Wanawake wa kiafrika wana inferiority complex?

mwanamke urembo.. kujiamini ni kitu ingine kabisa wala havina uhusiano mkuu

Hajui tofauti ya Uzuri,Urembo,na kujiamini kuwa ni vitu vitatu tofauti. Alafu usikute mtu kama huyu ndio wanakuwaga wakwanza awapo barabarani akaona mwanamke mzuri na mwenye urembo wa kupangiliwa ndiye uwa wa kwanza kugeuka na kuanza kumtamani...utawasikia daah mtoto mkali yule!!?...kasahau kuwa kinachomfanya ageuke na kumtanani yule mwanamke ghafla ni ule urembo wake,uzuri wake na mavazi aliyojipigilia. Ila akipita au akikutana na kuku wa kienyeji(demu wa kipili pili alafu wa Uswazi) utawasikia daah Demu m-baya huyu kama nini!!...hapo anasahau kuwa huyo Demu haijui Salon wala Urembo.

Hivi huyu mtoa mada hii anajuwa kuwa baadhi ya wanaume wanawapeleka wake/girl friends wao Salon na wanawalipia pesa kama laki tano au hata million moja for URembo service?
 

Naona mnafarijiana ujinga. Kwa taharifa yako mwanamke wa kiAfrika anajiamini sana na huyo mtoa mada hii analitambuwa hilo sana ila ameamua kufanya ligi na kufurahisha nafsi yake ila kwenye moyo wake anajuwa kuwa alichokiwakilisha hapa hakina mashiko na ameshindwa kukitetea kwa mantiki. Kama anasema au kuona kuwa Wanawake wa kiAfrika hawajiamini basi itakuwa wanawake wa Dunia mzima...maana wanawake wa Ulaya,Asia na America huko kote wanatumia Urembo.

Ndio maana nasema hoja ya rafiki yako haina mashiko. Huwezi kuwatenganisha wanawake na Urembo. Karibu tuendelee.
 

Attachments

  • image.jpg
    601.7 KB · Views: 131
  • image.jpg
    158.1 KB · Views: 135

Huku Kenya only natural women win miss KENYA.....wnaonyakua title ni walio na muonekano asili ya kiafrika kabisaa.....kama Lupita.....kwa hiyo hii ni weakness yenu watanzania.......namuunga mkono mleta mada.
 
Yuko njiani anakuja...ila siku nyingine ukiona topic kama hizi usisite kuniita maana ninampango wa kupunguza topic kama hizi hapa jukwaani kwa kuwaelimisha waleta hizi topic kwa lugha mzuri tu.

Nina mpango nimlete mwandani wangu umpambe harusi yangu
 
Huku Kenya only natural women win miss KENYA.....wnaonyakua title ni walio na muonekano asili ya kiafrika kabisaa.....kama Lupita.....kwa hiyo hii ni weakness yenu watanzania.......namuunga mkono mleta mada.

Huyo dada anayejibizana na mimi hawezi kujenga hoja inayoweza kukubalika na sehemu tofauti tofauti za Afrika ndio maana anajibu kwa kulinganisha yeye na wanawake wa dar na ndipo upeo wake ulipoishia. Ukimuuliza ni chakula gani au mavazi gani yanayotambulisha utaifa wake yeye atakwambia anavaa mavazi yanayopendeza kwa ajili ya urembo tu!!!!!!
Hao watu anaosema ni wachina na wazungu hawana tabia ya kudharau asili zao, wao hata wakifanya urembo unakuwa ni wa asili yao, ndio maana hata wahindi wanaenda saloon lakini mwisho wa yote utawatambua kwa uvaaji wao, rafudhi zao na chakula chao.
 

hajui mtoa mada bwana ila atakuwa kajifunza kupitia hii thread yake
 
Huku Kenya only natural women win miss KENYA.....wnaonyakua title ni walio na muonekano asili ya kiafrika kabisaa.....kama Lupita.....kwa hiyo hii ni weakness yenu watanzania.......namuunga mkono mleta mada.

