingine huishia hapo hapo chuoni. Huko nyuma wasomi waliwahi kumwandikia waraka mkuu wa nchi kuhusu haki za binadamu. Leo yupo hata mmoja aliyemweleza Kikwete wazi wazi juu ya dhuluma mbali mbali zinazoendelea? Acheni woga! [​IMG] Wake up to your reputation!
   
Loading...