magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,336
Wana-MMU salaam,
Wanajamvi binadamu kila mmoja tumeumbwa kwa maumbile tofauti,tunatofautiana kila kitu,ingawa thamani yetu kama Binadamu ni ile ile bila kujali sura,hulka,tabia nk.
Wanawake wasiovutia kwenye macho mengi ya wanaume na hata wanawake wenzao ndiyo ambao huwa wanafanikiwa sana katika maisha. Iwe katika biashara,elimu,ujasiriamali nk.
Mtu atajiuliza kwanini wao ndo wanafanikiwa zaidi kuliko wenye mvuto!? Jibu ni rahisi.
Tangu utotoni sura zao zinapoanza kujitokeza huwa wanafanyiwa mizaha kulingana na sura zao. Kuna mazingira hata mzazi wa mtoto mwenye sura mbaya huingia katika mtego wa kuichukia sura ya bintie. Mama anaweza kumfokea mtoto wake wa kuzaa kwa kumueleza jinsi alivyo na sura ya kutisha!
Hali hiyo huwa inaendelea hata akiwa anacheza na watoto wenzie. Shuleni pia hali huwa ile ile. Tangu hapo mtoto huanza kujichukia,wanapofikia umri wa kuanza kujitambua,huwa wanaanza kutafuta namna ya kufidia huo udhaifu.
Hatua ambazo huwa wanachukua,ni kuelekeza nguvu katika kile wanachokifanya. Kama ni kusoma huwa wanasoma hasa,kama ni biashara wataisimamia ipasavyo. Kila kitu huwa wanafanya kwa bidii kama njia ya kufidia kile ambacho wanaamini kinawatenga na wengine.
Huwa waanamini wakifanikiwa kila mtu atawaheshimu. Tatizo lao wakishafanikiwa huwa wanajikuta wanakuwa watu wa visasi bila hata wao wenyewe kujua. Mafanikio yao huwapa jeuri isiyo na kipimo,ni wanyanyasaji sana wa watu walio chini yao. Wakibahatika kupata nafasi kubwa katika jamii,mwanamke wa aina hii ni hatari kwa anaowaongoza.
Pengine hata yanayoendelea kule Dodoma,huenda kuna mtu mkubwa aliye juu kwa sasa na amepitia madhila hayo ya kutengwa. Shida ya watu kama hao hawawezi kuondokana na hilo tatizo kwasababu hata wao huwa hawajui kama wanalipa visasi kwa yale watendayo.
Nawasilisha..!