Naona mnatiana ujinga tu na kufarijishana wenyewe kwa wenyewe…na mleta mada alivyo na akili fupi yaani ameshindwa hata kwenda kwenye google ili ahakikishe Je,ni kweli Miss Kenya wote walioshinda hilo taji walikuwa natura? Badala yake kaishia kukupa like. Haya twende kazi
…Haya hizo hapo ni picha za Miss Kenya 2014' akiwa kwenye weaving na siyo Natural hair kama mnavyodanganyana. Karibuni tuendelee
 

Naona sasa unakimbilia kwenye mavazi ya Taifa na chakula' kwani mimi ni waziri wa utamaduni na chakula? ha ha haaa
Yaani hata sijui unasimamia kitu gani. Hapo juu nimekuwekea picha za Miss Kenya 2014 akiwa kwenye weaving…kama hazifunguki naomba uende kwenye google na tizama mamiss wote wa Kenya kuanzia mwaka 2010 tu hadi leo.
Alafu nimekuuliza maswali kibao lakini hata moja ulilonijibu zaidi ya kunishambulia tu. Mkuu chutama chini ya meza watu wanaokusoma hapa wanakucheka maana tokea hii mada imeanza ujaleta fact yoyote zaidi ya hisia tu…cha ajabu umeshindwa hata kuleta picha moja tu ya mdada wa ki Bongo akiwa natural ili kuipa uzito hoja yako.

Mimi nimekuletea fact kibao zenye ushahidi wa kutosha ambao unaonesha ukweli ninao usimamia wa kuwa HUWEZI KUMTENGANISHA MWANAMKE NA UREMBO na siyo Bongo tu bali ni Dunia mzima. uko mtupu chutama chini ya meza watu wanakucheka. Hivi unajuwa kuwa mwanamke anaweza kwenda Salon na akaspend tshs million moja? Uko dunia gani mkuu?

Karibu tuendelee.
 

Ni kweli,sio tu ktk nyanja za urembo hata kielimu pia.Kinachonishangaza siku zote wasichana wamekua wakiongoza ktk ufaulu wa masomo yao ktk elimu za sekondari lakini bado mpaka leo utagundua kuna baadhi ya fani zina wanawake wachache sana...baadhi wa wanawake wamekua pia wakichagua fani kutokana na "aina" ya kazi..mfano,baadhi wanapenda kukaa kwenye maofisi so fani kama za engineering,architecture na nyingine zinahusisha kazi ktk mazingira zaidi ya ofisi zinapata watu wachache sana na sababu kubwa ni kwamba zinaonekana ni kazi za "kiume" na hata wanawake wenyewe wanatetea hilo.
Niliposafiri kwenda Ulaya,nilijifunza vitu tofauti sana kuhusu wanawake wa huku (hata wale waafrika wa huku)
Kwanza, darasani hamna mwanamke au mwanaume ktk uwasilishaji wa elimu au ktk tijihada za mwanafunzi kufanikiwa kufaulu,wote wapo sawa,hata katika maisha ya kawaida mwanamke na uhuru na ugumu wa mambo kama mwanaume tu.
Huku kwetu bado kuna baadhi ya maeneo kuna "upendeleo" wa kijinsia ambao wakati unasaidia wanawake wasiojiweza Pia unalemaza wale waliopata nafasi kuitendea haki.Ndio maana si ajabu kusikia mtu anasema "hii ngumu""huoni kama mimi mtoto wa kike" siwezi n.k. Mfano kuna wakati mtoto wa kike anapofaulu, anapongezwa sio ktk "jitihada" zake zilizomfikisha hapo, lakini, ni kwa sababu yeye ni "mwanamke aliyefaulu",hata ile kauli ya "mwanamke anaweza akiwezeshwa" pia ni tatizo.

