Wanawake wanavyokaribia kutawala dunia

amygdala

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
1,082
Reaction score
997

Bi Hillary Clinton ndiye mwanamke wa kwanza kuteuliwa na chama kikubwa kuwania urais Marekani

Japo ni jambo ambalo linaamuliwa katika saa chache zijazo, ni jambo ambalo wengi wanasubiri kwa hamu na shauku kuu kuona iwapo litatilia.

Iwapo Bi Hillary Clinton atashinda kiti cha urais wa Marekani itakuwa ni mageuzi makubwa sana kwa Marekani na dunia nzima, na pia fahari kuu kwa wanawake.

Mwandishi wa BBC Katty Kay anachanganua:

Hii ni kwa sababu hili itamaanisha sasa shirika kuu la fedha duniani na mataifa matatu tajiri duniani yatakuwa yakiongozwa na wanawake.

hati inaendelea hivi: Uingereza Bi Theresa Mary May na Malkia Elizabeth, Ujerumani Bi Angela Merkel, na Bi Chistine Lagarde katika uongozi wa shirika la fedha duniani IMF.

Bi Theresa May, Waziri Mkuu wa Uingereza

Sasa katika orodha hiyo ongezea marais wa kike, wanawake wanaoongoza baadhi ya nchi zilizo na utawala wa kifalme na hata mawaziri wakuu wa kike, ndio utabainikiwa jinsi mambo yalivyobadilika katika safu ya uongozi iliyokuwa ikisheheni tu viongozi wa kiume miaka michache iliyopita!

Afrika kuna Ellen Johnson Sirleaf ambaye amekuwa rais wa Liberia. Amekuwa madarakani tangu 2006.

Bi Park Geun-hye, Rais wa Korea Kusini

Bi Park Geun-hye ndiye rais wa Korea Kusini. Amekuwa madarakani tangu 2013.

Bi Kolinda Grabar-Kitarović ni rais wa Croatia na amaekuwa madarakani tangu Februari mwaka jana.

Lakini je hilo lina uzito gani hasa katika minzani ya kuboresha maisha ya kila siku ya mwanadamu.

Kuna kauli zisemazo wanawake hawatakiani mema na mifano inatolewa ya baadhi ya taasisi zilizoongozwa na akina mama wakamavu, walioelimika vyema ... ambako haikuonekana bayana kuinua maisha ya wanawake wenzao kisera wala kiuchumi licha ya kuwa wengi wa walio maskini duniani ni wanawake, vijana na watoto.

Bi Sirleaf ameongoza Liberia kwa miaka kumi sasa

Hata hivyo utafiti mbali mbali uliofanywa na taasisi za kimataifa unaonesha kuwa wanawake wanapokuwa uongozini tatizo la mfumo dume hupungua , wasichana hupata motisha zaidi masomoni na katika kazi zao hata iwe ya ngazi ya chini kiasi gani.

Pia uongozi wa wanawake huendeleza sera za kutafuta suluhu za kidiplomasia kwa mizozo ya kisiasa kuliko kukimbilia vita - kwani wao ndio waathirika wa kwanza wakati amani inapovurugwa.

Zaidi ya hayo utafiti unaonesha ili mabadiliko ya kisawa sawa yafanyike, yakuboresha maisha ya wote kwa jumla ni sera za kuongeza idadi ya wanawake katika sekta zote za kimaisha zitekelezwe.

Malkia Elizabeth wa Uingereza

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Na sekta zinazopaswa kupewa kipa umbele kwa hilo ni katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kibiashara, fani za uandishi habari, udaktari, na hata katika jeshi.

Pia tafiti hizo zaonesha mwanapopewa fursa katika upande wa usomi, kutafuta maridhiano na kuwa kielelezo cha mifano miema wanawake wengi wako mstari wa mbele kuliko wanaaume ...bila kusahau majukumu yao ya a msingi ya kuwatunza waume zao, na kuwapa watoto ulezi bora

Wanawake wanavyokaribia kutawala dunia - BBC Swahili
 
Wakiwezeshwa wanaweza...

Muda si mrefu hatutasikia tena vita vya silaha bali vya kusutana kwa mipasho...

Ila kwakuwa maneno hayaui bora kusutana kuliko kuuana...
 

Michelle Batchelete ni Rais wa Chile, na Estonia (Jina gumu) ina rais mwanamke
 
ukweli ni kwamba tulitumia nguvu nyingi kuupindua utawala wa wanawake ila wao wanaurudisha kwa ubua.
 
ukweli ni kwamba tulitumia nguvu nyingi kuupindua utawala wa wanawake ila wao wanaurudisha kwa ubua.
aisee wanarud kwa kasi ya jet, yaan km christina fernandez na dilma rousef wangekuwepo wangekuwa wengi kweli
 
Huyo wa South Korea karibu wanamfukuza kazi.

Yule wa Brasil walishamfukuza kazi na sasa anasubiri kujibu kesi kwa Pilato.
 
Huyo wa South Korea karibu wanamfukuza kazi.

Yule wa Brasil walishamfukuza kazi na sasa anasubiri kujibu kesi kwa Pilato.
yule wa brazil alimletea sana figisu uncle SAM naona wakampangia mpango wa muda mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…