Nkuruvi
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 623
- 647
Habari za leo wana JF?
Kama kichwa cha uzi huu kinavyosomeka, nataka kufahamu kuwa Je wanawake walio katika ndoa za Mitala (Polygamy) (Mme mmoja, Wake wengi) huingia katika ndoa hizo kwa hiari zao wenyewe au ni mazingira yanawalazimisha? Binafsi kwa jinsi ninavyo wafahamu wanawake, najua kuwa ni watu wenye wivu haswaa wa mapenzi, hasa inapokuwa na mahusiano ya Mume na Mke. Sasa najiuliza kuwa, Inawezekanaje mwanamke aridhie kwa hiari mwanamume amletee mwanamke mwingine ndani ya ndoa? Najua kuna sheria za kimila na za kidini, lakini swali langu la msingi linabaki pale pale, je ni kwa ridhaa zao au mazingira (aidha ya kidini, kimila au mfumo dume) unamlazimisha mwanamke kuingia kwenye ndoa za mitala). Karibuni tujadili….