Lakini nafikiri tatizo sio wanawake, ni Utamaduni wetu ndio umetufikisha hapa tulipo,mfano Kiafrika(au kitanzania) mwanaume siku zote anaonekana wa hadhi kama anaweza "kulisha" au "kutoa" kwa ajili ya familia yake,wakati wanamke anaonekana wa hadhi kama "ataolewa" atakua na watoto, "kupika" n.k...ndio maana si ajabu kuona mwanaume anasikia faraja kama yeye anatunza familia,hata kama mwanamke yupo tu(labda awe masikini).Na watoto wanakua na hii hali, na inaendelea hivyo hivyo....

Yapo mambo mengine kama mtoto wa kike kupewa hela nyingi akienda shule,Tatizo la mahusiano na ndoa za mapema zinazomkabili mtoto wa kike....mimba kuonekana kama ni "ugonjwa", ndoa kuonekana kama ni "sumu" kwa wanawake wanaosoma na wale walio-olewa kuona "shule" Sasa basi n.k

Nawasilisha!
 

Cha ajabu hata wanaume wa kiafrika wanavaa suti na taina yote hii ni tamaduni wa mzungu hata hayo magari mnayotumia na hizo sahani mnazokula ni utamaduni wa mzungu kama kitu hukipendi usiaminishe na wengine tafuta mtu unaye fanana wengine waache waendelee na maisha afterall hakuna mtu aliyekuja duniani kwa kwa ajili ya mtu mwingine ulikuja kivyako utaenda kivyako na dunia utaiacha so acha watu waishi wanavyopenda.
 
hajui mtoa mada bwana ila atakuwa kajifunza kupitia hii thread yake

Unaunga mkono hoja dhaifu za huyo mwenye unyonge wa moyoni!! Hivi mtu hadi kufikia kufanya make-up usoni au kuvaa nywere bandia si maana yake haupo kwenye level unayoitaka? Hivi nyie mnaovaa mawigi yanayofanana na nywele za wazungu kungekuwa na uwezekano wa kubadili nywele asili mngechagua kipilipili au za kizungu? Maana mtu ukivaa nywele zinazofanana na za watu wa asili nyingine maana yake umeona zako mbaya, nini msichoelewa?
Kujitambua ni mwanzo wa hekima.
 

Watu kama ninyi ndio mnaohusika na kashfa za ushoga, unavyosema acha watu waishi kama wanavyopenda si una maanisha hata kama wewe ni mwanaume wakipenda kukuingilia kinyume waachwe tu kwa kuwa wamependa. Au watu wakifanya mapenzi mbele ya watoto au hata barabarani mchana kweupe waachwe tu kwa kuwa wamependa.
Think big.
 

Ngumu sana kueleweka
 

LUPITA ....Ndiye the most beautiful black woman today...kushinda hao ma miss bla bla wanaopanua miguu ilmradi waitwe ma miss whatever....research za Western magazines zasema Lupita is the most beautiful na ukiangalia hata kule wanamlilia huku wakisema ni malkia wa kiafrika kweli.......yaani hata wazungu mnaohangaika kufanana nao inabidi mpaka wawaelezeni kua urembo sio kuvaa wigi na kujikoboa bali hata uasili na uafrika wako kuanzia nywele za shungi hadi ngozi nyeusi ni urembo pia....keep it real ......alamsiki!!.
 
Mleta mada ....pata bonge la heshima!!...."standing ovation".....yaitwa ukoloni wa kifikra....nawasilisha!
 
ukiona mwanaume mzima kakubali kuingiliwa na dume mwezanke ina maana kapenda na ni hiyari yake, kufanya mapenzi mbele ya watoto jaribu kufanya kama uko na sound mind otherwise utakuwa kichaa kufanya mapenzi mchana. mambo ya kuingilia maisha ya watu binafsi kuhusu mavazi au urembo ndio ninayozungumzia mimi, sipendi mwanaume anayevaa cheni na hereni basi natafuta asiyevaa simple. sio kutopenda kwangu ndio nieneze chuki kwa wengine. kuna watu wanapenda waume zao wawe warembo wavae hereni sasa unataka nianze kuwapiga vita kisa mimi sipendi. tafuta mtu wa kufanana nae wengine waache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…