Unafikiri kulikuwa na upendo pale? we mtu kaletewa tu mke/mume bila kujuana wakakubali. Hawa mmoja mke alikuwa anavumilia tu hata akitendwa vipi? nakumbuka mke akipata kipigo au akirudi kwao kwa namna yoyote wazazi au ndugu wa mke walimrudisha kwa mumewe tena si kwa majadiliano ni amri sharti arudi. Ni uvumilivu tu wa aibu au mila ziliwafanya wanawake wabakie. Tumeshuhudia mitoto ya nje mingi tu, Kukaa kwenye ndoa kwa muda mrefu si kwamba kuna upendo na kuvunjika kwa ndoa si kwamba wanandoa hawakupendana, labda kuna kitu kimekosekana hapa kwa kizazi hiki.
nafikiri utofautishe enzi za mababu na mabibi na enzi zetu.hii ni karne ya 21 co karne ya kumi na. . . hata bible iko waz nyakat za mwisho watu watapenda pesa, na bible haisemi uongo hebu wacha tutimize maandiko kwan huwez pingana na bible. . . pesa ni sabuni ya roho. chezeya pesa wewe pesa ndo mambo yote. unaona bila pesa unavohangaika lait km ungelikuwa nazo wala huu uzi ucngekuwepo
Wanajisahau kuwa huwa wanawapendaga waliojiremba au waliopendeza hafu kuwapendezesha wapenzi wao wanang"aka sasa sijui tutapendezaje kama wasipotuwezesha, lol. Eti true love......true love bila kupendeza. bila mashamushamu aka.
Kwani ni wanaume wangapi wangefurahia kuoa wake wanaowazidi elimu au kipato? Kama wapo huwa wanahitaji penzi la muda mfupi tu sio ndoa. Kuna wanaume wengi tu anaweza akawa amevutiwa na wewe ila ukisema tu elimu yako anaanza kukuita dada. Wengine hajaribu hata classmates wenzie. Mi naona pande zote hii inahusu na huvunjwa tu pale penzi la kweli linapoonekana otherwise kuna wanaume na wanawake wengi wameoona kwa hizo sifa tu na kuwaacha wale waliowapenda ukweli.
Japokua mimi kwenye swali langu sijataja neno upendo,wacha nikuulize,ni wakati gani kati ya zamani na sasa upendo umeonekana kwenye uhusiano?
Kwani nyie mnashindwa kujipendezesha wenyewe?
To be honest ni sasa. Sasa watu hujichagulia wapenzi wao. Mambo ya kutodumu ni anaother mada ya kujadiliwa hapa.
Unajua upendo ni kitu gani?Kama ni sasa kwanini ndoa hazidumu,plz don't tell me tusijadili kutokudumu kwa sababu upendo ndo unasababisha ndoa idumu au isidumu.Kama upendo upo nyakati hizi kwanini ndoa hazidumu?
gfsonwin mkianzia wote chini, hiyo ni tofauti; tena mara nyingi mkija kufanikiwa wengi wa wanaume husahau mlipotoka na kutafuta vimodel kwamba ndio hadhi yao at that moment.
Lkn mwanamke akiwa juu, chances kubwa sana ya ndoa kuwa na matatizo. Too bad kila mtu anahitaji mapenzi lkn isingekuwa hivyo, kuliko kugamble looking for 1 understanding man among 10, bora kuwa mwenyewe!
Tunasaidiana. Hivi utajisikiaje mpenzio ndo akiwa anaprovide mahitaji? uanaume wako hapa utakuwa wapi? nonino?
Wewe ni kichwa cha familia bana hata bibilia inasema unatakiwa uwe juu kwa kila kitu for safe side.
Najua mtanibishia sana,lakini ukweli wa kile ninachokishuhudia na kinachotokea kinawatia hatiani. . . . .
Niliwahi kuwa na uhusiano wakati fulani na Luteni wa JW,lakini kabla uhusiano wangu ule na yule dada haujashika kasi niliamua kumwambia ukweli yule dada kunihusu,bahati nzuri sikua na elimu aliyokua akihitaji yule dada,na pia kingine ambacho sikua nacho ambacho alihitaji niwe nacho ni pesa,uhusiano wetu ulikufa siku ileile,usishangae nilivyosema bahati nzuri,we hujui kujua mtu ni wa hovyo mapema ni bahati,alinieleza wazi hawezi kuwa na mtu mwenye elimu kama yangu halafu asiekua na hela,nilicheka sana,wadada wa aina hii nimekutana nao wengi,wengine hawasemi lakini unajua tu . . . . . . Tangu mwaka uanze mpaka leo nimeshuhudia mahusiano kumi tofauti yakifa yangali machanga,na yamekufa baada ya wadada kugundua wanaume walionao,hawana hela wala elimu kubwa.
