Mwanapropaganda
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 4,235
- 2,512
Watu8 si umeitwa huku wewe uje uchangie muswadaaa?
KuUmizAna hukU kuSoma essAy niliAchA o level. RekoD i au diO tuIsikilize iliTuchaNgie
Pole sana Mwanapropaganda! Maana umeongea kwa hisia kali sana...lakini huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo.
Urembo"hasa wa nywele na kucha" kwa wanawake ni kama nature yao, si wanawake wa Asia,wa Ulaya au wa America...wengi wao wanapenda sana huu urembo wa nywele na kucha. Na hao wazungu uliowatolea mfano kwenye hii thread yako hao ndio watumiaji wakubwa sana wa nywele za bandia na kucha za bandia.
Hapo chini nakuwekea picha ya Mzungu akisukwa nywele za bandia na mchina akitengenezwa kucha za bandia. Narudia tena...huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo ila urembo usio wa mpangilio ni uchafu na ni hatari kwa afya ya muhusika.
Wewe huwezi kutofautisha kati ya inferioriyy complex na urembo.
Hata ukiweka picha za wazungu, wahindi au hata wachina huwezi kusema kwamba neno urembo kwao ni sawa na neno urembo kwa wanawake wa nchi za Afrika kama Tanzania, na wengi unaowaona wanajikoboa ni wenyeji wa ulaya wenye asili ya Afrika wanauonea aibu weusi wao, wewe kwa akili yako kuweka wigi ni urembo? Au kujichubua na kupiga make-up nako ni urembo? Kama ndio mbona urembo wote mwisho wake unaacha vielelezo kwamba muhusika alitaka kuonekana mzungu na si mjaruo.
Hao wahindi na wachina mbona urembo wao unaakisi utaifa wao na si uzungu?
Think big.
Mkuu, kusuka mitindo ya Rasta,kushonewa weaving, kusukwa pick&drop,make up na kubandika kucha ndio urembo na mwanamke yeyote akifanyiwa huduma hizo kwa mpangilio uonekana mrembo na mzuri. Narudia tena huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo. Na hizo picha nilizokuwekea hapo si za ulaya bali hiyo ni Bongo.
Karibu tuendelee
urembo is a good thing for them, but urembo uliozidi ndio mbaya
Urembo ni nini? Na urembo uliozidi upoje?
Mbona unaongea kwa kukariri tu? Hebu niambie tu maana ya urembo nijue unajua nini kuhusu. Yaani thread nzima umesoma ila hujaambulia kitu, na hata nilipokunukuu na kukujibu bado hujaelewa tu, au ndio tuseme iq ya watu wa kusini mwa jangwa la sahara ni ndogo kiasi cha kushindwa hata kuelewa neno moja kati ya kumi?
Hizo picha ulizoweka ya kwanza si mzungu, angalia vizuri.
Hata kama wanayafanya hayo, asili zao haziondoki, weupe wao unabaki kuwa weupe, na hata hizo nywere zinafanana na nywele zao halisi ndio maana nikasema maana ya urembo kwa mwanamke mzungu ni tofauti na kwenu ninyi, wao wanaikubali asili yao na hata lengo lao la kuweka make-up usoni sio waonekane wana asili nyingine kama ninyi mnavyodhani uzungu ni ujanja na uafrika ni uchafu.
Tulia kijana! Utapaliwa bure,twende taratibu. Eti nakariri? Nakariri nini? Kwahiyo hii mada uliyoimwaga hapa na wewe unakariri? Hizo picha unazozikataa hapa niliziweka kama fact kutokana na maudhui ya thread yako kwani ulifikiri wazungu na wachina hawaendi Salon kutengeneza nywele na kucha...so nilichokifanya mimi ni kukuletea ushahidi tu ili uone.
Tena nimekuletea picha za hapa hapa Bongo na sikutaka kukutafutia za kwenye google. Asikudanganye mtu,hata baadhi ya wanawake wa kizungu wanaikataa hasili yao ndio maana wanaenda kwenye masalon kwenda kujiongezea Urembo. Na hata wanawake wa kiafrica wakifanya haya mambo ya urembo hasili ya uafrika wao hauondoki kama ilivyo kwa wazungu na wahindi.
Huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo...karibu tuendelee.
Mwanapropaganda,unayafahamu mashindano ya Miss Tanzania? Kama jibu lako ni ndio...je umewahi kuona mshindi yeyote tokea kuanzishwa kwa mashindano haya amenyakuwa hilo taji la Miss Tanzania akiwa na nywele natura kichwani achilia mbali kucha natural?
Nasubiri jibu...karibu tuendelee.
Kama kuna wazungu wanakataa asili yao na kwenda saloon kujiongeza, iwe kweli au si kweli ila kiufupi ni kwamba asili yao na urembo wao hawauringanishi na wa kwenu.
Wao wanajiremba ila hawapotezi asili yao, hawajichubui, hawatumii mikogo ya kiafrika wakiwa wanatembea, kuketi au hata wakati wa kuzungumza.
Wewe unakazania urembo wa saloon na kucha tu wakati mimi nazungumzia inferiority complex.
Hayo mashindano yameingia nchini kwa sababu ile ile tu niliyoisema yaani inferiority complex, kama mnfekuwa mnajidhamini msingekubali kuongozwa na mawazo ya weuoe kwa kutembezwa uchi jukwaani.