Wanayanga huku ni kujenga au kubomoa??!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanayanga huku ni kujenga au kubomoa??!!

Discussion in 'Sports' started by Sajenti, Jun 1, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Katika maandalizi ya kuandaa rasimu ya katiba Yanga na uchaguzi mkuu wa timu hiyo, wanachama wengi wa klabu hiyo wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujiandikisha kushiriki katika mkutano mkuu wa klabu hiyo. Hali hiyo inafuatia "pololo" au ofa iliyotolewa na anayejiita mfadhili mkuu wa klabu hiyo Yusufu Manji kuwa wale wote watakajitokeza kujiandikisha watalipiwa kiingilio kuangalia mechi ya Taifa Stars na Brazil tarehe 7 June 2010 katika uwanja wa Taifa.

  Najiuliza aina hii ya wanachama wanaosubiri kutimiza wajibu wao katika klabu yao mpaka mtu atoe ofa ya kuwaingiza mpirani ndio wavutike kwenda kujiandikisha kushiriki mkutano mkuu wana maana au faida yoyote kwa hiyo klabu?? Nadhani ifike wakati hizi klabu zetu zibadirike katika mifumo yao ya kuendesha hizi timu maana kuwa na kundi kubwa la watu wanaojiita wanachama wakati hawana manufaa kwa ustawi wa klabu ni kurudi nyuma katika karne hii tunayohitaji mageuzi katika medani ya soka Tanzania. Kifupi wameniudhi sana!!! Habari ndio hiyo!!!:becky::becky::becky:
   
Loading...