Wanayanga wenzangu tuwape moyo viongozi

GANA BANKS

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
598
853
Huwa sipendi kuficha jambo,...!

Nasikitishwa na UPUUZI wa baadhi ya watu yamkini hata miongoni mwetu.

Wana-Yanga...! Huwa tunatengeza mianya sisi wenyewe ya kushambuliwa na maadui zetu,...! Viongozi wetu hawalali Kwa ajili ya furaha yetu lakini Kuna wakati
tunawavunja moyo saàna...!

Nilishawaambia na nitawaambia Wana-Yanga tupokee kile kinachoamuliwa na uongozi wetu na siku zote tuwe nyuma ya maamuzi Yao, wao wanajua KULIKO sisi Kwa kuwa ndio watu wanaotuwakilisha ndani ya klabu...!

JIFUNZENI KWA HAYA WENZETU,...KWENYE KILA KITU NDANI YA KLABU YAO NI MARA CHACHE SANA KUWAONA HADHARANI WANAPONDA WACHEZAJI NA UONGOZI WAO.

Wewe jiulize wao Kila kukicha WANAPONDA bigirimana, makambo na hata kisinda.

Mlishawasikia Kila mara WANAPONDA AKPAN, OKWA, KAPAMA, WATARA, NA WENGINEO?

Mtu na akili zake timamu kakazana kulaumu kwann METACHA Karudishwa ndani ya klabu..! Mara oooh lile duka, nani ana uthibitisho wa METACHA kuwa duka..!? Au ni story za kwenye mabaraza ya KAHAWA na bao tu.!? Waungeni mkono viongozi wenu kwenye maamuzi Yao..! Kazi wanayofanya sio rahisi hata kidogo...! Ni kweli METACHA alitukosea lakini hayo ndio maisha ya mwanadamu duniani,...! Tunakosea ili tujifunze,..! Na tunajifunza Kwa MAKOSA,..! NI NANI MKAMILIFU KWENYE DUNIA HII.

Zaidi ya hapo Kwa Sasa mpira ni kazi kama kazi zingine,. Tusirudishane kwenye zama za YANGA ya akina Sunday Manara na wazee wetu wengine waliokuwa wanacheza mpira zaidi Kwa mapenzi....! Kama usajili wa METACHA UMEKUKERA, JADILI SAJILI ZINGINE BASI,...! YANGA HATUJASAJILI MCHEZAJI MMOJA DIRISHA HILI...!

Mjadili MUSONDA, DOUMBIA NA HATA MUDATHIR.

MSIMPE PRESHA METACHA, MWACHENI AFANYE KAZI YAKE,. MAADAM VIONGOZI WETU WAMEONA UMUHIMU WAKE KIASI CHA KUMRUDISHA,..!

na zaidi ya hapo tuwe nyuma yake, tayari anavaa jezi yenye nembo ya klabu yetu..! Huyo ni mchezaji wetu...!

Asante Kwa kunielewa,Nitarudi kulekebisha muandiko.

Pateni Ujumbe kwanza.

Screenshot_20230116-105336_Yanga%20SC.jpg
 
Ila viongozi wetu wanatukosea mashabiki na hawajali cos wao ndiyo wanatoa maamuzi,Kumrudisha Morrison na sasa Metacha, viongozi wanapuuza hisia za mashabiki sana na ni mbaya sana
 
Ila viongozi wetu wanatukosea mashabiki na hawajali cos wao ndiyo wanatoa maamuzi,Kumrudisha Morrison na sasa Metacha, viongozi wanapuuza hisia za mashabiki sana na ni mbaya sana
Mkuu wewe binafsi, Morison na metacha wamekukosea nini Hadi ulaumu uongozi kuwarudisha?
 
Mkuu wewe binafsi, Morison na metacha wamekukosea nini Hadi ulaumu uongozi kuwarudisha?
Kwa nini wachezaji kati ya wanne walioongezwa dirisha hili, watatu tuliambiwa kabisa tukae mkao wa kutangaziwa ingizo jipya, ila kwa Metacha ameingizwa kimya kimya?
 
Kumbe kuzunguka kote, kumbe hoja zako ni kuhusu kupondwa urejeo wa Metacha Mnata. Kigupi viongozi wa Yanga wanapenda kutuabisha mashabiki nakuonekana kama Manara alikuwa mkweli juu ya idadi ya wenye akili Yanga. Ishu ya Morrison, Manara, na sasa Metacha.
 
kadi yako namba ngap kwa timu unayoishabikia?
 
Back
Top Bottom