Wanawake wa kiafrika wana inferiority complex?


Hivi mimi nazungumzia suala la mtu kwenda saloon kusukwa&kupakwa rangi au nazungumzia inferiority complex?
Tabia ya kuiga kwa wazungu ndio imekufanya uone kwamba kuweka nywele dawa au kuvaa wigi ni urembo sawa wanawake wa kibongo wanaoona wasipofanya ngono kinyume cha maumbile(kutoa tigo) ni kuonekana mshamba.
Kwa maelezo yako tu unaonekana wewe ni muathirika kisaikolojia na hayo mambo ya kujikataa huku ukiyapa jina la urembo. Inasikitisha sana.
 

Twende taratibu kijana,hii mada umeileta wewe so kubali kupata maoni tafauti tafauti na uyajengee hoja na si vioja.
Huo urembo wa kucha na nywele ambao unataka kuusogeza au kuutoa kwenye mada hii ndio huo huo uliokufanya ukaandika ulichoandika na kuleta hapa...angalia tena kwenye main post yako hapo juu utaona nywele na kucha umezitamka au kuziandika mara ngapi.

Nimekuambia hapa niwekee picha yoyote ya Miss Tanzania ambae ameshinda hilo taji bila ya kuwa na weaving kichwani na kucha za bandia hadi sasa ujaileta.

Pili nimekuambia kama First Lady wa Dunia(Mitchell Obama) ana weaving kichwani sembuse mwanamke wa Bongo au wanawake wa kiAfrika? Sasa kama u-natural unalipa mbona hatujawahi kuona Miss Tanzania au Miss World alieshinda taji hilo akiwa na nywele za kipili pili kichwani?

Na kama kushonea weaving au kuweka relaxer kichwani ni ushamba mbona First Lady anaeishi kwenye Dunia ya kwanza mbona anafanya huo Urembo? Au na yeye ni mshamba?

Mkuu,huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo. Karibu tuendelee.
 
Mtoa mada don't be over dramatic. Watu unaoweza kusema wanajikataa ni wale wanaotaka kujibadilisha jumla kwa kujichubua ili wawe wazungu koko tu basi!!!!

Kusuka rasta, kuweka weaving, kupaka make up (poda, wanja, lipstick etc.) na kutengeneza kucha ni urembo tu. Na urembo haumbadili mtu hata siku moja, bali unaongeza tu vionjo.

Ni sawa na kuweka sukari kwenye chai, royco kwenye mchuzi and so on. Ukiweka royco kwenye maharage hayabadiliki kuwa mchuzi wa nyama, wala ukiweka maziwa kwenye chai haibadiliki kuwa uji bali vinabaki kuwa vitu vile vile ila vyenye ladha zaidi.

Nakolezea hapo kwenye "LADHA ZAIDI" maana poda watu hawapaki wawe wazungu, wanapaka kukausha uso na kufunika mabaka labda yaliyotokana na chunusi.

Au we unaonaga wadada wote wanaopaka make-up wanawafanania wazungu?. Je hiyo make-up inambadili mtu? Chausiku atakuwa Marry kwakupaka poda na lipstick?NOPE!!!

So let women be women, msilazimishe mambo ambayo hayapo. Insecurities zipo na hilo linaeleweka lakini kusuka, kujipodoa kidogo na kutengeneza kucha has NOTHING to do with it!!!!

Alafu usiseme make-up na nywele "zinawafanya wajione sawa na wazungu" maana hauna uhakika kwamba wanajiona hivyo. Sema tu kama wewe unawaona sawa na wazungu if that's the case.Na hapo hamna atalaeweza kukubishia maana ni maoni yako binafsi.
 

Dada wewe sidhani kama ulielewa somo la ufahamu na ufupisho, yaani unaongea kwa mbwembwe nyingi lakini hakuna points.
Mwanzo wa uzi wangu nilisema kwamba inferiority complex ni tatizo la kutokujikubali kwa kuwaona wenzako ni bora kuliko wewe, na wewe ni mmoja ya watu hao, ndio maana bila aibu ukajilinganisha wewe na first lady michelle wa marekani,

kwanini hukujilinganisha na first lady wa Taifa lako? Au unaona kwamba u-marekani ni bora kuliko u-Tanzania? Hata hao unaowaita ma-miss wana akili za kujikataa kama wewe, ndio maana wanaona wakivaa nywele zinazofanana na za wazungu watakuwa wamekamilika kuliko kuwa na nywele zao za kipilipili.

Wewe jiulize ni kwanini mawigi yote yanafanana na nywele halisi za wazungu? Au uliwahi kuona kuna wigi zinazofanana na nywele zako za kipilipili? Wazungu wanajua tu kwamba waafrika wengi hawaipendi asili yao kwahiyo ili kupata uhakika wa soko wanatengeneza kile mnachoona bora ndio maana hata mitindo ya nguonazovaa zinaonesha namna mnavyowatukuza huku mkijikana mioyoni mwenu huku mkichukua hatua ya kujaribu kujifananisha nao kwa kisingizio cha urembo!!!

Kujishtukia ni mwanzo wa ukombozi.
 