Lakini pia najua mahusiano zaidi ya matano ambayo yanaendelea lakini wanaume wale wamewadanganya wanawake kuhusu kipato na elimu.Je wanawake mnapenda uongo? . . . . . Ukweli ulio wazi ni kuwa,wanawake hawawataki wanaume kama mimi wasio na elimu wala pesa.Najua mtakuja na ubishi wenu hapa na maisha yenu ya mdomoni msiyoyaishi ya kudai eti mnataka mwanaume mwenye upendo wa dhati wakati mnajua ni uongo.
Mwanamke anataka mwanaume mwenye hela, elimu kubwa na sura kama ya mdoli.
Hayo ya upendo na kumjua Mungu ni uongo. Hebu nenda Love Connect (hua naiona kama chit-chat) uone kama sisi wa darasa la saba na tunaishi kwa vibarua kama tuna nafasi. Tukiacha mizaha ya love connect, Ukweli ndo huo, hayo ndo yanayotokea mitaani, ukija huku wanajidai nataka mwanaume mwenye upendo mengine mungu atatupa,ukikutana nae mtaani anakuangalia juu chini kisha anakuhoji elimu na kazi unayofanya,mkiachana unaona simu hapigi tena wakati kabla hajajua kuhusu hayo ya kazi na elimu,sms na simu mpaka zilikua kero(nina watu wa3 yamewatokea).
Mimi kwa mfano,sijazoea kudanganya,waliopata kukutana nami wanajua,ninakuambia ukweli,mimi ni darasa la saba,kama unasepa usepe,sina sababu ya kudanganya,mara niazime gari sijui nguo!
Nakuambia wazi nakaa uswazi,nyumba haina bafu,ukitaka kuoga unasubiri usiku,choo pasport size,huwezi tembea,niache atakaeona upendo ndo mpango mzima atakua nami.
Kama hujiamini utaishi maisha fake sana. . . . . . . . All an all wanawake 98% wanataka wanaume wenye hela na elimu kubwa,ila watu hawa wamegeuka kilio kwa akina dada baada ya hao jamaa kutokua waaminifu.
Huo ndio UKWELI hata mkibisha!Action speaks than words!!!!
mmmh! We mtoto unamajibu mazuri hebu ni PMHakuna raha katika mahusiano kama kuanza na mtu akiwa hana kitu alafu mkatafuta pamoja.
Cha msingi mmependana .. Elimu siku hizi zipo mpaka za watu wazima lolz, evening class za kumwaga n.k
Pesa mtatafuta pamoja.. Haya mambo ya kutaka kua na mtu sijui ana ma range, sijui apartment, mahela na upuuzi mwingine ni kujitafutia mabalaaa tu.. Tatizo huwaga hawasemi yakiwakuta.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
mmmh! We mtoto unamajibu mazuri hebu ni PM
Ukweli ni kwamba, wanawake wengi mimi included tunataka mwanaume ambaye anakupenda na he can take care of you, financially na kimawazo na kimtazamo; hivyo basi tungeprefer au tunadream kuwa awe na uwezo kukuzidi (kama wewe unao any), elimu/uelewa wa mambo kukuzidi n preferable hata akuzidi walau miaka 2.
Ukipata unaye mzidi hivyo vyote juu, hata kama unanpenda kiasi gani, kama uelewa wake mdogo ndoa huwa na shida sana. Nami nimeshashuhudia my friends ambao ndoa zimevunjika coz mwanaume hajiamini na kuamua kuwa physical just to prove yeye ndie man of the house.
I was in a sort of the same relationship, sikumzidi pesa, but elimu na mafanikio; siwezi rudia bora niwe peke yangu aisee!
Sikatai, kuna baadhi yetu tunakuwa na nyodo lkn ni wachache sana kuliko wanaume mnavyopenda kujiaminisha ktk story zenu kiasi kwamba mnaanza kujihami kwa ubabe usio na kichwa wala miguu.
Kuhitimisha nasema, wanawake hatupendi kudanganywa but tunahitaji mwanaume tunayeweza mtegemea!