Wanawake wawili wadakwa na kete 114 za bhangi

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,773
3,471
Mwanza. Wanawake wawili ni miongoni mwa watu zaidi ya 15 waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya mkoani Mwanza

Watu hao wamekamatwa wakijihusisha nadawa hizo ndani ya wiki moja kuanzia Febuari 6.

Habari zinasema wanawake hao wamekamatwa wilayani Magu wakiwa na kilo 114.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema watuhumiwa 11 wamekamatwa wilayani Nyamagana na Ilemela na kilo 57 za dawa za kulevya aina ya miraa na kete mbili zinazodaiwa kuwa ni heroin.

“Mtuhumiwa mwingine ambaye ni mfanyabiashara wa vipuri vya magari, alikamatwa eneo la Butimba akiwa na kete 240 ya dawa za kulevya zinazodaiwa kuwa ni heroin na ndunga mbili,” amesema.

Msangi amesema mtuhumiwa huyo alitaka kuzitumbukiza chooni dawa hizo ili kupoteza ushahidi, lakini polisi waliwahi kukata bomba.
 
Back
Top Bottom