Wanawake wa Tanga wako Juu - Truth be told

Kwanza, jamani waacheni dada zetu wa Kitanga. Ila ukweli unabakia Tanga kwenye suala la mapenzi hakuna sehemu inayofikia (ukiondoa Mombasa!) Tanga hakuna kitu kinaitwa mapenzi kuna kitu kinaitwa "mahaba". Mahaba ni fani iliyotulia na kurithishwa. Mwanamke wa Tanga hakupi mapenzi anakupa mahaba. Watu wengine ndio wanajaribu mapenzi. Wakati mapenzi watu wanapeana vyumbani mahaba yanaanza 12 asubuhi hadi usiku wa manane; kuanzia unapotoka Kazini, kurudi lunch hadi ukitoka kazini.

Kitu pekee wanachodai - na mtoa mada kakiweza vizuri - wewe mhudumie na usimbanie hiyo pesa. Tena wana uaminifu vile vile (loyalty) sijui kwanini! Kanuni yao - hudumia utahudumiwa!

Au mmesahau hadi wanawake wa Kipemba miaka michache tu iliyopita walilalamika "Wanaume zetu wakenda Tanga hawarudi!"

haaa nilisikia bbc swahili wale wapemba wanalalamika
 
Back
Top Bottom