Haya ni maneno ya mkosaji...alafu sijui unasimamia kitu gani. Kwanza umemsoma Lizzy hapo juu.?
Hivi ni nani kakuambia wanawake wa kiAfrika hawajiamini? Kwa maana hiyo na wanawake wa kizungu nao hawajiamini? Maana na wao wanaenda Salon kutafuta Urembo. Au kwa mzungu ni sawa ila kwa mwafrica hapana? Mkuu urembo wa kucha na nywele kwa mwanamke ni kama unavyoona tui la nazi likiwekwa kwenye samaki au kwenye wali...hii yote ni kukifanya chakula kiwe na radha mzuri' the same ilivyo kwa baadhi ya wanawake hapa Duniani wanapenda urembo ili kunogesha muonekano usio na mashaka.

Alafu unasema eti tunaiga wazungu!' Sasa kama wazungu hao hao wametuletea dini,mavazi,magari,simu,computer nk...unashangaa kitu gani kama tutaiga na urembo pia? Eti mamiss wana akili za kujikataa kama mimi...ar u sure na unachokiongea au ni kutaka ligi tu na wewe uonekane umejibu? Nimekuambia hapa kama u-natural ndio dili na ni mpango mzima mbona hatujawahi kuona Miss Tanzania au Miss world yeyote alieshinda hilo taji la urimbwende akiwa na nywele za kipili pili kichwani? Kama yupo tupia picha yake hapa tuione. Au ndio kusema wewe unaakili kubwa sana kushinda waandaaji wote wa haya mashindano ya Umiss hapa Tanzania na Duniani kote kwa ujumla? Au wewe unaakili sana kushinda Rais Obama aliyemruhusu mke wake kushonea weaving?

Hapa Bongo peke yake kila ukutanapo na wanawake watano sehemu yoyote ile basi wanne watakuwa wameshonewa weaving au misuko ya rasta...na ukikutana na wanawake kumi basi nane kati yao watakuwa na weaving au msuko wa rasta kichwani. Kama uamini maneno yangu naomba ufanye utafiti huu sasahivi ukianzia na hapo ulipo sasahivi.(kama uko Bongo)

Mkuu,chutama watu watakucheka...huwezi kumtenganisha mwanamke na Urembo.
 

Attachments

  • image.jpg
    544.4 KB · Views: 188
  • image.jpg
    506 KB · Views: 197
  • image.jpg
    498.7 KB · Views: 164
  • image.jpg
    575.4 KB · Views: 177
  • image.jpg
    536.6 KB · Views: 141

Kwani hujui kuwa saloon ni moja ya uvumbuzi wa mzungu? Yaani wewe nikiomba nikutofanishe na nani ntakufananisha teja ambaye akila unga au kujidunga sindano yenye dawa ya kulevya anajiona yuko katikati ya mitaa mikubwa ya ghorofa marekani akifanya anasa kumbe yupo kwa mtogole chini ya mfereji wa maji taka huku akiwa anejisaidia ndani ya suruali yake.
 
Last edited by a moderator:
Siku tukiona kwenye tv mzungu amevaa pichu kichani, waafrika tulivyowaajabu tutaiga. Kumbe huenda mvaaji alikuwa chizi
 
mwanamke urembo.. kujiamini ni kitu ingine kabisa wala havina uhusiano mkuu
 
Mwanapropaganda wewe chapa lapa! Umewasilisha hoja nzuri sana lakina naona huyu dada Milioni-hairs nahisi katika kuelewa mambo ana alama ya Z (Siyo F maana hii ina afadhali kidogo).Wewe unazungumzia issue kubwa yeye analeta hoja nyepesi.Mimi nimekuelewa na nakupa tano!
 

Pamoja sana mkuu.
 
Watu8 si umeitwa huku wewe uje uchangie muswadaaa?

tokea nianze kubrauzi jeiefu kwa redio kolu huwa napata tabu sana kuona notifikesheninz

hata hivyo hii mada mi naona imekaa kujadiliwa na wanawake wenyewe ndio inapendeza...
 
Last edited by a moderator:

Naona sasa umeishiwa hoja na badala yake unaleta vioja. Sawa Salon zilianzia kwa Wazungu...lakini Je,hao wazungu wamevumbua vitu vingapi ambavyo leo hii mimi na wewe tunavitumia? Au umeona Salon tu?

Hata hivyo nimekuuliza maswali kibao lakini hakuna hata moja ulilonijibu...zaidi ya wewe kutaka kunitoa nje ya mada.
Narudia tena...Huwezi kumtenganisha mwanamke na Urembo hata ufanye nini! Si Bongo, si Zambia,Si South Africa,si Kenya,
si Dubai,si India,Si Spain,si Germany,si Marekani na wala si Uganda huko kote na Dunia yote kwa ujumla wanawake wanapenda urembo"hasa wa nywele na kucha" ndio maana unaona kila kukicha wanachama wa Urembo wanazidi kuongezeka badala ya kupungua. Hapo sijakupeleka vijijini,wilayani,mikoani na kwenye majiji.

Usisahau kunijibu maswali yangu yote niliyokuuliza kwenye hii mada yako...kama huyaoni sema niyaandike tena.
 

Attachments

  • image.jpg
    396.1 KB · Views: 75
  • image.jpg
    599 KB · Views: 78
  • image.jpg
    460.2 KB · Views: 145
  • image.jpg
    492.9 KB · Views: 83
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…